Zitto kuhamia CUF na kugombea ubunge huko Mtwara

Zitto kuhamia CUF na kugombea ubunge huko Mtwara

Seif al Islam

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
2,156
Reaction score
640
Taarifa zilizopo hapo makao makuu ya cuf maeneo ya buguruni na kuthibitishwa na baadhi ya watu walio karibu na uongozi wa juu wa cuf ni kuwa mbunge wa kigoma kaskazini kupitia chadema bw. zitto kabwe anajiandaa kuhamia cuf na kugombea ubunge wa moja ya majimbo ya mkoa wa mtwara.

Taarifa hizi zinakuja kipindi am,bacho jitihada za zitto mwenyewe na wapambe wake walioko nje na ndani ya chadema kutaka kumpatanisha zitto na mbowe zikiwa zimegonga mwamba hasa baada ya zitto kujikoroga kwa kutoa masharti ya yeye kurudishwa chadema.

Hatua hii ya zitto inachangiwa na kile kinachoitwa kushindwa kwa harakati za chama cha act kujipenyeza katika siasa za mkoa wa kigoma hasa jimbo la kigoma kaskazini ambalo zitto alipanga kugombea ubunge kupitia tiketi ya act.matokeo mazuri ya act katika uchaguzi wa serikali za mitaa ndicho kiliwekwa kama kigezo cha zitto kuhamia act na kugombea ubunge wa kigoma kaskazini.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kwa kuzingatia kuwa cuf ni sehemu ya ukawa, prof. lipumba tayari alishawasiliana na mwenyekiti wa chadema mh. mbowe na kumweleza jambo hilo ambapo mh. mbowe japo alionyesha awali kutoliunga mkono kwa kuzingatia uzito wa hujuma na tuhuma dhidi ya zitto lakini prof.lipumba alimuhakikishia kuwa anammudu zitto na kuwa jambo hilo lisingeharibu wala kuyumbisha mipango ya ukawa kuelekea 2015.Mkutano wa hivi majuzi uliohutubiwa na lipumba na zitto huko mtwara ni mwanzo tuu wa mpango kamambe wa "kumuandalia zitto makao" huko mtwara.

NAWASILISHA.
 
mtasema mengi sana, wana cdm. Sasa akiingia CUF si ukawa ndio umekwisha.
 
Hizo ni tetesi tu, ngoja tuvute subira ili hatimaye tupate kujua ukweli au 'urongo' wa taarifa hizo.
 
CUF atakuwa amepotea njia. Ni bora tu asameheane na akina meku aendelee kubaki CDM.
 
Zitto alikuja Mtwara mwaka 2009 kumzika mke wa Mzee Mandanda maeneo ya sokoni mkwata, uhusiano wa Zitto na huyo mzee inasmekana ni mchumba wa binti yake anayesoma china, basi kama hivyo atakuwa yuko ukweni, atapata company kubwa huko kama akina shilingi,Ley,kitunguu, shabby n.k
 
Itakuwa vema, maana kumpoteza kijana kama yeye sio vizuri.
 
Sidhani kama hilo linawezekana ,ila tuchukulie Zitto ameamua hivyo ,au kwenda Chama kingine chochote labda NCCR ,kinachotokea haswa unapotokea kutokuelewana katika kundi ,inakuwa ni vigumu kuwepo na ushirika wa kimawazo ,ni kitu natural kinakuwepo ambacho hakiwezi kuondoka.

Mfano Zito amerejea Chadema ,kumbuka hakuna mtu mwema anekosa adui hata adui anakuwa na adui yake ,Zito will never be the same as inside CDM and the others also will never be the same with Zito as before ingawa utakuwepo ushirikiano ,ila Zitto ikiwa ameamua kuenda chama kingine basi ushirikiano utakuwa mkubwa huko atakakokuwa na hata ushirikiano mfano wa UKAWA Zito atakuwa hana wasiwasi wa kuwepo mivutano kati yake na CDM ,CDM watakuwa huru dhidi ya Zito nae Zito atakuwa yupo huru zaidi ,ni vigumu kuielezea hii hali lakini natumai imeeleweka.
 
Zitto nenda chama ambacho utakuwa huru katika kupigania maslahi mapana ya Taifa, Bado tuna imani na wewe.Kwani tuhuma uchwara hazijatukatisha tamaa kwakuwa tunafikiri kabla ya kuamua na hatutumii akili za kuambiwa tu bali tunachanganya na za kwetu.
 
