Zitto: Magazeti mawili yakaliwa kooni kuvujisha siri ya uhusika wa Muhongo kupandisha umeme

Rutaca

Member
Nov 13, 2014
94
236
Jana na Leo magazeti ya Mwananchi na The Citizen yameandika kuhusu kuhusika kikamilifu kwa Waziri wa Nishati na Madini kwenye mchakato mzima wa kupandisha bei ya umeme nchini. Magazeti hayo yalitoa ushahidi wa maandishi kwamba Waziri wa Nishati na Madini alimwandikia Waziri wa Fedha kuhusu mpango wa kupandisha bei ya umeme nchini.

Leo Wizara ya Nishati na Madini imetoa Taarifa kwa vyombo vya habari kukanusha habari za magazeti hayo. Vile vile Waziri amesambaza SMS kukanusha kushiriki kwake. Katika SMS yake hiyo Waziri amefikia hatua ya kutoa SIRI za Baraza la Mawaziri jambo ambalo ni kinyume cha kiapo chake na kinyume cha sheria.

SMS hiyo inasema " HAIWEZEKANI MUHONGO AKUBALI BEI KUPANDA
(1) Mwaka 2012, 2014 na kwenye vikao vya World Bank na AfDB Muhongo aliwakatalia suala la bei Kupandishwa hadi Mramba akamshitaki kwenye Baraza la Mawaziri

(2) Muhongo ndiye alishawishi TANESCO iondoe Malipo ya Maombi ya umeme na Service Charge.

(3) EWURA na waliotumbuliwa TANESCO na Wizarani wamenunua wasemaje na magazeti ya Kenya. Wapo wasiopenda zoezi la kufuta rushwa na wizi ndani ya TANESCO." Kwamba Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO alimshtaki Waziri wake kwenye Baraza la Mawaziri ni jambo jipya na dhahiri kwamba katika kujitetea Waziri ametoa SIRI za Baraza la Mawaziri. Adhabu ya kosa hili ni kufukuzwa Uwaziri.

Maelezo ya Wizara kuhusu bei ya Umeme yanaonyesha kuwa ni uwongo kwa lengo la kujitetea kwa Rais. Leo nilikuwa ninasoma Taarifa ya IMF ya tarehe 12 January 2017. Taarifa hii HAPA inaonyesha kuwa Serikali na IMF wamekubaliana kupandisha bei ya umeme ili kuliokoa Shirika la TANESCO. Wizara ya Fedha kamwe haiwezi kukubaliana na IMF bila Taarifa kutoka Wizara ya kisekta.

Rais John Pombe Magufuli awe makini Sana na Wasaidizi wake. Wanamdanganya wanapoona wamekosea ili kusukumia lawama wengine. Kwenye hili la bei ya umeme ushahidi ulio mbele yetu unaonyesha kuwa Wizara ya Nishati na Madini ilihusika moja kwa moja kupandisha bei ya umeme. Rais anapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya wasaidizi wanaopiga majungu wenzao ili iwe fundisho kwa wengine.

Tunajua na kuunga mkono nia njema ya Rais kutaka wanyonge kuwa na umeme nafuu. Pia tunajua Rais ni msema kweli na haonei mtu. Kwenye hili la TANESCO ameonea mtu kwa kumwadhibu kwa makosa ya watu wengine wenye mamlaka zaidi
 
Toka Muhongo amechukua wizara hiyo hali ya Umeme imekuwa nzuri kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru.

Aliwahi kuwekwa Simbachawene kwa miezi michache ilikuwa balaa. Ngeleja ndio usiseme. Muhongo amefuta biashara ya Majenereta na mmi nauza Jenereta miezi mitatu sasa hakuna wateja.

Ukimpima kiongozi based on results Muhongo is the best, ila kama mnataka wanasiasa wazuri mtoeni ila Mimi ameokoa biashara yangu iliyotaka kufa kwa kukosa umeme wa uhakika wa Tanesco
 
mwananchi ni gazeti makin kwa sasa, wanafanya uchunguzi,wanatoa habari muendelezo. hongereni.

mwananchi iliwahi kuandamwa kipindi Fulani, ooh gazeti la Kenya halina uzalendo oo my God yakaisha.

sasa kuhusu kufukunyua issue ya Muhongo Na kuweka bayana ushiriki wake katika sakata la tanesco sidhani watabaki salama. ni hatari.

Muhongo alilazimishwa kujiuzulu katika kashfa ya escrow lakini bado akapewa tena uwaziri,

swali mkurugenzi tanesco alitumbuliwa,kwanini Muhongo km alishiriki Na km ushahidi upo nae asipewe haki yake.

ngoja tuone!!
 
Ni aibu wizara kwa hadhi yake kupinga habari zilizotolewa kwenye magazeti. Wangezikanusha kama zilivyoandikwa hoja baada ya hoja ili sisi tuliosoma na kusikia maoni ya wizara tukaelewa nani mbaya wetu. Tusisahau kuwa media kwa walioendelea na kustaarabika ni mhimili wa nne wa utawala!
 
Muhongo hana cha kukwepa hapa kwani ukweli lazima usemwe hata kama amekingiwa kifua na mkubwa
 
Toka Muhongo amechukua wizara hiyo hali ya Umeme imekuwa nzuri kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru. Aliwahi kuwekwa Simbachawene kwa miezi michache ilikuwa balaa. Ngeleja ndio usiseme. Muhongo amefuta biashara ya Majenereta na mmi nauza Jenereta miezi mitatu sasa hakuna wateja.

Ukimpima kiongozi based on results Muhongo is the best, ila kama mnataka wanasiasa wazuri mtoeni ila Mimi ameokoa biashara yangu iliyotaka kufa kwa kukosa umeme wa uhakika wa Tanesco
kama kweli ni mchapakazi kama unavyosema si afute mikataba ya iptl inayokula mamilioni ya kodi za wa Tanzania kila siku pale Tanesco, unadhani wanaotaka kupandisha umeme wanapenda iwe hvo au wanashindwa kuendesha shirika kwa mikataba ya kipuuzi
 
Back
Top Bottom