Zitto: Kuna operation maalum ya kunimaliza (kuniua)

Zitto: Kuna operation maalum ya kunimaliza (kuniua)

AbaMukulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
2,070
Reaction score
3,618
Kupitia account yake ya twitter mbunge wa Kigoma mjini amesema kuna operation maalumu iliyoanzishwa kwa lengo la kummaliza.

Tunafahamu kuwa Operesheni Maalumu #Mzizima2 imepewa kibali kutekelezwa. Dhima ‘ Vita ya Mwisho kuleta Nidhamu kamili’ inataka kinachoitwa kumnyamazisha SAI ( mie huyo ). Wakajipange upya Tu. Mungu tu Ndio anaweza kuninyamazisha. SIOGOPI mwanadamu mwenzangu aslani

We are aware of a special operation to ‘finish’ me off. Special Operation code named ‘Mzizima 2’ has been given the go ahead with the mission ‘Final Battle for the Total Discipline’. The aim of the mission is to completely silence the voice of SAI (aka Zitto). They Better replan

 
Inawezekana kabisa maana ya Lissu yalianza hivi hivi.

Hata Ben Saanane ilikuwa hivi hivi na mpaka leo hajulikani alipo.

Zitto amekuwa akivujisha mambo mazito na sijawahi sikia kakamatwa au kushitakiwa kwa kuchafua watu fulani zaidi ya kushitakiwa hivi karibuni.

Kama madai haya nayo ni ya kweli kama tulivyoona kwa Lissu, basi kuna watu/mtu (mhusika wa mambo haya ) lazima ajiulize ni kwanini siri zinavuja kama kweli wote wanaomzunguka wanamkubali na pia yeye mwenyewe ajitafakari kama yuko .......

Kwa maneno mengine, kama madai haya ya Zitto yana ukweli na siri zinavuja kama hivi, basi wahusika wajitafakari sana kama wako pamoja(wote wanaridhika na matendo haya).
 
Katu siwezi kupuuza madai kama haya!!!

Hata Ben Saanane alitujuza members wenzake hapa hapa JF kwamba anatishia kuuawa lakini, kama ilivyo ada, wakatokea watu wakamkejeli na kumuita anatafuta kiki!!

Thread ile ilifuatia threads zingine 2 tu, na muda mfupi baadae, taarifa za kutoonekana kwa Ben zikaanza kusambaa na hadi hivi sasa hatujui kimemkuta nini hasa!!!

Na ndicho pia kilitokea kwa Tundu Lissu pale aliposema bayana kuna watu walikuwa wanamfuatilia!

Sijapata kughadhibika kama hata baada ya kuwa TL amemiminiwa risasi, bado wakatokea washenzi na kudai hizo ni kiki tu!
 
Nimefurahi tu na Code za Operation umeweka wazi ..hao waliopanga huko wanashangaa sasa hivi hizo info zimevujaje

Haya mashetani yamesha onja damu ya Lissu,Mawazo,Azory ,Ben Saanane na wale waliokuwa wanaelea mto Ruvu kwenye viroba Mwigulu akatuambia ni wahamiaji haramu ,bila kusahau Kibiti hivyo hawawezi acha
Uzuri auwae kwa upanga atauliwa kwa upanga ni swala la muda tu

Na amwagae damu zisizo na hatia laana yake ipo mpaka kizazi cha nne huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katu siwezi kupuuza madai kama haya!!!

Hata Ben Saanane alitujuza members wenzake hapa hapa JF kwamba anatishia kuuawa lakini, kama ilivyo ada, wakatokea watu wakamkejeli na kumuita anatafuta kiki!!

Thread ile ilikuwa ndiyo thread ya mwisho kwa Ben na kiasi cha wiki moja baadae, taarifa za kutoonekana kwa Ben zikaanza kusambaa na hadi hivi sasa hatujui kimemkuta nini hasa!!!
Kwasasa taarifa yoyote ya vitisho c ya kupuuzwa
 
Back
Top Bottom