Mchokonoaji
Member
- Oct 1, 2009
- 26
- 1
Jana Zitto alimuunga mkono Chenge kuwa wahusika walioteuliwa na Rais basi Rais aachwe awawajibishe yeye mwenyewe. Muda huo Chenge alimaanisha MASWI na WEREMA. Kwa hasira Zitto alishauri basi na wengine wote waliobaki wawajibishwe na mteuzi wao ambaye ni Rais na akashangiliwa na CCM sana.
Ushauri huu wa Zitto umezua machukizo kwa wengi. Hata hivyo binafsi niliutafakari ushauri huo na kuuelewa nini maana ya Zitto.
Binafsi nauona kuwa ushauri ambao ungekula upande wa mafisadi na mbaya zaidi ungemhusisha Rais moja kwa moja kwenye sakata hili na kumwangushia jumba bovu.
Nidhahiri kuwa endapo wangemuachia Rais aamue wangekuwa wamemkabidhi lawama ya kushindwa kuwawajibisha wateule wake na hivyo kumuonesha yeye kama kiini cha tatizo.
Kutokana na ukweli kuwa Rais asingeweza kuwatimua maswahiba zake hao. ZITTO alilenga kuiaibisha CCM kuanzia mwenyekiti wake.
Hili lingeiharibia CCM zaidi in the long run japo ingewalinda kwa urahisi mafisadi hawa kipindi hiki kigumu kwao.