Zitto na Hamphrey Polepole wauponda UKAWA

Zitto na Hamphrey Polepole wauponda UKAWA

Msemaji Ukweli niwahakikishie tu kuwa hata muongee vipi hamuwezi kuwabadili watanzania. tunafahamu fik ZZK na HP wanatumiwa kuhujumu UKAWA na ndio maana wao wanamshambulia mtu badala ya taasisi. Wao akina HP na ZZK hasa HP kama wanao ushahidi wenye mashiko walipaswa kufungua mashtaka kwani mahakama pekee ndiyo inayomhukumu mtu. Tuhuma peke yake hazitoshi kutushawishi tumkatae EL kwani hata JK alipokua anagombea wapo watu walimtuhumu na bado tukampa kura. Nadhani hivi sasa msihangaike kukimbilia kwenye vyombo vya habari kumchafua mgombea wetu. enendeni kwenye walipo wananchi mkamwage sera zenu na muwashawishi wananchi. Tumekwisha amua watanzania kuwa wakati wa mabadiliko ni huu na atakayefanikisha mabadiliko haya ni EL. HATUDANGANYIKI KAMWE. OKTOBA 25 KURA KWA UKAWA . TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA
MUUNGANO wa vyama vinne vinavyoshirikiana katika Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), umejikuta ukikumbana na upinzani unaoshika kasi nje ya muungano huo, wakati ukikabiliana na sintofahamu inayoendelea ndani yake, huku viongozi wake wakilalamika kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe.

Juzi, Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Hamphrey Polepole, badala ya kuunga mkono umoja huo unaojinasibu kutetea Rasimu ya Katiba iliyotengenezwa na Tume hiyo, alielezea kushangazwa na Chadema kukubali kuondoka kwa misingi ya kupambana na rushwa, na kumtangaza mgombea urais, ambaye kilimtuhumu kwa kadhia hiyo.

Mbali na Polepole, Kiongozi Mkuu wa ACT –Wazalendo, Kabwe Zitto, akizungumza mkoani Morogoro, alitaka Watanzania waunge mkono wagombea wa chama hicho, kwa madai kuwa vyama vinavyounda Ukawa, vimebadilika ghafla kutoka kuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge na kugeuka kukumbatia ufisadi, huku CCM ikituhumu umoja huo kwa kughushi kadi zake.

Polepole Akizungumza kupitia kipindi cha ‘Mada Moto’ kilichorushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten juzi usiku, Polepole alisema chama hicho hakikupaswa kukimbilia kumpokea Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, kwa kuwa kilitumia kete ya umaarufu wake kisiasa kumshutumu kuwa hafai.

Alisema, Chadema ni taasisi ambayo ina misingi yake, hakuna mtu anayepaswa kuivuruga kwa nia ya kutaka kumfanya mtu mmoja anufaike na chama hicho.

“Chadema wana misingi yao ambayo hakuna mtu anayepaswa kuivuruga. Kwa maana nyingine misingi hiyo ni sawa na imani ambayo haibadiliki kutoka katika msingi wake, hivyo walichofanya nawashangaa,” alisema.

Mjumbe huyo wa Tume hiyo ambayo ilikuwa chini ya uenyekiti wa Jaji mstaafu, Joseph Warioba, alisema hata upande wa Lowassa na wana Chadema wanapaswa kujiuliza iwapo ujio wake ndani ya chama hicho una manufaa mapana yenye malengo ya kuendeleza misingi iliyowekwa au wanafikiria kushika dola pekee.
Alisema waziri mkuu huyo wa zamani amekaribishwa Chadema ambacho kinaunda Ukawa, akiwa tayari ameshiriki kuiunga mkono na kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa wananchi, wakati Ukawa wenyewe wanaipinga, hivyo kilichompeleka ni msukumo wa kuingia madarakani na siyo Katiba inayotetewa na umoja huo.

Alihoji kama kweli kifikra mgombea huyo anarandana na mawazo ya wale waliomkaribisha, wakati wao wamekuwa wakihubiri kile kilichomo ndani ya Katiba Iliyopendekezwa na Tume, ambayo msimamo wake ni serikali tatu wakati Lowassa alipiga kura na kuunga mkono uwepo wa serikali mbili.

“Ukisikiliza wanasema tunataka kuing’oa CCM, hiyo ndio mada kubwa. Huyu ndio anaijua CCM, mimi nauliza hivi sisi tuna mtindo wetu wa kufikiri, tuna mtindo wa kufanya mambo yetu ili yaende? Hivi leo mnampata mtu mwingine ana itikadi nyingine anakuja, kiitikadi hilo haliwezekani. “Hivi unadhani Ukawa ina uhalali wa kusema inapambana na ufisadi ilhali inafahamu Lowassa, Membe na wengine walisimamishwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kufanya rafu? Hivi ninyi mna uhalali leo tena wa kumyooshea mtu kidole?” Alihoji.

Alisema aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ana siri nzito moyoni kwa kuwa haiwezekani kiongozi huyo kuwa miongoni mwa waliomkaribisha Lowassa na siku chache akaamua kujiondoa kabisa madarakani.

“Mimi nasema, na nataka niwaambie waandishi wa habari mheshimiwa Lipumba ana siri kubwa...”alisema mjumbe huyo ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa nchini.

Zitto Naye
Zitto akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Jimbo la Morogoro Mjini, mkoani humo juzi aliwaomba Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Morogoro kuunga mkono chama chake kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais ili kipate uwakilishi kwa lengo la kuwatetea watu wanyonge.

Alisema ACT-Wazalendo, ndio chama kilichobaki katika kuendelea na misingi yake imara ya kutetea wanyonge, baada ya kutokea mtikisiko wa vyama vya siasa vya upinzani, hasa vinavyounda Ukawa.
Kwa mujibu wa Zitto, vyama hivyo vya Ukawa vimebadilika ghafla kutoka mstari wa mbele wa kutetea watu wanyonge, na kugeuka kukumbatia ufisadi, kinyume na msimamo wao wa awali na matarajio ya wananchi walio wengi.

“Ndugu wananchi wa manispaa ya Morogoro, chama hiki sasa ndiyo kimbilio lenu, hakijabadili misingi yake iliyojiwekea ya kupambana na ufisadi... Tunalo azimio la Tabora tulilohuisha kutokana na Azimio la Arusha na moja ni kila kiongozi lazima atangaze kwa kuorodhesha mali yake,” alisema Zitto.

CHANZO:Habarileo.

 
Back
Top Bottom