Zitto Kabwe: What you failed us

Zitto Kabwe: What you failed us

Mario Kejob

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
441
Reaction score
536
The people Kigoma Urban constituency have spoken very loudly and clearly that enough is enough of wasting their precious time of advocacy for issues that matters to them. Over the years, you spent most of your time talking issues of national interest like analysing BOT, IMF and World Bank data and building strong foundation of your young political party.

Sasa basi, mambo ambayo hukuyatetea kwa nguvu zako zote ni haya:
  • Ukamilishaji wa mradi mkubwa wa maji ambao umekuwa ukisusua kwa muda mrefu.
  • Ukamishaji wa barabara ya ushoroba wa kati( Dar-Kigoma) ambayo kwa miaka yako mitano ya ubunge iliyoisha ilitakiwa iwe imekamilika.
  • Barabara ya Kigoma Nyakanazi bado inasuasua mpaka leo.
  • Mpaka leo Kigoma hakuna umeme wa kutosha na kuna megawatts mbili tu za ziada. Sasa huo uchumi wa viwanda utawezekana vipi na umeme huo mdogo?
  • Umeme wa mto Malagarasi hukuupigia chepuo za kutosha.
  • Kwa nusu karne sasa usafiri wa ziwa Tanganyika ulikuwa unategemea sana meli na vyombo kutoka Tanzania. Mimi sio mshabiki wa meli ya Liemba kuendelea kutumika kwani sidhani kama meli hiyo ni sea worthy kutokana na umri wake. Na Mungozo nayo ndio hivyo tena.
  • Kuona tumepigwa bao na Congo kwa kuleta meli mpya na kubwa, kwa kweli nilisikitika sana. Ilitakiwa sisi ndio tuwe na meli kama hiyo. Walioko vitani wametushinda kufikiri kweli!
  • Na nimeona hata baadhi ya viongozi wamesherehekea jambo hili
  • Bandari ya Kigoma ku-operate chini ya Kiwango ambapo imesababisha mdororo wa uchumi mjini hapo. Miaka ya sabini bandari hiyo ilikuwa ina-serve nchi tatu na mkoa wa Kigoma kuchangia asilimia kumi na saba ya pato la taifa.
  • Reli ya SGR kwenda Mwanza kabla ya Kigoma ambapo mzigo mkubwa huenda Congo na sio Rwanda. To your credit, you tried on this one lakini hukuendeleza mapambano.
  • Ujenzi wa High School za kutosha ni kama haupo ukilinganisha na shule za O level zilizopo.
  • Hospitali ya Maweni kuongezwa ubora na uwezo kwani inahudumia mpaka wagonjwa kutoka nchi jirani. Na hii fursa ambayo inaweza kuchangia kwenye pato la taifa.
  • Kutokuwepo kwa University kwenye ukanda huo.
  • Mali ghafi ya kiwanda cha cement ipo ya kutosha tu hivyo uwepo wa Kiwanda hicho ungepunguza gharama za ujenzi na ziada kwenda nchi jirani ambako kuna mahitaji makubwa. Tatizo ni lile lile,umeme.
  • Kiwanda cha kusindika mazao ya ziwani na uwepo wa cold rooms za kuhifadhia.
  • Usisitizo kwenye zao la mchikichi. Ikumbukwe zao hili ndio liliwatoa Malaysia. If they can do it, we can do it too. Hapa ulijaribu kidogo.
  • Jengo la abiria uwanja wa ndege wa Kigoma.
  • Kuirudisha forodha ya Ujiji ambayo ndiyo ilikuwa chanzo kikuu cha mapato cha wakazi wa mji huo. Wakazi wengi waliuhama mji baada ya forodha hii kuondolewa.
- Na last but no the least, mkoa wa Kigoma is very strategically positioned. Una access ya nchi tatu. Sasa, this is a high time kwa Manispaa ya Mji Kigoma- Ujiji kupandishwa hadhi na kuwa Jiji ili iweze kupata necessary finances kutoka serikali kuu katika kufikia azma hiyo. Katika mikoa muhimu mitatu kabla ya uhuru Kigoma ilikuwepo, somehow along the road we lost our way. Ndio maana kabla ya uhuru Kigoma ilikuwa na usafiri wa mjini(dala dala) maji, umeme, simu, treni,meli, uwanja wa ndege na bandari inayohudumia nchi tatu.

