Zitto: "Majibu ya Sumari ni 'ovyo ovyo'"; atakiwa kufuta kauli!

Angekuwa na hizo busara angeomba msamaha lakini Zitto HAKUOMBA msamaha kwa kuwaita watanzania waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi nchini UK kuwa ni wapuuzi.
 
Kwa hiyo kama kafukuzwa kote huko kwa ajili ya kusimamia ukweli aache ili rekodi yake isionyeshe kafukuzwa sehemu nyingi?
Bora kuwa na rekodi kama hiyo kwa kusimamia ukweli kuliko kuwa kama wale wabunge wasaliti wanaosaliti waliowatuma kwa kujipendekeza kwa mafisadi. OVYO KABISA
 
hivi wabunge wa ccm wao kwao masilahi ya nchii hii ni yapiiiii???

wanaboa sana kwa tabia zao hizo za KINAFIKIIIIIII....

TUWAPUMZISHEEE JAMANIIII...

Cha ajabu ni kwamba wao hawafaidiki chochote na utajiri wa lowasa, RA wala huyo mkapa wala shg10 wengine hawapati na wanabaki kama walivyo sijui wanatetea mafisadi kwa faida gani
 

Sasa kama mtu kajibu utumbo aambiweje, kuwa jibu zuri wakati ni la hovyo. Kwani kuwa Mpinzani huruhusiwi kutumia lugha. Mpinzani haina maana wewe sio mtanzania. Kama majibu yao ni ya hovyo ni hovyo tu na ndio maana hata maamuzi yao ni ya kipuuzi nchi imezama kwa kuchagua maneno. Unajua nidhamu ya woga imeifilisi tanzania kizazi kipya inabidi kiwache kabisa kuabudu watu bali kutii sheria na kumfanya kila mtu azifuate bila kujali itikadi, na kipimo kinachotumika kiwe sawa sio cha masikini na tajiri, msomi na si msomi, ccm na wengine la hasha, moto kwa kwenda mbele. Sasa tuambie hovyo hovyo lina ubaya gani kamusi inasema nini? najua wapambe wa waziri wana hasira kwani kweli hakujibu kitu kaongea hovyo hovyo badala ya kujibu sasa anajicheka ujinga, na ukizingatia bunge limejaa vilaza kazi ndio hiyo.

maendeleo ya Tanzania yatakuja woga watakapokufa.
 
Angekuwa na hizo busara angeomba msamaha lakini Zitto HAKUOMBA msamaha kwa kuwaita watanzania waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi nchini UK kuwa ni wapuuzi.

Nawe bana....! sasa aombe msamaha kwa sifa ambayo inawahusu hao jamaa.....Hivi wewe kwa mfano; kama ni mpumbavu...mtu akakwambia we mpumbavu amekosea?

Angeomba msamaha angekuwa mnafiki mkubwa!
 
Shy, why are you not shy in making irrelevant contributions?

JF members here are deliberating whether or not MPs have the right (and obligatio) to tell Ministers who give misleading answers to questions of national importance, that they are talking rot. If Zitto is to be made to shut up, because of telling them off, who will speak for us?

The topic in front of Parliament was about the misappropriation of billions of shillings by Government officials through Meremeta, Tangold, Deep Green and Kagoda companies. The Deputy Minister of Finance avoided answering the question and arrogantly told Hon Dr Slaa to 'cook up' another question.

If Tanzanians are to divert their attention from this vital issue and go into light talk on fights between Shy and Zitto, we won't go far in the fight versus grand corruption and general decadence of this country.
 
Jamii haijengwi kwa maneno kama ya zitto na wale wote wanaosupport ushambenga wake , haijengwi kwa maneno matupu na majina vivuli ya watu wenye ajenda za siri kwa nchi hii
 
lakini ukiangalia kiundani pia si Mudhihiri peke yake anayefanya hivi. Kuna kitu kikubwa sana kimejificha nyuma ya mabadiliko ya tabia za kuchangia hoja za wabunge wa ccm na siamini kuwa ni matokeo ya uchaguzi mkuu pekee, lazima kuna kitu kingine nyuma yake...
 
Bunge litamchukulia hatua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe zitto kwa kuwa amekataa kufutakauli yake kwamba Naibu waziri wa Fedha na uchumi, Jeremiah sumari alitoa majibu ya hovyohovyo wakati anazungumzia suala la kampuni ya Meremeta.

Wakati anachangia bajeti ya ofisi ya waziri Mkuu muda mfupi uliopita, Zitto alizungumzia
sualala Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kuchunguza ufisadiunaodaiwa
kufanywa kupitia Benki Kuu Tanzania(BOT).

Wakati anazungumzia suala hilo, Mbunge huyo alisema, Sumari alitoa majibu ya Hovyo hovyobungeni na akaiomba Serikali isiingilie uchunguzi anaoufanya CAG.

Mbunge wa Nkasi, Ponsiano Nyami aliomba muongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa
Kwamtipura, Zubeir Ali Maulid kwa maelezo kuwa Zitto ametoa maneno ya kuudhi.

Kwa mujibu wa Nyami,maneno hayo yana maana kwamba, Sumari aliyatoa majibu bila kufikiriahivyo maneno ya Mbunge huyo yafutwe kwenye kumbukumbu za Bunge(Hansard).

