Zitto na Hamphrey Polepole wauponda UKAWA

Zitto na Hamphrey Polepole wauponda UKAWA

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,051
MUUNGANO wa vyama vinne vinavyoshirikiana katika Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), umejikuta ukikumbana na upinzani unaoshika kasi nje ya muungano huo, wakati ukikabiliana na sintofahamu inayoendelea ndani yake, huku viongozi wake wakilalamika kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe.

Juzi, Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Hamphrey Polepole, badala ya kuunga mkono umoja huo unaojinasibu kutetea Rasimu ya Katiba iliyotengenezwa na Tume hiyo, alielezea kushangazwa na Chadema kukubali kuondoka kwa misingi ya kupambana na rushwa, na kumtangaza mgombea urais, ambaye kilimtuhumu kwa kadhia hiyo.

Mbali na Polepole, Kiongozi Mkuu wa ACT –Wazalendo, Kabwe Zitto, akizungumza mkoani Morogoro, alitaka Watanzania waunge mkono wagombea wa chama hicho, kwa madai kuwa vyama vinavyounda Ukawa, vimebadilika ghafla kutoka kuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge na kugeuka kukumbatia ufisadi, huku CCM ikituhumu umoja huo kwa kughushi kadi zake.

Polepole Akizungumza kupitia kipindi cha ‘Mada Moto’ kilichorushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten juzi usiku, Polepole alisema chama hicho hakikupaswa kukimbilia kumpokea Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, kwa kuwa kilitumia kete ya umaarufu wake kisiasa kumshutumu kuwa hafai.

Alisema, Chadema ni taasisi ambayo ina misingi yake, hakuna mtu anayepaswa kuivuruga kwa nia ya kutaka kumfanya mtu mmoja anufaike na chama hicho.

“Chadema wana misingi yao ambayo hakuna mtu anayepaswa kuivuruga. Kwa maana nyingine misingi hiyo ni sawa na imani ambayo haibadiliki kutoka katika msingi wake, hivyo walichofanya nawashangaa,” alisema.

Mjumbe huyo wa Tume hiyo ambayo ilikuwa chini ya uenyekiti wa Jaji mstaafu, Joseph Warioba, alisema hata upande wa Lowassa na wana Chadema wanapaswa kujiuliza iwapo ujio wake ndani ya chama hicho una manufaa mapana yenye malengo ya kuendeleza misingi iliyowekwa au wanafikiria kushika dola pekee.
Alisema waziri mkuu huyo wa zamani amekaribishwa Chadema ambacho kinaunda Ukawa, akiwa tayari ameshiriki kuiunga mkono na kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa wananchi, wakati Ukawa wenyewe wanaipinga, hivyo kilichompeleka ni msukumo wa kuingia madarakani na siyo Katiba inayotetewa na umoja huo.

Alihoji kama kweli kifikra mgombea huyo anarandana na mawazo ya wale waliomkaribisha, wakati wao wamekuwa wakihubiri kile kilichomo ndani ya Katiba Iliyopendekezwa na Tume, ambayo msimamo wake ni serikali tatu wakati Lowassa alipiga kura na kuunga mkono uwepo wa serikali mbili.

“Ukisikiliza wanasema tunataka kuing’oa CCM, hiyo ndio mada kubwa. Huyu ndio anaijua CCM, mimi nauliza hivi sisi tuna mtindo wetu wa kufikiri, tuna mtindo wa kufanya mambo yetu ili yaende? Hivi leo mnampata mtu mwingine ana itikadi nyingine anakuja, kiitikadi hilo haliwezekani. “Hivi unadhani Ukawa ina uhalali wa kusema inapambana na ufisadi ilhali inafahamu Lowassa, Membe na wengine walisimamishwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kufanya rafu? Hivi ninyi mna uhalali leo tena wa kumyooshea mtu kidole?” Alihoji.

Alisema aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ana siri nzito moyoni kwa kuwa haiwezekani kiongozi huyo kuwa miongoni mwa waliomkaribisha Lowassa na siku chache akaamua kujiondoa kabisa madarakani.

“Mimi nasema, na nataka niwaambie waandishi wa habari mheshimiwa Lipumba ana siri kubwa...”alisema mjumbe huyo ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa nchini.

Zitto Naye
Zitto akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Jimbo la Morogoro Mjini, mkoani humo juzi aliwaomba Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Morogoro kuunga mkono chama chake kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais ili kipate uwakilishi kwa lengo la kuwatetea watu wanyonge.

Alisema ACT-Wazalendo, ndio chama kilichobaki katika kuendelea na misingi yake imara ya kutetea wanyonge, baada ya kutokea mtikisiko wa vyama vya siasa vya upinzani, hasa vinavyounda Ukawa.
Kwa mujibu wa Zitto, vyama hivyo vya Ukawa vimebadilika ghafla kutoka mstari wa mbele wa kutetea watu wanyonge, na kugeuka kukumbatia ufisadi, kinyume na msimamo wao wa awali na matarajio ya wananchi walio wengi.