Kwa hiyo anatakiwa mbunge atakaye rudisha glory hii ya mji wa Kigoma na si data analysist or a typical politician.

Kazi kwako mbunge mteule.
 
Hakuna rangi tutaacha kuona awamu hii..
Huu ushindi wa kishindo una maana yake "acheni tujipongeze kumaliza upinzani"
Walisema sana wanahujumiwa na wabunge na viongozi wa upinzani wakishirikiana na mabeberu

Nadhani sasa baada ya kukosa scapegoat watahamia kwa wafanyabiashara. Watawa extort watimize matakwa yao ya kusupport majukumu ya serikali or else watabebeshwa furushi la mavi la uhujumu uchumi kwa kushirikiana na mabeberu.

Then watapanda majukwaani kusema wanahujumiwa ndio maana maendeleo hayaji. Mtu una serikali, dola, bunge unahujumiwa vipi?
 
Walisema sana wanahujumiwa na wabunge na viongozi wa upinzani wakishirikiana na mabeberu

Nadhani sasa baada ya kukosa scapegoat watahamia kwa wafanyabiashara. Watawa extort watimize matakwa yao ya kusupport majukumu ya serikali or else watabebeshwa furushi la mavi la uhujumu uchumi kwa kushirikiana na mabeberu.

Then watapanda majukwaani kusema wanahujumiwa ndio maana maendeleo hayaji. Mtu una serikali, dola, bunge unahujumiwa vipi?
Huwa wanatafuta vichaka vyepesi vya kufichia madhaifu yao "hivi kwanini neno mabeberu huwa liko Tanzania tu? Hao tunaowaita mabeberu ndio tunaowakimbilia kila uchao!! Net zao ndio zinawafunika hata haohao wanaowakashifu achilia mbali ile miradi "kwa hisani ya serikali ya kibeberu!!"
 
Unavyolalamika hivi utadhani sehemu nyingine za nchi zimepiga hatua na hilo jimbo la Zitto pekee ndio lipo nyuma kuzidi yote...

Ushawahi kufika kwenye majimbo ya wakongwe kama Chenge, Mkuchika, Lubeleje, Ndugai etc ukajionea mambo yalivyo huko?

Kwanza hata tusiende mbali, hapo hapo mkoni Kigoma, je kuna majimbo mangapi ambayo CCM imekuwa ikiyashikilia tokea mwanzo wa siasa za vyama vingi?

Maana jinsi unavyoandika ni kama Zitto alikuwa mbunge wa mkoa mzima, ni kama Zitto alikuwa mkuu wa mkoa, mkurugenzi wa kila halmashauri, DC wa kila wilaya, etc...
 
Kwani Kigoma ni mkoa mpya Tanzania? hiyo miaka ya nyuma kwanini hawakuyafanya hayo unayoongea? Kigoma utabaki kuwa mkoa maskini sababu ndio sera ya CCM.
 
Jamaa umeandika utasema Zitto ndio mwenye mfuko wa fedha za kutelekeza hayo yote au unadhani yeye ndio mkusanya Kodi?

Ungejua majukumu ya bunge usingeandika haya.
 
Walisema sana wanahujumiwa na wabunge na viongozi wa upinzani wakishirikiana na mabeberu

Nadhani sasa baada ya kukosa scapegoat watahamia kwa wafanyabiashara. Watawa extort watimize matakwa yao ya kusupport majukumu ya serikali or else watabebeshwa furushi la mavi la uhujumu uchumi kwa kushirikiana na mabeberu.

Then watapanda majukwaani kusema wanahujumiwa ndio maana maendeleo hayaji. Mtu una serikali, dola, bunge unahujumiwa vipi?
Wafanyabiashara mbona yameshatukuta mkuu!!!
Tumebebeshwa mamizigo mazito balaa na hawa mawakala wa shetani.
Kwa kweli kwa hali hii,naona investiments zangu zihamazo ntahamishia nchi nyingine,maana walao nyama ya mtu hawaachi.
 
Back
Top Bottom