Mwenyekiti wa Bunge alikubali hoja ya Nyami kuwa maneno hayo yafutwe kwenye hansard, naakamtaka Zitto pia ayafute maneno hayo na aendelee kuchangia bajeti hiyo.

Zitto alilalamika ni kwa nini ametakiwa afute maneno hayo wakati kuna Mbunge alilaaani
mawaziri hakuambiwa afute maneno yake, na kuna Mbunge alimshambulia waziwazi Waziri wa Menejimenti ya utumishi wa Umma, Hawa Ghasia lakini hakutakiwa kufuta maneno yake.

"Mheshimiwa Mwenyekiti,majibu ya Waziri kwa Mbunge wa Karatu ni ya hovyo hovyo" alirudiakusema Mbunge huyo.Zitto amekataa kufuta maneno hayo na kusema kwamba yupo tayari kwa lolote kutoka kwenye kiti cha Spika.

Mwenyekiti wa Bunge amesema, Zitto atachukuliwa hatua.

Wakati huo huo wabunge wameendelea kuwashambulia mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne wakiwatuhumu kuwa wanagawa fedha za Serikali kwa upendeleo na hawataki kushughulikia matatizo yanayowakabili wananchi.


Source: Habarileo mchana


 
Jamii haijengwi kwa maneno kama ya zitto na wale wote wanaosupport ushambenga wake , haijengwi kwa maneno matupu na majina vivuli ya watu wenye ajenda za siri kwa nchi hii

Ndugu yangu Shy....eti nini? Jamii haijengwi na maneno ya watu wa aina ya Zitto...fine, inajengwa na maneno ya watu gani? RA,EL,BM,JK,.....who?
 
Hahahahahhaha halafu akija mtaani? huu ushauri wako babu kubwa!!!!!!

Mkuu hukuwepo enzi za buzwagi? alipo kuja mtaani tukampokea, kilichofuata waulize walio mtimua ndani ya jumba, mbona walijijutia? Na wathubutu sasa kuleta ufyongo wao tena!

Yaani mtu akisema kweli ndo kakosea? tumechoka, kwani si ni kweli majibu yalikuwa hovyo kabisa?
 
Jamii haijengwi kwa maneno kama ya zitto na wale wote wanaosupport ushambenga wake , haijengwi kwa maneno matupu na majina vivuli ya watu wenye ajenda za siri kwa nchi hii

Shy, leo mbona hivyo!? Kila mtu unam-crash. Embu tueleze jamii huwa inajengwa vipi? au kwa maneno kama haya yaliyowahi tutolewa na waziri fulani wa fedha......Wanzania hata majani mtakula lakini lazima ndege ya Rais inunuliwe....
 
Kaza Butti Bwana Zitto, Maana mara nyingi wabunge wa CCM wanadhani kuwa Wao ndio Wabunge pekee yao Hapa tanzania na hivyo kuchukua madaraka pekee na hata wakisema hakuna mtu wa kusema kuwa CCM wanasema uongo ila ni Chadema, Usiogope wala nini!! Tupo pamoja Bwana Zitto
 
shy, leo mbona hivyo!? Kila mtu unam-crash. Embu tueleze jamii huwa inajengwa vipi? Au kwa maneno kama haya yaliyowahi tutolewa na waziri fulani wa fedha......wanzania hata majani mtakula lakini lazima ndege ya rais inunuliwe....

huyo zitto ni kioo cha jamii sehemu alipo ni nuru ya nchi yetu lazima apaheshimu hata anachoongea sio sehemu ya mipasho travertine pale , hatuhitaji viongozi wa aina hii mbeleni hawa wanaweza kutupiganisha vita
 
Jamii haijengwi kwa maneno kama ya zitto na wale wote wanaosupport ushambenga wake , haijengwi kwa maneno matupu na majina vivuli ya watu wenye ajenda za siri kwa nchi hii

bwan Shy lkn umesahau kumlist Mudhihiri hapa na maneno yake ya 'USHAMBENGA' (as u call it) aliyoyatoa bungeni hivi karibuni
 

Kilasara;

I think Shy is blinded or something by his/her personal conflicts with Mr. Zitto such that he can't any longer see and distinguish the good and bad from the MP....Very sad! He has a biased mind on Zitto really!
 
Kilasara;

I think Shy is blinded or something by his/her personal conflicts with Mr. Zitto such that he can't any longer see and distinguish the good and bad from the MP....Very sad! He has a biased mind on Zitto really!
very sad indeed..
 
Waziri Sumari aliongea hovyo hovyo na kwa kashifa na mbwembwe nyingi,kwani ana madaraka gani ya kumwambia mbunge (Dr.Slaa)ambaye anawakilisha wananchi atafute hoja nyingine wakati hoja yenyewe haijawahi kujibiwa hata siku moja,Miaka mingapi sasa hiyo hoja inapelekwa bungeni na haijawahi kutolewa jibu
Zitto kaza uzi tulisikia wote na ilirudiwa sana kwenye vyombo vya habari ilikuwa hovyo kabisa na isiyo faa
Na spika awe na uwiano wakusikiliza hao watoa hoja kwa sababu wanakazania kusemea kauli za wapinzani tuu mbona hatusikii kwa wana CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…