Zitto Kabwe wewe kwa sasa ni msaada mkubwa sana kwa watanzania baada ya Tundu Lissu na hata wanaokushambulia hawajui kuwa hata wao unawasemea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kwa utawala huu tulionao sasa, watu tukichagua kukaa kimya au tukageuka wapiga makofi, kwa hakika tutaumia na kuteseka sana hasa sisi wananchi wa kawaida.

Ukweli ni kwamba wote tuna wajibu wa kukosoa na kukemea lakini nyinyi wenzetu wenye umaarufu na ambao sauti zenu zinasikika kila kona,mna wajibu mkubwa zaidi na wewe ukiwa mnwanasiasa maarufu unatimiza vizuri sana wajibu wako huo japo siku za mwanzo wa utawala huu kidogo ulikengeuka(ulijisahau).

Naomba nitamke wazi hapa kuwa ni imani yangu kitendo cha hawa mabwana kuchukua wanasiasa wa chama chako ulikuwa ni mpango wa Mungu kwani alijua kitachochea jitihada zako hizi za ukosoaji na hivyo utatimiza kile alichokitaa utimize na hiki si kingine bali ni huu ukosoaji tunaouona leo hii.

Kwa mtazamo wangu,tangu tupate uhuru hakuna awamu inayohitaji ukosoaji kama hii kwani ni awamu iliyosahau kwa kiasi kikubwa maendeleo ya watu na badala yake inajali zaidi maendeleo ya vitu hivyo hatuna budi kupaza sauti.

Hivyo, binafsi yangu navyoona unaandika tweet zanye maneno makali, nafarijika sana kwani ujumbe unafika, unawagusa na unawafanya wajitafakari na kwa njia hiyo unasaidia sana wananchi wa kawaida wakiwemo hata wale vibaraka ambao ni wapambe na wasiojua kuwa hata wao kesho wanaweza kuwa wahanga kwa namna moja au nyingine.

Mfano mzuri ni kwenye zao la korosho, ambapo wewe na wabunge wengine mlisimama kidete kutetea wakulima wa zao hilo ingawa kilioni chenu hakikusikilizwa ila leo tumeanza kuona madhara ya kupuuza hoja zenu na hii ni kupitia tweet za picha anazopost Nape kuonyesha ni jinsi gani zao hilo kwa sasa linashambuliwa na wadudu kutokana na kukosekana kwa dawa zinazotakiwa kupambana na wadudu hao.

Binafsi nasema wewe endelea kupaza sauti kama alivyokuwa anafanya Tundu Lissu na ambavyo anaendelea kufanya hata leo hii kupitia maandishi yake ya mitandaoni maana kila mtu akichagua kukaa kimya basi kwa hakika tutaumia zaidi maana huku kuwasema kunasaidia kuwafanya wasijisahau sana.

Namshukuru pia madam Fatma Karume ambae nae kaamua kuwa mwiba kwa watawala kwa faida ya wange na nina hakika mwenyezi Mungu atawasimamia.

Tunawashukuru sana na Mungu awabarike maana hata nyie mngeweza kuchagua kukaa kimya kama wafanyavyo wasomi wengine wa nchi hii na watu wengine maarufu.

Mko wengi lakini nyinyi niliowataja mmewazidi wenzenu na kwa hakika mmejitoa mhanga.

Hongereni sana.
 
SS umefanyia Zitto dharau kubwa sana na umemtusi .

1. Umesema baada ya kudhuriwa ndipo Xitto ameweza kujaza pengo la Lissu. Mbona Zitto ndiye aliyekuwa mchangia mwenye busara na hoja zenye maana na za kuketa mafanikio zaidi ya Lissu.

2. Umesema mwanzoni wa awamu hii alifanya makosa kwa sababu aliunga mkono kazi za Raisi Magufuli. Sasa kama Raisi alifanya kazi nzuri hastahli sifa.

Kijana kutoka kwenye bongo hadi damu na mpaka kwenye mkojo, una husda, wivu na nia za uchoche,i
 
SS umefanyia Zitto dharau kubwa sana na umemtusi .

1. Umesema baada ya kudhuriwa ndipo Xitto ameweza kujaza pengo la Lissu. Mbona Zitto ndiye aliyekuwa mchangia mwenye busara na hoja zenye maana na za kuketa mafanikio zaidi ya Lissu.

2. Umesema mwanzoni wa awamu hii alifanya makosa kwa sababu aliunga mkono kazi za Raisi Magufuli. Sasa kama Raisi alifanya kazi nzuri hastahli sifa.

Kijana kutoka kwenye bongo hadi damu na mpaka kwenye mkojo, una husda, wivu na nia za uchoche,i
Zitto wa 2016 sio Zitto wa leo wala jana na ukumbuke alikuwa anashambuliwa sana kuwa anasaliti wenzake.
 
nashangaa sna kwa mbowe heche juakali msigwa kukaa kimya kwnye matukio mengi.zitn tu ndyo amekuwa mpinganaji.
 
Zitto amebadilika sasa tunamuelewa vizuri,Tupo naye Pamoja! Mazwazwa ya SISIEMU hayajui kwamba Zitto anawasemea hadi wao walio vifungoni kwa MKOLOMIJE.
 
najua hilo

Lakin watawala ndugu

Sio watu wazur

Labda fatma sabab baba yake yupo kwenye system
Mimi nafurahi hawa niliowataja huwa wanawachana kwa maneno makali ambayo anastshili kulingana na matendo yake.

Wabongo wengi tunaheshimu kile cheo mpaka tunakuwa kama wajinga (vipofu na viziwi) na yeye ana-take hiyo advantage kwasababu anajua wengi wanaogopa kumwambia ukweli wala kuhoji matendo yake.

Huyu mtu ni wa kumchana kama wanavyofanya atachukia lakini ujumbe ataupata na atajitafakari.
 
Back
Top Bottom