Zitto, Lowassa na Mbowe - Dhana ya Usaliti na Ujinga wa Watanzania

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,299
2,000
Mwaka 2010 kupitia BBC kuna mkenya aliulizwa kuhusu siasa za TZ na Amani yetu tukufu. Alijibu kuwa waTZ ni either wajinga au hawajui haki zao kabisa. Ilipita miaka mingi sikuwahi kuelewa hili jibu na nilihisi ni udhalilishaji.

Hili la Ujinga nilitafakari sana, how could that be?

Marehemu Shekh Hassan Ilunga , alisema Uongo ukirudiwa rudiwa rudiwa hugeuka kuwa ukweli.

Moja ya sifa kuu ya bwana Zitto ni USALITI hii ni dhana ambayo imegeuka kuwa ukweli na itamuandama ZZK mpaka kufa kwake, na sehemu kubwa ya jamii imeshaamini hivyo.

Lakini Je ni upi Usaliti wa ZZK?

Kimsingi mpaka sasa hakuna kati yetu anayeweza kuja na ithibati ya hakika juu ya usaliti wa huyu bwana. Ni maneno yaliyoanzishwa kwa maslaha fulani ili mambo mengine yafanyike. Ni kipindi hiki hiki cha mambo fulani yafanyike ndicho kipindi ambacho Agenda ya Usaliti ilizuka na kuzaa matunda.

Wamarekani walishawahi kusema kwamba kitu chochote ambacho hakina uthibitisho ambao everyone can check and prove it tunasema ni claims. Claim isn't a way to truth untill proven to be true.

Nikaanza kuelewa ujinga wa waTZ na nikajua ni wapi tunakwama.

WaTZ tunapenda kufikiriwa badala ya kufikiri.

Chadema ni chama pekee ambacho kilijijenga katika misingi thabiti kwa msaada mkubwa wa Dr Slaa. Misingi ya kupambana na rushwa na ufisadi uliokithiri katika utawala wa awamu ya 4.

Lakini pamoja na hayo dakika za mwisho yalifanyika mapinduzi ambayo yaliacha maswali mengi kuliko majibu yaliyopelekea Dr Slaa kuachana na siasa za Chadema kabisa na kufanya maisha yake. Hili lilikuwa ni pigo kwa Chadema kumpoteza Critical Thinker. Matokeo yake tunaona ni jinsi gani Chadema ilivyouliwa na wanachadema wenyewe kwa tamaa za pesa kwa watu wachache.

Maswali ambayo sisi Wajinga hatujawahi kujiuliza,

1 Je katiba ya Chadema inasemaje kuhusu ukomo wa mtu kuwa mwenyekiti wa Chama? Tunajua wapinzani wetu wakuu CCM ni miaka 10, je chadema ni mingapi na Mbowe amekuwa mwenyekiti kwa muda gani ?

2. Kukaribishwa kwa Edo Chadema na kupewa nafasi ya kugombea uraisi moja kwa moja kuna leta tafsiri gani chini ya uenyekiti wa mbowe ?

3. Ni mbinu gani ambazo Lowasa ambaye kimsingi ameshakufa kisiasa alizitumia kushawishi baadhi ya management ya Mbowe na kupewa highest position kwenye nafasi ya marathon ya uraisi?

4. Ni kweli timu nzima ya Chadema iliridhia haya maamuzi? Kama ndio ni kwanini kina slaa walijiengua na usaliti huu?

5. Tunajua hakuna free lunch, je Edo alitoa nini ambacho kilishawishi wachache Kwenye chama na kumfanya kuwa muwakilishi wa chadema nafasi ya uraisi ? Kuna siri gani hapa, Mbowe ana majibu.

Ikiwa ameweza kuuza chama kwa duni thamani, atashindwaje kuuza nchi ?

Ikiwa ameweza kuditch wote waliosimamia chama katika misingi thabiti ya kutokomeza ufisadi na kumpa mtu ambaye hana histora yoyote katika chama, je tunamuweka kwenye kundi gani huyu bwana, ni Upi usaliti kati ya huu na wa ZZK ?