“Ndugu wananchi wa manispaa ya Morogoro, chama hiki sasa ndiyo kimbilio lenu, hakijabadili misingi yake iliyojiwekea ya kupambana na ufisadi... Tunalo azimio la Tabora tulilohuisha kutokana na Azimio la Arusha na moja ni kila kiongozi lazima atangaze kwa kuorodhesha mali yake,” alisema Zitto.

CHANZO:Habarileo.

 
Don't worry about the old version.they have to think about them self.


Swissme
 
Chadema ni chama cha kifisadi na wala rushwa ni kundi la watu wanaofanya biashara kupitia siasa hawafai kama gonjwa la ukimwi.
Sawa mama yangu hila kila kila kitu kina mwanzo na mwisho.like you now your so old mom.

swissme
 
HAWA VIUMBE NI WA KUOGOPA WAOGOPWE WA PUUZWE THEY CANT COMPETE WITH MOVEMENT FOR CHANGES WALICHOAMBULIA WALE TARATIBUii
 
HP alishasema yeye ni mwana-CCM, na Zitto anafahamika kwamba ni msaliti. Sasa unategemea vipi kupata nyama ya nguruwe, kwenye makambi ya kisabato??
 
Bavicha guys and ukawa fans your leaders might be wrong learn to think for yourself.
 
Katika hali isiyo yakawaida japoa nakuambiwa nawahusika kwamba tuko kwenye maandalizi yakuwasha mtambo wa gesi ila ukweli uu hapa;:
Kuna bwana mmoja family frnd ambaye ni meneja Tanesco mkoa flani hapa nchini sitautaja kwasababu za usalama wake .alikuwa akiongea na mzee wa kwetu katika mazungumzo ya kawaida jamaa alifunguka na kusema huu sio mgao wala cjui kutest mitambo ya gesi hii ni oder kutoka juu magogoni kwamba kuhakikisha Taarifa za habari aziwafikii wananch wengi ambapo mida ya habari kuonyeshwa kwenye Tv umeme unatakiwa usiwepo karibu sehemu zote nchini, na umeme uwashwe sa tano usiku mpka sa nane mchana. Au muda mwingine sa tano usiku alafu ukatwe sa kumi na mbili asubuhi yote haya ni kwaajili taarifa za ukawa zisiwafikie wananchi kwa asilimia kubwa,..


Kweli nilichukua yale maneno ya jamaa nikatafakari nikachanganya na zangu nikaunga hizi dots nikajua hapa kuna ukweli 100%
Angalia umeme ulianza kukatwa lini.. Ni siku lowasa anaonyweshwa live kujiunga na chadema.
baba riz alisema ataakikisha wanashinda huu uchaguzi kwa njia yoyote ile na namna yoyote ile na uhakika wakushinda wanao na watashinda kwa mbinu yoyote ile.. Nikachanganya na dots na nape kwamba watashinda kwa goli la mkono, kwa dots hzo unaweza ukaona hili jambo ni la kweli tupu.

Sasa UKAWA kuweni makini ku rafu inaenda kuchezeka na imeshaaanza. BY Lupamba'sgrandson
 
Kutetea ufisadi na mafisadi inatakiwa uwe na roho ya kifisadi pole vijana wa mafisadi kwani huoni aibu kutetea mafisadi papa?
wewe humtetei magufuli?
mwaka huu lazima mtataga
zit na polepole wote ccm so hakuna cha ajabu hapo
 
UKAWA wategemee nini cha muhimu kutoka kwa MWana CCM polepole anayeMuhofu Lowasa ambaye yeye polepole alipiga DEBE sana Ili Lowasa AKATWE NA chama chake cha CCM na AKAKATWA KWA kutumia mbinu za kucheza RAFU za JK ?

Na Ukawa wategemee nini cha Muhimu kutoka kwa ZZK ALIyetimuliwa CDM Na kukataliwa chama chake cha ACT Kuijiunga na UKAWA? Mti wenye Matunda siku zote Hupigwa MAwe...

Polepole kwa yeye kuwapo CCM anategemea MAbadiliko gani kwa manufaa ya mamilioni ya watanzania, zaidi ya yeye Kulisha Tumbo Lake?..
 
Ufisadi upo wapi hapa? Miaka yote munakipa ridha yakuongoza inchi ccm, hamuoni uchafu wake. Leo lowasa kujs UKAWA, ninongwa. Munaongopa nini nie ma ccm? Mwaka huu ni wakihama kwa ccm.
 
Polepole ni ccm, unafikiri ata tetea UKAWA? Hizi longolongo za watu wa ccm kujifanya una upenda UKAWA zinatoka wapi?
 
Kutetea ufisadi na mafisadi inatakiwa uwe na roho ya kifisadi pole vijana wa mafisadi kwani huoni aibu kutetea mafisadi papa?

Hivi ni lini ccm walipiga vita ufisadi? Ccm ndiyo chama namba moja kinachotetea na kukumbatia mafisadi. Hebu tueleze hapa, kuanzia Richmond, meremeta, escrow na nyingine nyingi, nani alishafikishwa Mahakamani? Stupid guy.!
 
Back
Top Bottom