Mimi nilidhania kuwa siasa ni uwanja wa mapambano ya fikra na si uadui!
Kupishana mitazamo hakuna maana ya udhaifu, na badala yake ni ukomavu.
Kama lipo linalofanyika kwa masilahi ya taifa kuna tatizo gani kukaa meza moja?
Suala hilo tusiliangalie kwa akina Zitto, nimeliona hapa JF. Watu hawapambanishi hoja bali hoja zinawapambanisha hadi kurushiana maneno machafu. Siasa haiendi hivyo.
Kuhusu umri, hili tumelijadili mara nyingi. Mimi sipendi kubaguana kwa kigezo cha ujana au uzee.
Kwanini watu tusiangalie mambo haya wakati wa kumtafuta au kuchagua kiongozi.
1. Mtizamo wake kuhusu jamii 2. Uelewa wake wa jamii 3. Uadilifu wake katika jamii 4. Historia yake ya ubunifu, utendaji na uongozi 5. Exposure katika dunia ya leo 6. Ueledi na maarifa aliyojipatia kupitia elimu 7. Misimamo yake kuhusu masuala ya jamii. Haya ni kwa uchche tu.
Naiangalia jamii yetu sijaona mahali ambapo ujana umesaidia kiongozi au uzee umekuwa dawa ya uongozi.
Katika kipindi hiki cha uongozi wa ujana, taifa limekuwa katika vurugu ya maadili kuliko wakati mwingine wowote.
Hata wazee wameiga mfano na tumeona wazee walioapa kwa kutumia katiba wakifanya tusiyotarajia.
Blair, Obama, Clinton, Putin n.k hawakuchaguliwa kwasababu ni vijana, bali kwa mitazamo na fikra pevu na wote wana prove hivyo. Hii haina maana Churchil, Washington, Gandhi na Mandela wapo chini yao, la hasha.
Kigezo cha kuwalinganisha si umri ni yale niliyoyataja.
Yahya Jamein na Samwel Doe wamekuwa marais katika umri wa chini ya 30. Ni kipi cha ajabu tunachoweza kusema walikifanya tofauti na William Tolbert, Augustino Neto au Nassar?
Tuwaangalie viongozi kwa thamani na wasifu wala sio wajihi