Zitto Kabwe yuko Uingereza: Afanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
Leo asubuhi nimefanya mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza Ndg. Jeremy Corbyn katika Ofisi ya Jimboni kwake Islington Kaskazini.

Tumezungumza kuhusu ujenzi wa Ujamaa duniani katikati ya wimbi la siasa Kali za mrengo wa kulia zinazoendelea sasa.

Pia tumejadiliana wimbi la kubana uhuru wa mawazo na demokrasia Afrika na Tanzania hususan.

Nimempa rasmi mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kidemokrasia wa kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha utakaofanyika jijini Arusha tarehe 25 Machi 2017. Chama cha Labour kimekubali kuhudhuria mkutano huo.

Ndg. Corbyn pia amenialika kwenye mkutano mkuu wa Labour ambapo Seneta Bernie Sanders atahudhuria pia.

Zitto Kabwe
Zitto Z Kabwe

+
 
Kumekuwa na mjadala wa wapi yupo ZZK hasa baada ya kusikika TAARIFA kuwa anatafutwa na Polisi.Leo hapa Uingereza , Ndugu ZZK ameonekana hadharani akiwa na Kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza na ambaye ndio Kiongozi wa upinzani katika Bunge la Uingereza Ndugu Jeremy Corbyn.

Siasa za ZZK ni next level interactions zake katika nyanja za Kimataifa na uwezo wa kupata Taarifa nyeti za kiusalama unamfanya kuwa Kiongozi wa pekee. Ushauri kwa Malaika Mtukufu , badilisha gia za kudeal na huyo jamaa vinginevyo wazungu watakuzuia kukanyaga hata Nairobi , shauri yako.
 
Nakumbuka alishawahi Fanya mazungumzo Na balozi wa uingereza sikumbuki ilikua ishu gani, lakini ni kipindi alipokua mwenyekiti wa poac, Leo baada ya kutoroka anaibukia huko!

Wenye akili kazi kwenu sasa!
 
ACT, tuelewesheni jamani, yupo ziara ya kikazi au ukimbizini?? Ni nini alikifuata huko? Ana ruksa ya mh raisi kusafiri nje ya nchi?? Kidogo natatizika kuwa iweje aende matembezi wakati wenzake ndo kwana wameanza kikao cha bunge??
 
Kumekuwa na mjadala wa wapi yupo ZZK hasa baada ya kusikika TAARIFA kuwa anatafutwa na Polisi.Leo hapa Uingereza , Ndugu ZZK ameonekana hadharani akiwa na Kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza na ambaye ndio Kiongozi wa upinzani katika Bunge la Uingereza Ndugu Jeremy Corbyn.

Siasa za ZZK ni next level interactions zake katika nyanja za Kimataifa na uwezo wa kupata Taarifa nyeti za kiusalama unamfanya kuwa Kiongozi wa pekee. Ushauri kwa Malaika Mtukufu , badilisha gia za kudeal na huyo jamaa vinginevyo wazungu watakuzuia kukanyaga hata Nairobi , shauri yako.
Hahaha tatizo lako umezidisha feeling than thinking.. Magufuli ni baba LA mababa. Next level niamini mimi huo ndio ukweli. Magufuli anafanya vizuri. Hizo nyingine ni sound sound tu.
 
Hongera kwa kuwa Mwanasiasa mwenye exposure na ambaye yuko informed pamoja na mapungufu yako.

Lakini Ujamaa (PURE) haujawahi kufaulu mahali popote duniani. Maana ulithibitika kuhamasisha Uvivu, Kutegeana na Kuzuia wenye uwezo kuendelea hadi kuwasubiri walio chini.
Labda utueleze ni ujamaa upi ambao tuutegemee kutoka kwako.
 
Ama kweli nimekubali wanasiasa wanajua kucheza na akili zetu....
Mpaka sasa najiuliza je kama polisi walikuwa wanamsaka alipitaje airport?
Acha bana, ulishashangaa nembo ya taifa inapita eapot? Ushashangaa vita ya mkuu wa mji panya road na ile kitu inapita wapi?
 
Back
Top Bottom