Zitto:Kuomba msaada kwa kila mgeni anayetutembelea nchini awamu hii ni kinyume na Azimio la Arusha

Modibo

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
425
700
" tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; [ ...... ] tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo". - Azimio la Arusha 1967.

Miaka 50 baadaye Hali ni hiyo hiyo. Kila Rais wetu akikutana na Rais wa nchi nyengine au hata Balozi tu inatoka Taarifa kwa vyombo vya habari Tanzania imeahidiwa misaada. Reli kwa mfano, tumeomba na ' kukubaliwa' Uchina. Tumeomba India. Tumeomba Uturuki. Sasa tumesaini mkataba wa ujenzi hakuna hela ya china wala India. Tumetangaza mkataba wa USD 1.2bn wakati kwenye Bajeti tuna USD 450m tu. Tukiendelea kutenga Bajeti kiwango hiki hiki kila mwaka itatuchukua Bajeti 3 kufikisha Reli mpya Morogoro.
Huu ni mfano mmoja tu wa uhalisia wa kuishi kinyume na maono ya Azimio la Arusha. Kwanini tunatangaza maombi ya misaada kana kwamba tumepewa misaada hiyo tayari? Kwanini kila mgeni anayetutembelea sisi tunaomba tu? China Reli na tumekosa. India Reli na mengine wamenyuti. Uturuki Reli na kampuni yao tumeipa biashara tayari. Hata Morocco tumewaomba misikiti na viwanja vya mpira. Miaka 50 mwelekeo wa nchi umebadilika kana kwamba nchi hii haijawahi kuwa na Azimio la Arusha.

Tumekuwa omba omba na kutangaza kuomba omba bila aibu. Azimio lilionya Februari 5, 1967.

Je una nukuu yako ya Azimio la Arusha? Ilete hapa tuijadili na kulinganisha na Hali ya sasa.

14 14
 
uko wapi Zitto? bungeni huonekani rudi tupambane adui ni vizuri kukabiliana naye ana kwa ana kama anavyofanya Lema na LISSU na Lijualikali.Usiku umesonga sana mchana kunakalibia
 
Natamani nimtukane Yuda KABWE. Yeye mbona anazurura huko nje ya nchi akipitisha BAKULI. Sijui anataka nini maana Mradi wa Treni ukikamilika Unafika hadi kwenye Jimbo lake la Kigoma Mjini. Sasa huyu mnafiki utasema ànafikiria wananchi kweli?? Yeye mwenyewe na chama chake ni OMBAOMBA na akipewa misaada hawakumbuki wenzake na ndio maana wanamkimbia kwa USALITI wake.
 
Azimio la Arusha ndilo lililoiingiza hii nchi kwenye lindi la umasikini.

Labda Zitto alikuwa hajazaliwa na hajayaona ya kabla na hakuwepo miaka ya awali ya azimio la Arusha.

Atuulize tuliokuwepo tumpe data za uhakika tungali hai.
Nilisoma sehemu umepigwa Ban ni kweli mkuu???
 
Hauwezi kuleta Azimio la Arusha katika karne hii ya sayansi na teknolojia, na kama kweli ACT wanalitaka Azimio lilozikwa na Azimio la Zanzibar, basi wapinzani wakubali nchi iwe ya mfumo wa chama kimoja.
 
Hivi naweza pata nakala ya Azimio la Zanzibar?
 
Zitto swahiba wako JK ndio alikua bingwa wakuomba Wazungu mbona hukumwabia haya?
 
" tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; [ ...... ] tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo". - Azimio la Arusha 1967.

Miaka 50 baadaye Hali ni hiyo hiyo. Kila Rais wetu akikutana na Rais wa nchi nyengine au hata Balozi tu inatoka Taarifa kwa vyombo vya habari Tanzania imeahidiwa misaada. Reli kwa mfano, tumeomba na ' kukubaliwa' Uchina. Tumeomba India. Tumeomba Uturuki. Sasa tumesaini mkataba wa ujenzi hakuna hela ya china wala India. Tumetangaza mkataba wa USD 1.2bn wakati kwenye Bajeti tuna USD 450m tu. Tukiendelea kutenga Bajeti kiwango hiki hiki kila mwaka itatuchukua Bajeti 3 kufikisha Reli mpya Morogoro.
Huu ni mfano mmoja tu wa uhalisia wa kuishi kinyume na maono ya Azimio la Arusha. Kwanini tunatangaza maombi ya misaada kana kwamba tumepewa misaada hiyo tayari? Kwanini kila mgeni anayetutembelea sisi tunaomba tu? China Reli na tumekosa. India Reli na mengine wamenyuti. Uturuki Reli na kampuni yao tumeipa biashara tayari. Hata Morocco tumewaomba misikiti na viwanja vya mpira. Miaka 50 mwelekeo wa nchi umebadilika kana kwamba nchi hii haijawahi kuwa na Azimio la Arusha.

Tumekuwa omba omba na kutangaza kuomba omba bila aibu. Azimio lilionya Februari 5, 1967.

Je una nukuu yako ya Azimio la Arusha? Ilete hapa tuijadili na kulinganisha na Hali ya sasa.

14 14
Azimio la Arusha lilifia Zanzibar. Sasa Zitto bado anafikiri lipo au?

Ingawa tuliimanishwa kwamba Tanzania si nchi ya kuhitaji msaada wa yeyote au kokote.
 
Kulikataa moja kwa moja azimio ni kukumbatia ubepari na athari zake nafkiri kama lina makosa ambayo kila nikilisoma naona kama yapo basi ni ktk uchumi tuu lakini maadili yapo vizuri. Na wengi wanalolipinga humu wanataka katiba ya warioba ndipo utakapo shangaa
 
Zitto uko serious? Awamu ya tano inaomba misaada ya wageni wanaotutembelea...na awamu ya nne ambao ni marafiki zako na wadau wako wa biashara walifanyaje? Unajua kila mwezi walikuwa wanajazana kwenye ndege kwenda kuomba misaada ambayo haijaja na nchi imefilisiwa na matumizi mabaya ya mapato ya umma. Acha unafiki....huwezi kufika nao popote
 
Azimio la Arusha ndilo lililoiingiza hii nchi kwenye lindi la umasikini.

Labda Zitto alikuwa hajazaliwa na hajayaona ya kabla na hakuwepo miaka ya awali ya azimio la Arusha.

Atuulize tuliokuwepo tumpe data za uhakika tungali hai.
Andika kitabu uweke hizo data zako kwa maandishi....usilete hadithi zenu kama za Abuniwasi
 
Zitto uko serious? Awamu ya tano inaomba misaada ya wageni wanaotutembelea...na awamu ya nne ambao ni marafiki zako na wadau wako wa biashara walifanyaje? Unajua kila mwezi walikuwa wanajazana kwenye ndege kwenda kuomba misaada ambayo haijaja na nchi imefilisiwa na matumizi mabaya ya mapato ya umma. Acha unafiki....huwezi kufika nao popote
huoni hata juzi tumeomba msaada wa kujengewa msikiti na kiwanja cha mpira
 
" tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; [ ...... ] tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo". - Azimio la Arusha 1967.

Miaka 50 baadaye Hali ni hiyo hiyo. Kila Rais wetu akikutana na Rais wa nchi nyengine au hata Balozi tu inatoka Taarifa kwa vyombo vya habari Tanzania imeahidiwa misaada. Reli kwa mfano, tumeomba na ' kukubaliwa' Uchina. Tumeomba India. Tumeomba Uturuki. Sasa tumesaini mkataba wa ujenzi hakuna hela ya china wala India. Tumetangaza mkataba wa USD 1.2bn wakati kwenye Bajeti tuna USD 450m tu. Tukiendelea kutenga Bajeti kiwango hiki hiki kila mwaka itatuchukua Bajeti 3 kufikisha Reli mpya Morogoro.
Huu ni mfano mmoja tu wa uhalisia wa kuishi kinyume na maono ya Azimio la Arusha. Kwanini tunatangaza maombi ya misaada kana kwamba tumepewa misaada hiyo tayari? Kwanini kila mgeni anayetutembelea sisi tunaomba tu? China Reli na tumekosa. India Reli na mengine wamenyuti. Uturuki Reli na kampuni yao tumeipa biashara tayari. Hata Morocco tumewaomba misikiti na viwanja vya mpira. Miaka 50 mwelekeo wa nchi umebadilika kana kwamba nchi hii haijawahi kuwa na Azimio la Arusha.

Tumekuwa omba omba na kutangaza kuomba omba bila aibu. Azimio lilionya Februari 5, 1967.

Je una nukuu yako ya Azimio la Arusha? Ilete hapa tuijadili na kulinganisha na Hali ya sasa.

14 14
UNAOTA NDOTO ZA MCHANA NINII ! NANI ANA HABARI NA AZIMIO HILO ! TOKA MAFICHONI UONE MWANGA !
 
Back
Top Bottom