6. Je ni waTZ wangapi walishawahi kuhoji hili ? Au kumuhoji Mbowe ilikutoa majibu sahihi juu ya Usaliti wake .

Je ni upi usaliti kati ya Mbowe, Edo na Zitto?

Kupokea makapi ya CCM na kutoa nafasi za juu? There must be something behind. Na hili halijasahaulika katika vifua vya Wanachadema.

5. Lowasa amerudi CCM, je ni waTZ wangapi wamehoji kigeugeu hiki , je alifuata nini Chadema ? ameondoka na siri ngapi za chama ambazo atazipeleka kwa mamlaka za juu ? na je ame share siri ngapi za CCM na serikali husika katika mamlaka ya Chadema ?

Pamoja na yote hayo hutosikia hata siku moja Lowasa akiitwa Msaliti wala Mbowe akiitwa msaliti —Tafakari Mtanzania.

Narudia tena kusema Tanzania hakuna upinzani bali kuna matapeli na wafia njaa.

CCM sio chama bora tena kwetu kimeshindwa kuibadilisha nchi badala yake kila shughuli za maendeleo zinafanywa kisiasa.

leo ukitembea maeneo mengi utaona barabara zinajengwa, barabara za mwendokasi wa mbagala zimeshaanza bila ya kujali kuwa mradi wa awali upo mbioni kuzkwa na hakuna anayehoji.

Jafo alikuja kisiasa kuzima kelele za mwendokasi na hutosikia tena baada ya siku ile, lakini bora ya shida za CCM kuliko upinzani uchwara wa nchi hii.

Nina imani upinzani utazaliwa TZ wapinzani ambao watakuwa na nia ya dhati ya kuingia ikulu, upinzani ambao kwa hakika utataka kuleta Mabadiliko ya kweli, upinzani wenye tija bila kujali dini wala ukabila.

TAFAKARI!

Sunday 31, March 2019
-----------------------
Lakini je ilikuwa
 
Dripboy

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
3,195
2,000
Upinzani uchwara upo kwenu/kwako na ukoo wenu, unauliza maswali ya msingi sana lakini mwishoni umeharibu umeandika uhalo wa bata jike.

Dkt slaa hajawahi kuwa nguzo muhimu ndani ya chadema yule ni ndumila kuwili mkubwa sana hana tofauti na mnyaturu mama mghwira wana tabia za tamaa shida yao si kutatua matatizo yaliyopo ni kuyashibisha matumbo yao bwege sana wewe mnajifanya wasomi kumbe hovyo.
 
Jibu hoja. Usini attack. Huu ni ukweli mchungu. Huwa sina maslahi kwenye posti zangu , ni misinterpretation ya watu wasiopenda kufikiri.

Nakuomba urudi kwenye point.
 
Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
5,924
2,000
Chadema siwezi kuwasamehe kwa kosa walilofanya, kumchukua mtu waliyetuaminisha kwa 100% kuwa ni fisadi, then wakampa nafasi awe president candidate wao/wetu ili hali alishaanza safari ya matumaini akiwa na kile chama cha kifisadi yaani ccm.

Mleta mada upo sahihi. Mtu ukitaka kugusa maslahi ya viongozi basi lazima uundiwe zengwe, na mwisho wanakutosa. Siasa za bongo hovyo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof sas

Senior Member
Jun 24, 2014
127
225
Mwaka 2010 kupitia BBC kuna mkenya aliulizwa kuhusu siasa za TZ na Amani yetu tukufu. Alijibu kuwa waTZ ni either wajinga au hawajui haki zao kabisa. Ilipita miaka mingi sikuwahi kuelewa hili jibu na nilihisi ni udhalilishaji.

Hili la Ujinga nilitafakari sana, how could that be?

Marehemu Shekh Hassan Ilunga , alisema Uongo ukirudiwa rudiwa rudiwa hugeuka kuwa ukweli.

Moja ya sifa kuu ya bwana Zitto ni USALITI hii ni dhana ambayo imegeuka kuwa ukweli na itamuandama ZZK mpaka kufa kwake, na sehemu kubwa ya jamii imeshaamini hivyo.

Lakini Je ni upi Usaliti wa ZZK?

Kimsingi mpaka sasa hakuna kati yetu anayeweza kuja na ithibati ya hakika juu ya usaliti wa huyu bwana. Ni maneno yaliyoanzishwa kwa maslaha fulani ili mambo mengine yafanyike. Ni kipindi hiki hiki cha mambo fulani yafanyike ndicho kipindi ambacho Agenda ya Usaliti ilizuka na kuzaa matunda.

Wamarekani walishawahi kusema kwamba kitu chochote ambacho hakina uthibitisho ambao everyone can check and prove it tunasema ni claims. Claim isn't a way to truth untill proven to be true.

Nikaanza kuelewa ujinga wa waTZ na nikajua ni wapi tunakwama.

WaTZ tunapenda kufikiriwa badala ya kufikiri.

Chadema ni chama pekee ambacho kilijijenga katika misingi thabiti kwa msaada mkubwa wa Dr Slaa. Misingi ya kupambana na rushwa na ufisadi uliokithiri katika utawala wa awamu ya 4.

Lakini pamoja na hayo dakika za mwisho yalifanyika mapinduzi ambayo yaliacha maswali mengi kuliko majibu yaliyopelekea Dr Slaa kuachana na siasa za Chadema kabisa na kufanya maisha yake. Hili lilikuwa ni pigo kwa Chadema kumpoteza Critical Thinker. Matokeo yake tunaona ni jinsi gani Chadema ilivyouliwa na wanachadema wenyewe kwa tamaa za pesa kwa watu wachache.

Maswali ambayo sisi Wajinga hatujawahi kujiuliza,

1 Je katiba ya Chadema inasemaje kuhusu ukomo wa mtu kuwa mwenyekiti wa Chama? Tunajua wapinzani wetu wakuu CCM ni miaka 10, je chadema ni mingapi na Mbowe amekuwa mwenyekiti kwa muda gani ?

2. Kukaribishwa kwa Edo Chadema na kupewa nafasi ya kugombea uraisi moja kwa moja kuna leta tafsiri gani chini ya uenyekiti wa mbowe ?

3. Ni mbinu gani ambazo Lowasa ambaye kimsingi ameshakufa kisiasa alizitumia kushawishi baadhi ya management ya Mbowe na kupewa highest position kwenye nafasi ya marathon ya uraisi?

4. Ni kweli timu nzima ya Chadema iliridhia haya maamuzi? Kama ndio ni kwanini kina slaa walijiengua na usaliti huu?

5. Tunajua hakuna free lunch, je Edo alitoa nini ambacho kilishawishi wachache Kwenye chama na kumfanya kuwa muwakilishi wa chadema nafasi ya uraisi ? Kuna siri gani hapa, Mbowe ana majibu.

Ikiwa ameweza kuuza chama kwa duni thamani, atashindwaje kuuza nchi ?

Ikiwa ameweza kuditch wote waliosimamia chama katika misingi thabiti ya kutokomeza ufisadi na kumpa mtu ambaye hana histora yoyote katika chama, je tunamuweka kwenye kundi gani huyu bwana, ni Upi usaliti kati ya huu na wa ZZK ?

6. Je ni waTZ wangapi walishawahi kuhoji hili ? Au kumuhoji Mbowe ilikutoa majibu sahihi juu ya Usaliti wake .

Je ni upi usaliti kati ya Mbowe, Edo na Zitto?

Kupokea makapi ya CCM na kutoa nafasi za juu? There must be something behind. Na hili halijasahaulika katika vifua vya Wanachadema.

5. Lowasa amerudi CCM, je ni waTZ wangapi wamehoji kigeugeu hiki , je alifuata nini Chadema ? ameondoka na siri ngapi za chama ambazo atazipeleka kwa mamlaka za juu ? na je ame share siri ngapi za CCM na serikali husika katika mamlaka ya Chadema ?

Pamoja na yote hayo hutosikia hata siku moja Lowasa akiitwa Msaliti wala Mbowe akiitwa msaliti —Tafakari Mtanzania.

Narudia tena kusema Tanzania hakuna upinzani bali kuna matapeli na wafia njaa.

