Zitto, Lissu na Mbowe wanafanya makosa kama ya Morgan Tsvangirai

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Wakati Zimbabwe wanatafuta uhuru, kikwazo kikubwa kwao ilikuwa ni serikali ya Uingereza iliyokuwa inampa support Smith. Katika harakati hizo, Zimbabwe walifundishwa kupambana na Waingereza ili wafanikiwe uhuru wao.

Morgan alipokuwa anapambana na Mugabe akafanya kosa la kutafuta msaada toka Uingereza. Pamoja na kumchoka Mugabe, Morgan hakuonekana kuwa mtu sahihi wa kushika nafasi hiyo. Bahati mbaya hata SADC waliona ni upuuzi tu!

Tunao akina Zitto, Lissu na Mbowe. Huu ni mwaka wa uchaguzi ndo wanachachamaa kuzunguka Ulaya na US wakiomba msaada na kuishitaki serikali wanayoiita ni ya CCM.

Je, kweli wanaamini wananchi wanafurahia sana kusikia mtu anataka kutawala kwa msaada wa US na Ulaya?

Naweza kusema huo ni ujuha. Kwa ufahamu wa leo, huwezi saidiwa na US kutawala nchi baadaye US ikuachie bila kuivuna nchi inavyotaka.
 
Tafsiri ya "UJUHA" tunaipata kwako wewe muandishi wa huu uzi. Wananchi tumeichoka CCM sana, sio uongo wala nini.

Ni bora nchi hii itawaliwe "KICHIFU" kuliko mtawala kutoka "CCM".

CCM ni chama kinachoongoza kwa ufisadi Africa nzima, nchi hii ufisadi wote uliofanyika kuanzia Uhuru mpaka sasa, umefanyika chini ya "KIVULI CHA UTAWALA WA CCM".

Hakuna hata sehemu moja kuna "PUA" ya vyama vya upinzani hapa.

-Mikataba ya madini.
-Mikataba ya unyonyaji.
-EPA
-Escrow
-Dowans
-Kuuzwa kwa mali za serikali (Kuna watu waliwapa ndugu zao na vimada mijengo).
-10% za ujenzi wa barabara za lami.
-1.5 trillioni (upotevu).

Mpaka nimechoka mikoni kuandika hio list.
 
CCM ameshakuwa adui wa nchi hii na vijana wengi tunaiona CCM kama chama kinacho tuharibia maisha yetu...hamna uchumi wanaojenga zaidi ya kueneza umasikini for over 50 years, tulipende hili chama nini? Wacha liondolewe even if for the facts tunajua marekani ni taifa hatari...mkoloni mweusi ni mbaya sana.

Ntalipendaje taifa langu sina ajira? Sina mtaji, sina matumaini? I have nothing except my own strength! Yani CCM iondolewe tumeichoka, huo uzalendo wanao wao Sababu wameshiba. Mimi na njaa, uzalendo wa nini? Sina uzalendo kwa hii serikali hata kidogo!
 
CCM ameshakuwa adui wa nchi hii na vijana wengi tunaiona CCM kama chama kinacho tuharibia maisha yetu...hamna uchumi wanaojenga zaidi ya kueneza umasikini for over 50 years, tulipende hili chama LA nini? Wacha liondolewe even if for the facts tunajua marekani ni taifa hatari...mkoloni mweusi ni mbaya sana. Ntalipendaje taifa langu sina ajira? Sina mtaji, sina matumaini? I have nothing except my own strength! Yani CCM iondolewe tumeichoka....huo uzalendo wanao wao Sababu wameshiba...Mimi na njaa, uzalendo wa nini? Sina uzalendo kwa hii serikali hata kidogo!
Labda vijana wahuni wa JF
 
CCM ikirudi madarakani October 2020, lazima US kama si kui-Libya nchi yetu basi watai-Iraq. yote mawili ni majanga.

Hiyo upende usipende lazima itatokea labda upinzani ushike madaraka!
 
Analysis yako imekosa weledi. Hivi unajua kuwa bila ya support ya UK na US, harakati za kuondoa ubaguzi wa rangi kwa kutumia nchi za mstari wa mbele, OAU na Umkondo wa Sizwe, zilikuwa zimeshindwa?

Ni baada ya jitihada kubwa za kidiplomasia za kuzishawishi Uingereza na Marekani kufanikiwa, ndipo Makaburu waliposalimu amri.

Hata kufanikiwa kwa Mwalimu katika kutafuta uhuru wa Tanganyika, kulitokana zaidi na jitihada za kidiplomasia za kuyashawishi mataifa makubwa kutuunga mkono. Ukumbuke kuwa jitihada za akina Kinjekitile, Chabruma, Mkwawa, Isike - zote ziliginga mwamba.

Hata wakati wa vita dhidi ya Id Amin, mwalimu alilalamika sana juu ya OAU kwa kushindwa angalao kutamka tu kuwa uvamizi wa Amin ulikuwa haramu. Unadhani kwa nini aliitaka kauli hiyo?

Katika mapambano yoyote, na hasa ya kupambana na mwenye nguvu, ushindi wake hutegemea zaidi kuungwa mkono, ndani na nje.
 
