Kitu ambacho CHADEMA hakitaruhusu kutokea ni kuunga mkono mgombea urais wa ACT WAZALENDO.nilitabiri hii na lazima itimie kuwa Membe to Act then Act na Chadema mezani halafu kidedea atakuwa ni BM kuwania katika tiketi ya muungano wa upinzani....ila mtakuwa mmemsaliti Lissu.
Kamanda Membe atatueleza mengi siku za usoni na ana kazi yake kubwa upinzani.Na Mwandishi Wetu, Kilwa
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa Benard Membe kujiunga na upinzani rasmi hapa nchini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa, Zitto alisema mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge na waziri wa wizara nyeti hapa nchini ana fursa ya kuunganisha Watanzania wenye kiu ya mabadiliko kupitia vyama mbadala vya siasa.
"Ndugu yangu Benard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM. Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko. Ni hatua sahihi.
"Hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala ili kuwapa Watanzania Mabadiliko wanayoyataka," alisema.
Kiongozi huyo wa ACT ambaye yuko katika ziara ya kichama ya mikutano ya ndani Kusini mwa Tanzania, alisema anaelewa mwanasiasa huyo bado anapambana kubaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini muda huu anahitajika zaidi kwenye upinzani.
Membe, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini, alifukuzwa uanachama wake CCM miezi michache iliyopita na hali yake kwa sasa iko kwenye sintofahamu.
Akizungumza na redio moja ya kimataifa hivi karibuni, Membe alisema ingawa kwa sasa bado anaangalia hatma yake ndani ya CCM, upo uwezekano wa kuwania Urais kupitia vyama vingine mbadala.
Lakini, katika mkutano huo wa Kilwa; Kusini mwa Tanzania anakotokea Membe, Zitto alisema historia itamhukumu vibaya mwanasiasa huyo endapo hatafanya uamuzi wa kujiunga na upinzani sasa.
"Mimi najua Membe anaipenda Tanzania na ni Mwana demokrasia.
Adhihirishe mapenzi yake kwa nchi yetu kwa kuongeza nguvu wa vyama mbadala.
"Kama kuna kosa la uhaini basi itakuwa ni kwa Membe kutofanya maamuzi ya kuwatumikia Watanzania nje ya CCM. Ninamsihi kuwa afanye tafakari na kufanya maamuzi sahihi na wananchi," alisema Zitto huku akishangiliwa na umati uliohudhuria mkutano huo.
Membe amegeuka kuwa mmoja wa wakosoaji wa utawala wa Rais John Magufuli, akikosoa hadharani mambo anayodhani hayako sawa kiutawala.
Ukosoaji huo umemjengea umashuhuri mkubwa kiasi kwamba sasa anatajwa kuwa mmoja wa wanasiasa wanaotajwa kuweza kuwania Urais wa Tanzania kupitia upinzani ( vyama mbadala) mwezi Oktoba mwaka huu.
Zitto anaendelea na ziara yake ya mikoa ya Kusini.
Mwisho
Chadema hawawezi kumkubali membe hata iweje,huku wao wana chaguo la Mbowe,lissu au Nyalandunilitabiri hii na lazima itimie kuwa Membe to Act then Act na Chadema mezani halafu kidedea atakuwa ni BM kuwania katika tiketi ya muungano wa upinzani....ila mtakuwa mmemsaliti Lissu.
Ndio maana wakaitwa wapinzani njaa hata mbowe na lisu walimuita lowasa na sumaye kila jina baya halafu wa kawasafisha na lowasa akawa mgombea uraisi, Tanzania hakuna wapinzani ni wachumia tumbo tuZitto Mwaka 2015 alikuwa mtu wa kwanza kumsema Membe juu ya ufisadi wa pesa za LIBYA alipotangaza kugombea kupitia ccm leo anamsafisha! shame.
Membe hawezi kutoboa na uwenda akauzika upinzani zaidi ya fisadi lowassa alivyofanya.
Katika siasa hamna adui wa kudumu au rafiki wakudumu kichopo ni maslahi ya kudumu......kwahiyo hiyo sio issueZitto Mwaka 2015 alikuwa mtu wa kwanza kumsema Membe juu ya ufisadi wa pesa za LIBYA alipotangaza kugombea kupitia ccm leo anamsafisha! shame.
Membe hawezi kutoboa na uwenda akauzika upinzani zaidi ya fisadi lowassa alivyofanya.
This is well calculated by chadema! Hawana mbavu za kupimana na jpm, wao watamteua lissu ila lisu atajitoa. Watamuunga mkono membe.Kitu ambacho CHADEMA hakitaruhusu kutokea ni kuunga mkono mgombea urais wa ACT WAZALENDO.
Kufanya hivyo itakuwa ni tiketi ya moja kwa moja kuwa kimeiruhusu ACT kukua kupitia mgongo wake na CHADEMA kusinyaa kupitia ACT.
It will never happen.
Umenikumbusha namna 2015 ulivyokuwa mwaka wangu mgumu kisiasa. Chama nilichokiamini kilisaliti harakati kimiujiza ujiza. Naona zile tikitaka zinajirudia. Acha waendelee kujivuruga.Ningekuwa Membe, Wakati huu ndio ungekuwa Wakati wa kupumzika kisiasa, kwani si rahisi Kwa mtu kama Membe Kwa siasa alixokuwa amefikia halafu Leo arudi chekechea, hizi siasa ndizo zilizowashusha hadhi kina Sumae na wengine,
Lakini Kwa kuwa huenda tena ikawa na siasa zilezile za CCM na ujasusi wake, Membe nenda kama ulivyotumwa na CCM kafanye yako, na temu hii hili bomu likiwalipukia hawa vichwa maji labda watakoma kushobokea vitu vizuri vizuri vilivyotegwa barabarani vikitafuta wajinga wasio ridhika na vyao
2015 nililazimika kukikacha Chama changu pendwa Kwa vitu hivihivi vya kijinga
Kinachowindwa na Zitto kwa Membe sio yeye kama yeye inawindwa pesa yake waibomoe kama walivyobomoa ya LowasaNdio maana wakaitwa wapinzani njaa hata mbowe na lisu walimuita lowasa na sumaye kila jina baya halafu wa kawasafisha na lowasa akawa mgombea uraisi, Tanzania hakuna wapinzani ni wachumia tumbo tu
Ni issue. Umesahau kuna unafiki wa kudumu pia. Kama huu.Katika siasa hamna adui wa kudumu au rafiki wakudumu kichopo ni maslahi ya kudumu......kwahiyo hiyo sio issue
Sio mchezoKinachowindwa na Zitto kwa Membe sio yeye kama yeye inawindwa pesa yake waibomoe kama walivyobomoa ya Lowasa
Wanaiwinda hela yake
Nyie mliemtukana EL kwenye kampeni mbona aliporudi CCM mlimpokea kama mfalme?Ndio maana wakaitwa wapinzani njaa hata mbowe na lisu walimuita lowasa na sumaye kila jina baya halafu wa kawasafisha na lowasa akawa mgombea uraisi, Tanzania hakuna wapinzani ni wachumia tumbo tu