CCM sio chama bora tena kwetu kimeshindwa kuibadilisha nchi badala yake kila shughuli za maendeleo zinafanywa kisiasa.

leo ukitembea maeneo mengi utaona barabara zinajengwa, barabara za mwendokasi wa mbagala zimeshaanza bila ya kujali kuwa mradi wa awali upo mbioni kuzkwa na hakuna anayehoji.

Jafo alikuja kisiasa kuzima kelele za mwendokasi na hutosikia tena baada ya siku ile, lakini bora ya shida za CCM kuliko upinzani uchwara wa nchi hii.

Nina imani upinzani utazaliwa TZ wapinzani ambao watakuwa na nia ya dhati ya kuingia ikulu, upinzani ambao kwa hakika utataka kuleta Mabadiliko ya kweli, upinzani wenye tija bila kujali dini wala ukabila.

TAFAKARI!

Sunday 31, March 2019
-----------------------
Lakini je ilikuwa
Greater thinker...big up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,541
2,000
Mimi naomba nikujibu ingawa sijatumwa na CHADEMA wala yeyote uliowataja kwenye bandiko lako. Na haya ni mawazo yangu kulingana na hoja zako ulizozitoa.
Nikianza na Zitto uliyempa sifa kuu ya USALITI. Kwanza kabisa hii ni hukumu umeitoa na kasha ukaipooza kwa kisentensi cha kiingereza kwamba Claim isn't away to truth until proven to be true. Huwezi kumuita Zitto msaliti kasha wewe huyo huyo ukasema hizo ni accusations tu hazina ukweli na ukataka proof, kama hukuwa na proof kuhusu hilo usingemuita MSALITI, ungesubiri ujilidhishe na tuhumu kasha ndio umuite MSALITI.
Binafsi kwangiu Zitto ni msaliti na na ana uchu wa sifa au kujumuishwa kwenye sifa asizostahili, kama ni kuilikomboa taifa hili kutoka kwenye utawala mbovu Zitto siwezi kusema ni mmoja wao, huyu ni mchumia tumbo na ni opportunist mkubwa, aliitumia CHADEMA kujijenga akidhani amekomaa sasa akaanza kuiharibu, alipopainika akafukuzwa akaanzisha chama cha ACT kwa mbwembwe na kujiona shujaa, lakini watanzania walipomkataa akagundua hajakomaa, hivyo akaanza kuomba kuungana na aliowasaliti CHADEMA akidai kwamba hakuna chama kitaweza kuiondoa ccm madarakani bila kushirikiana na vingine, alikuwa akiomba kushirikishwa kwenye UKAWA, sijui kama watamkubali lakini ningekuwa ni miongoni mwa wafanya maamuzi ningemkatalia liwe funzo kwa vijana wote wenye hulka natabia za ZITTO.

Kuhusu Dr.Slaa nadhani umepotoka kama sio kwamba hufahamu. Huyu licha ya upadri wake alikuwa ni mwana CCM mzuri tu, lakini alivyotaka kugombea huko ccm akashindwa kufuata taratibu zao zilee za kura ya maoni, alijiondoa na kuomba kujiunga na CHADEMA. Huyu hakuianzisha CHADEMA aliikuta, na alitokea CCM lakini nashangaa hukumuita ni MAKAPI ya CCM kama ulivyo muita Edo. Dr. slaa alikuwa akijijenga yeye ndani ya chadema sio CHADEMA maana aliikuta, naye alikuwa na malengo yake huko ndani ya CHADEMA, sasa aliposhindwa kuyatekeleza akasusa. kama edo ni makapi basi na Dr.slaa ni makapi ya CCM na hata yeye alipoondoka Chadema kama Edo, Dr.Slaa naye alirudi CCM huko huko, mbona yeye ulimsitiri hukumuita MSALITI kama kurudi ccm ni usaliti sielewi hii dhambi yeye kwanini umuepushe nayo.