CCM ikirudi madarakani October 2020, lazima US kama si kui-Libya nchi yetu basi watai-Iraq. yote mawili ni majanga.

hiyo upende usipende lazima itatokea labda upinzani ushike madaraka!
unasubilia hilo kwa hamu? ikiondoka nani atawale? Mbowe wa CHADEMA? UNaamini hapo kuna kichwa cha kutawala nchi hapo? Aache kuuza bangi za billicanas
 
Analysis yako imekosa weledi. Hivi unajua kuwa bila ya support ya UK na US, harakati za kuondoa ubaguzi wa rangi kwa kutumia nchi za mstari wa mbele, OAU na Umkondo wa Sizwe, zilikuwa zimeshindwa?

Ni baada ya jitihada kubwa za kidiplomasia za kuzishawishi Uingereza na Marekani kufanikiwa, ndipo Makaburu waliposalimu amri.

Hata kufanikiwa kwa Mwalimu katika kutafuta uhuru wa Tanganyika, kulitokana zaidi na jitihada za kidiplomasia za kuyashawishi mataifa makubwa kutuunga mkono. Ukumbuke kuwa jitihada za akina Kinjekitile, Chabruma, Mkwawa, Isike - zote ziliginga mwamba.

Hata wakati wa vita dhidi ya Id Amin, mwalimu alilalamika sana juu ya OAU kwa kushindwa angalao kutamka tu kuwa uvamizi wa Amin ulikuwa haramu. Unadhani kwa nini aliitaka kauli hiyo?

Katika mapambano yoyote, na hasa ya kupambana na mwenye nguvu, ushindi wake hutegemea zaidi kuungwa mkono, ndani na nje.
Imeandikwa Zimbabwe wewe unarukia ubaguzi wa rangi, shiiit!
 
Labda vijana wahuni wa JF
Wewe endelea kulala usingizi wa pono, probably unafikili hizi ni zama za miaka ya 90! Ogopa vijana wasomi wanapokuchoka kuliko a league of idiots huko vijijini mnapovuna kura wasiojua ABCs kuhusu maisha yao, an Arab spring haikuanzishwa na vijana wa vijijini ila wasomi walioona maisha yao yanaharibika, wapuuzi kama nyie huwa mnajiona mko salama mpaka mtakapoona mitaa haipitiki. Nakuhakikishia CCM ikiendelea kutokujenga uchumi na mazingira ya ajira kwa vijana itaondolewa hata kwa nguvu, sikujui unijua ila IPO siku utakumbuka.kama unaweza jifunza jambo jifunze uchaguzi huu uone wangapi watajitokeza kupiga kura....ukiona watu hawajitokezi jiulize kwann, sababu nakuhakikishia mwaka huu wapiga kura mtawapata vijijini sio mijini, na mkishinda kwa asilimia 99 mnajiona wajanja kama mahayawani wakati huo ushindi wa 99% ndio kaburi lenu? Nawashauri ibeni, uweni watu, ondoeni wapinzani wote mshinde kwa asilimia 100, serikali si yenu? Mabunduki si yenu? . Na huko Zanzibar mtazingua mtapigwa vikwazo vya kiuchumi, tutaona mtakavyo survive kabla hao wanajeshi hawajaanza kudai mshahara kwa mtutu wa bunduki..ila wanadai kusikia kwa mamba mpaka damu masikioni.
 
Imeandikwa Zimbabwe wewe unarukia ubaguzi wa rangi, shiiit!
Upeo wako ni mdogo kuweza kuelewa hoja.

Cha muhimu, ni kuwa pamoja na umuhimu wa nguvu za ndani, inahitajika nguvu ya uungwaji mkono ya kimataifa, katika kuondoa dhuluma. Tumefanya hivyo kutokomeza ubaguzi wa rangi South Africa, kurudisha utawala wa kidemokrasia nchini Comoro, kumwondoa mvamizi Id Amini kutoka kwenye ardhi yetu, na itaendelea kufanyika hivyo kila penye dhuluma.
 
CCM ikirudi madarakani October 2020, lazima US kama si kui-Libya nchi yetu basi watai-Iraq. yote mawili ni majanga.

hiyo upende usipende lazima itatokea labda upinzani ushike madaraka!
Wewe una PHD ya utahira na umeisomea kwa mabeberu.swali dogo tu kwako tangu wameziharibu hizo kuna matokeo chanya katika nchi zote kuliko hapo awali au unawaswa?
 
Mleta mada habari za asubuhi. Naona umekosa mtetezi hata mmoja! Pole sana. Watag wadau waje tusimame pamoja.

Wakubwa wenye madaraka huko juu serikakini, Nimekutana na mstaafu wa mwaka Jana, hali yake yasikitisha. Hana monthly pension wala burungutu hajapata. Anadaiwa ada, mbolea na kuendeleza maisha ya kila siku. ANGALAU tuikumbushe Serikali KUWAPA fair. Mara salary ya mwisho inapoingia mfumo ubadili formula ili mwezi ujao apate pension yake, inawezekana. VIGEZO kwamba sijui hawa kujaza abcd kwa sasa kwao sio hoja YAO. Wameitumikia nchi hii kwa miongo si chini ya 3. Wametingwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaona walivyokujibu? Kama wewe ni adui yangu, nitatafuta adui yangu mwingine ambaye hatuna active ugomvi anisaidie nikupige, then nirudi nijadiliane na passive adui tumalize uadui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom