Naomba wahusika Uzi huu usiunganishwe na nyuzi nyingine zinazo husiana na msamaha kuhusu Zitto lengo ni kufikisha ujumbe.
Ndugu zangu wana jukwaa poleni na majukumu.
Nasema tumsamehe, tulikula naye nasema tumsamehe, Tumetoka naye Mbali nasema tumsamehe, Hiki ndo kipimo cha uungwana wetu nasema Tumsamehe, Chondechonde tusiwape faida wabaya wetu nasema tumsamehe, Hii ni kamba anavuta tunavuta matokeo yake itakatika, nasema tumsamehe.
Ndugu yangu Mbowe umemtoa Mbali kijana huyu, mwenyewe pia amesema hivyo mara kadhaa,naomba tumsamehe, nasema 7 mara 70 tumsamehe, chondechonde babangu mzee wangu Dk Slaa nasema ni mwenzetu tumsamehe,tukumbuke wema wake. Tuwaonee huruma watanzania walio jawa tumaini, uungwana ni vitendo nasema tumsamehe Mandela pamoja na kufungwa miaka 27 nakutemewa mate kwenye kikombe chake cha uji, na kila aina ya mabaya yasiyo stahiki kufanyiwa na binadamu lakini aliwasamehe Makaburu tena msamaha wa kweli. nasema Tumuenzi Mzee wetu Mandela kwa kwa kumsamehe Zitto.
Nasema tumsamehe pasipo masharti, pasipo kujali itikadi zetu , neno moja tu nasema tumsamehe, nasema tukimsamehe naamini aweza kuwa kiongozi mwema na muadilifu,mwaminifu na akawa mfano wa kuigwa. Wabaya wetu wanacheka wana furahi a tunavyo vuana nguo mitaani, wanacheka wanasema kimenuka, wabaya wetu sasa wamejazana baa wanakesha huku wakishikana mikono na kutosi wanasema safi sana, chonde tusiwape ushindi wabaya.
Nasali usiku kucha nasema Mungu inusuru Chadema na watanzania, Mh Mbowe tunatambuwa vyema mmewekeza nguvu,mali na kila namna ya kukijenga chama, lakini jambo kubwa nalo ni hili la watanzanini walio wekeza matumaini yao kuwa chadema ndo mkombozi, pia wako watanzania wanao amini kuwa Keki ya Taifa wataila kupitia Chadema, tuwaonee huruma. Asubuhi kunakucha naomba tuite vyombo vya habari tusiseme mengi bali neno moja tu kuwa tumemsamehe mwezetu tena kwa msamaha wa kweli, Watanzania watafurahi wakisikia tumemsamehe Mh Zitto.
Zitto si mwizi, si jambazi, si mkwapuaji,si kibaka nasema tumsamehe,tena pasipo kuhesebu makosa yake wala umri wa makosa yake, ni mwanzetu ni kijana wetu amejikwaa, alilpotea, tumrudishe kundini tena tumwandalie Karamu tule naye tunywe naye tumkumbatie tena hadhara, wabaya wetu waone kuwa tumemsamehe mwenzetu na tunampenda. Mh Tundu Lissu na Mh Myika na wengine wote nasema Tumsamehe kwa moyo wa dhati tuweke masilahi ya taifa mbele.
Hakika watanzania wenye mapenzi mema na Chama hata wasio wanachama watafurahi kusikia au kuona tukimsamehe mwenzetu, yatupasa kuamini kuwa naye ni binadamu anastahiki kusamehewa, katu hatutolaumiwa kwa msamaha huu kwa mwenzetu. Chonde chonde, kazi iliyofanyika kuijenga chadema nikubwa kuliko, ya kutaka kuibomoa inayofanyika sasa.
NB
Namalizia kwa kusema katika kutatua tatizo unaweza kusababisha tatizo lingine likawa kubwa kuliko lile la awali, lakini pia tukumbuke katika nia njema kabisa ya kutenda mema makosa yanaweza kufanyika, tutangulize umakini katika utatuzi wa jambo hili, lakini pia tutangulize umakini ktika ujenzi wa taifa letu.
Mungu ibariki Chadema Mungu ibariki Tanzania