Kuhusu Edo kujiunga chadema huelewi kitu kimoja, muda huo ilikuwa sio chadema inaamua, ilikuwa ni muungano wao wa UKAWA, kwasababu UKAWA hautambuliki kwa msajili wa vyama vya siasa asingeweza kugombea kupitia UKAWA ilibidi ajiiunge na chama kimoja wapo, kwakuwa CHADEMA, lakini angweza kujiunga kwa chama chochote mwananchama wa UKAWA kama CUF,NLD, NCCR au CHAUMA. Lakini kwakuwa alijiunga chadema ukuliza kwam maamuzi hayo yalilidhiwa na wengine au la, Ndio walikubali ajiunge. Edo hakuwa na cha kutoa ila mtaji aliokuwa nao kipindi hicho ni wafuasi wake waliokuwa huko CCM. Kama ni Makapi basi sijui nani siyo kapi.
Wanachama wa hivi vyama ni wananchi wa Tanzania, hivyo sidhani kama kuna chama kinaagiza nje wananchama wapya, ni sisi hawa hawa tunakuwa recycled tu, leo CCM kesho Chadema.

Nadhani kama ulitaka kuchambua SIASA ulikosea kuishambulia CHADEMA.

Mimi nimejitahidi kiasi change ila wenyewe watakuja.
 
Hapana hujaelewa mada kabisa. Rudia kusoma kwa mstari sijamuita ZZK MSALITI nimezungumzia dhana iliyokuwepo juu yake. Ni kasema kwamba ni mpango na agenda maalumu ya kumuita msaliti ili asiendelee na safari yake ya matumaini ndani ya Chadema.

Hata hivyo umeendelea kumuita ZZK msaliti, bahati nzuri umesema ni mawazo yako. Hoja yangu ni kwa yeyeyo mtanzania anayemuita ZZK msaliti basi aje na Ithibati, tofauti na hapo hizo ni claim as long as hazina ithibati.

Lakini pia umezungumza sana na stori zile zile za mtaani hujafanikiwa kujibu hoja hata moja.
Yes ilikuwa ni muunganiko wa vyana lakini yeye alipitia Chadema. Na aliendelea kudumu kwa muda baadae kurudi nyumbani yaani CCM , je ni yupi msaliti kati ya Mbowe Edo na ZZK .

Nakuomba urudi kwenye point za msingi kwenye mada.
 
Rohombaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
12,200
2,000
Upinzani uchwara upo kwenu/kwako na ukoo wenu, unauliza maswali ya msingi sana lakini mwishoni umeharibu umeandika uhalo wa bata jike.

Dkt slaa hajawahi kuwa nguzo muhimu ndani ya chadema yule ni ndumila kuwili mkubwa sana hana tofauti na mnyaturu mama mghwira wana tabia za tamaa shida yao si kutatua matatizo yaliyopo ni kuyashibisha matumbo yao bwege sana wewe mnajifanya wasomi kumbe hovyo.
Dah...kujua na kulielewa tatizo...ndiyo mwanzo wa utatuzi

Sent using Beretta ARX 160
 
Nov 11, 2016
90
125
Je mbona hujahoji katiba ya UDP ambayo imempa mamlaka mwenyekiti wa chama hicho bwana John Momose Cheyo kuwa kiongozi wa chama hicho maisha?Kipi kilimkuta makamu mwenyekiti bwana Amani Nzugile Gidulamabambase baada ya kugombea cheo cha bwana Cheyo?msomi mzima ovyo jitafakari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,299
2,000
Je mbona hujahoji katiba ya UDP ambayo imempa mamlaka mwenyekiti wa chama hicho bwana John Momose Cheyo kuwa kiongozi wa chama hicho maisha?Kipi kilimkuta makamu mwenyekiti bwana Amani Nzugile Gidulamabambase baada ya kugombea cheo cha bwana Cheyo?msomi mzima ovyo jitafakari

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo jina lako lol .

Please nakuomba urudi kwenye point. Hoja za msingi umeziacha. Nimehoji sababu Chadema ndio kilikuwa chama pekee chenye vijana mahiri na wenye kufikiri katika upande wa upinzani. Na tulikiamini katika nia ya dhati lakini kumbe tulikuwa tunatumika kunufaisha matumbo ya watu.

Ni nani Msaliti kati ya Edo- Mbowe na Zitto?

Ni lini watanzania tutaacha Ujinga wa kukaririshwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom