Kwa mujibu wa maelezo yao ni kwamba mpango unasema serikali itakuwa inatenga 35% ya mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ambapo Zitto amesema imetenga 0%. Mwigulu akasema mpango unasema ni 35% ya bajeti, Zitto akamwambia achana na huo mpango wako wenye kiingereza cha kuungaunga so akamfungulia mpango wa kiswahili ambao ndio uliopitishwa na bunge.........Nchemba akagwaya
Nchemba kama hakuuelewa huo mpango wa maendeleo namshauri aonane na Dr Mpango atamwelewesha vizuri. Serikali iliji-commit kutenga 35% ya mapatoo yake ya ndani kila mwaka for 5 years. Na sababu kubwa ya kutaka hiyo 35% itoke ndani ni ili kuepukana na tatizo la utegemezi wa wahisani ambao mara nyingi wanatoa kiasi tofauti na walichoahidi au/na wanatoa hela kwa kuchelewa. Hivyo ikaonekana ili mpango huo usisue-sue basi 35% itokane na makusanyo ya ndani.
Sasa Nchemba analeta ngonjera za first class! Na CCM wakumbuke hii ni bajeti ya pili, wamebakiwa na bajeti 3 tu kufikia tamati ya huo mpango wa miaka mitano (2011-16). So far wamefanya nothing, na wakiendelea kujitetea kwa kueleza marks za darasani watajikuta muda umeisha bila kufanya chochote. They've messed up MKUKUTA, they are off-target za vision 2025 na huu mpango wa maendeleo nao unaelekea huko huko kuzimu.