Zitto kutogombea Kigoma Mjini

Zitto kutogombea Kigoma Mjini

Ally mvano

Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
73
Reaction score
24
Hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa chama hicho Ndugu Jafari Kasisiko katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Mjini hapo na kuahidi kuleta jina la mgombea wao siku chache mbeleni
 
Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu
Ushirikiano wa vyama
Kumekuwa na shauku ya wananchi kwa sisi
kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili
kufanikisha malengo yetu ya kuleta mapinduzi
ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo ...wa
uchumi unaonyonya wananchi. Msimamo wetu
upo wazi na tumeueleza mara kadhaa
1 tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana
kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu
ALLIANCE na Msimamo wetu kuhusu mabadiliko
ya Katiba.
2 tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi
na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za
uongozi.
3 hatuna shida na Tupo tayari kushirikiana na
chama chochote kilicho tayari kushirikiana na
sisi ikiwemo UKAWA ili kuunganisha nguvu
kuitoa CCM kwa malengo ya kujenga uchumi
shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora,
wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi
wote na wenye kutokomeza umasikini.
ACT Wazalendo haijatoa kauli yeyote dhidi ya
UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya
watu. Bali tumeweka wazi kuwa lazima misingi
ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika
ushirikiano. Tupo tayari kwa UMOJA. UMOJA ni
moja ya misingi mikuu 10 ya chama Chetu na
Umoja ni nguvu.
Tupo tayari
 
Thubutu. Unadhani Zitto hataki ugali. Yaani Zitto mwenyewe asiseme mtu mwingine aje amsemee?
Nadhani mleta mada, humjui vizuri Zitto.

Hapa chini ni baadhi ya kauli tata za Zitto
1/Sina mpango wa kugombea tena Ubunge 2015
2/ACT siijui ni ya nani na sihusiki na uanzishwaji wake.
3/Sina mpango wa kuondoka CHADEMA na nitakuwa wa mwisho kuhama CHADEMA.
4/Mwaka 2015 nimejipanga kugombea urais na sio ubunge tena.
5/Mara baada ya kuacha ubunge 2015 nitaachana na siasa, nitakwenda chuo kikuu kufundisha.
6/Sina mpango wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya ACT.
7/Sijui chochote kuhusu mpango wa siri wa kina Kitila Mkumba na Samson Mwigamba kuhusu mapinduzi ya kisiasa ya uongozi wa CHADEMA ili mimi niwe mwenyekiti.
8/Mimi ni mjamaa ninayeamini na kuishi sawa sawa na falsafa za mwalimu Nyerere za Kijamaa.
9/UKAWA ni wasaka tonge tu, sina muda wa kushirikiana nao.
10/Sakata la ESCROW ni mimi niliyeliibua, kulisimamia mpaka likafanikiwa kuwaangusha mawaziri bungeni, pasipo mimi kusingetokea kitu.
 
11/Hatuna shida na Tupo tayari kushirikiana nachama chochote kilicho tayari kushirikiana na sisi ikiwemo UKAWA
 
uwongo si siasa ila siasa zina propaganda sasa huyu ni muongo ni mtu anaona wenzie mafala
 
Zzk hana mpango wa kugombea urais ndio maana alisema ikitokea akapatikana mtu wa kugombea atampisha nafasi ya kiongozi mkuu wa chama na yeye kubaki mwana chama wa kawaida
 
Inashangaza mtu katika nafasi ya ubunge anazungumzia kugombea uraisi huku akijua hana umri unaotakiwa its shame
 
Huyu kijana ni sheedaaa hana lolote ni msaka tonge wa kutumainiwa.
 
Chadema zitto amewashika pabaya,hamli,hamlali mnamuwaza
 
Back
Top Bottom