Mambo mengine yana sikitisha sana na kushindwa kuamin humu ndani likiandikwa jina la Zitto comment nyingi mara hiv kuna vitu vingi vy kujadili humu nan asiye mjua zitto ni mtu wa media anachezea akili zenu, nguvu y mtu mnapima kweny media kama ananguvu atuambie tuna Madiwan wangap jimbo lake jaman kaz y mtu mnaipimaje? Jiulizeni zito huyu alipita kwa asilimia ngp uchaguz uliopita na kupata upinanzan mkal wa ccm bila hisani ya jk angekua wp leo? Na kauli zake za uoga ntagombea kinondon cjui wp naemjua zito toka mwanzo hakua mpiganaji. Aje atueleze pesa za Uswisi zpo wap tuache ushabik wa kitoto. Aje aseme alikua naibu katibu mkuu ni mtu mkubw chamani tulimpeleka operations za Tanga,Mtwara cost zone yote alipiga compain atuambie tulipata kura ngap? Hakuna asiyejua kama zitto ni mpenda madaraka na kujikweza.. me nashauri tuu aende popote akafanye siasa atafanikiwa naona tatizo ni huo uwenyekiti bila Freeman akuna chadema kw sasa labda badae atokee muadilifu zaidi wa kutoa chama hapa kwend mbele zaid y hapa lakin cyo type ya zito.. nawasilisha
 
Zitto alikuja Mtwara mwaka 2009 kumzika mke wa Mzee Mandanda maeneo ya sokoni mkwata, uhusiano wa Zitto na huyo mzee inasmekana ni mchumba wa binti yake anayesoma china, basi kama hivyo atakuwa yuko ukweni, atapata company kubwa huko kama akina shilingi,Ley,kitunguu, shabby n.k

Sikuwa nafaham hapo kabla kama ZZK anamchumbia mtoto wa mzee Mandanda
 
Taarifa zilizopo hapo makao makuu ya cuf maeneo ya buguruni na kuthibitishwa na baadhi ya watu walio karibu na uongozi wa juu wa cuf ni kuwa mbunge wa kigoma kaskazini kupitia chadema bw. zitto kabwe anajiandaa kuhamia cuf na kugombea ubunge wa moja ya majimbo ya mkoa wa mtwara.

Taarifa hizi zinakuja kipindi am,bacho jitihada za zitto mwenyewe na wapambe wake walioko nje na ndani ya chadema kutaka kumpatanisha zitto na mbowe zikiwa zimegonga mwamba hasa baada ya zitto kujikoroga kwa kutoa masharti ya yeye kurudishwa chadema.

Hatua hii ya zitto inachangiwa na kile kinachoitwa kushindwa kwa harakati za chama cha act kujipenyeza katika siasa za mkoa wa kigoma hasa jimbo la kigoma kaskazini ambalo zitto alipanga kugombea ubunge kupitia tiketi ya act.matokeo mazuri ya act katika uchaguzi wa serikali za mitaa ndicho kiliwekwa kama kigezo cha zitto kuhamia act na kugombea ubunge wa kigoma kaskazini.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kwa kuzingatia kuwa cuf ni sehemu ya ukawa, prof. lipumba tayari alishawasiliana na mwenyekiti wa chadema mh. mbowe na kumweleza jambo hilo ambapo mh. mbowe japo alionyesha awali kutoliunga mkono kwa kuzingatia uzito wa hujuma na tuhuma dhidi ya zitto lakini prof.lipumba alimuhakikishia kuwa anammudu zitto na kuwa jambo hilo lisingeharibu wala kuyumbisha mipango ya ukawa kuelekea 2015.Mkutano wa hivi majuzi uliohutubiwa na lipumba na zitto huko mtwara ni mwanzo tuu wa mpango kamambe wa “kumuandalia zitto makao” huko mtwara.

NAWASILISHA.
Wew dada wew majungu hujaacha tu jaman!!
 
Hizo zitakuwa mbinu za zitto kutaka kung'ang'ania urais,, anataka kutumia huu upenyo wa UKAWA kugombea urais na bado ataleta vurugu ndani ya UKAWA kwa tamaa na mbinu zake chafu kila siku.....
 
Back
Top Bottom