Zitto Kabwe unamaanisha nini hapa?


Kaka yangu Watanzania tumekubali kufanywa mazezeta kwa kukubalia haya:

Nikikuchukia basi nataka watanzania wote wakuchukie mfano halisi ni JK chuki ya JK kwa Lowassa imetufanya watanzania wengi tumchukie Lowassa badala ya kuchukia Matendo ya Lowassa na yanayoshabiahiana na hayo mfano ufisadi na rushwa na si kumchukia mtu.Kama tungekuwa na akili kuanzia ndani ya CCM wasingelikubali hilo leo tusingekuwa hapa tulipo.

Pili tunapumbazwa na lugha za vitisho na chuki ili tugawanyike na wachache waendelee kula raslimali zetu bila kutumia nguvu nyingi.Leo tumewekewa chuki na visasi kwa wenye nacho bila kujiuliza utajiri wao umepatikanaje??Hivi ni kweli matajiri waote ni lazima wawe wameiba??Je wanaCCM walioiba raslimali zetu na leo wako madarakani wamefanywa nini??Je hawa matajiri ni hawa wawili tu Manji na Mbowe ndiyo waliyotuletea umasikini Tanzania??Je wale wa Escrow,UDA,Stanbic,Richmond,Kivuko kibovu,nyumba za serikali,Green blblah,makaa ya mawe,madini yetu,hawa viongozi walioletea Taifa hasara wamefanywa nini??Hivi ni halali tuawasulubu hawa wawili tu??

Hivi tumeshindwa kabisa kujiuliza tatizo ni nini??Kwanini tujengewe chuki na viongozi wa dini wakubaliane nayo wanalipwa nini??Ni aibu kwa Taifa lenye viongozi wa dini na wastaafu kuliangalia hili kisa ni uoga,basi bora usizaliwe kama upo kwenye nafasi badala ya kutetea haki uko busy kuongeza chuki,basi hustahili kuishi.

Kuna baadhi yetu ukiona hoja zetu 100% ni Ubaguzi,Chuki na Visasi sababu tu viongozi/watawala hawawapendi wapinzani,kaka tunatakiwa kubadilika.
 
Magufuli Ni Second Nyerere Anaweza Kukosea Mengi kwasababu yeye sio Malaika Lakini Wizi,Hapana..

Hawezi Kuiba hata Tzs100/=..
lumumba "school-of-thought" is very gullible and, at most, very naive

time will tell
 

Mkuu nakuvulia kofia kama hata robo ya watu humu ndani wangekuwa na mawazo kama yako, tungekuwa tunajadili mambo ya muhimu na wanasiasa labda wangebadilika maana wangejua tunakijua nini wanachokifanya. Mitandao imesaidia nchi nyingi duniani kuleta mabadiliko ya kiuchumi na siasa. Lakini mitandao ya Tanzania inawasaidia walio madarakani na wanaotaka kuingia madarakani kufuja kila kitu sababu kitu kikubwa kwako ni support kubwa wanayoipata kutoka kwa makundi yaliyogawanyika.

Makonda kataja majina ya wanaoshukiwa kuwa wauzaji na watumiaji unga. Kashambiliwa na wabunge wa pande zote mbili CCM na UKAWA. Sina hakika kama waliungana kwa kuilinda katiba, niasema hivi sababu kabla ya kutajwa Mbowe na Manji na Zungu hakuna aliyesema hili ni kosa. Hapa ni unafiki mkubwa kwa makundi yite mawili.

CHADEMA walitumia haki gani kumtangaza Lowasa na wana CCM wengine kama ni wezi na mafisadi????
Nape na CCM yake walitumia kifungu gani kumtangaza nchi nzima Lowasa kama ni fisadi wakati mimi na wewe tunajua kuwa Mahakama peke yake ndiyo yenye uwezo kikatiba kumhukumu mtu kama mwizi ama fisadi, naomba wewe unisaidie wapi Nape na Slaa ama Lissu waliitwa na kikao chochote cha Bunge kuulizwa kama Makonda alivyoitwa???? Hakuna jibu la maana utalipata lakini kama ulivyosema hivi sasa mpaka humu JF watu wanajitoa akili kwatetea wabunge kwa kumwita Makonda. mimi binafsi sioni kosa alilolifanya Makonda kwa nchi kama ya kwetu ambayo sijui kama ina Katiba kweli ama ni kama Somalia.

Kuhusu mabadiliko, Ndugu yangu si rahisi kuyapata mabadiliko ya kweli. Mimi ni mmoja wa vijana wa wakati huo mageuzi yalivyoanza na tulihamsika zaidi ya watu uliowaona mwaka jana maana sisi tulitumia akili zetu hatukuwa nyumbu. Tatizo lilonikwaza niachane na siasa za upinzani na kuwa mtazamaji ni pale Kina marando, Lamwai, Mtei, Seif na wengine wengi walipodharau maoni ya wana mageuzi wa kweli kina Mzee Chief Abdalah Fundikira, James Mapalala, kasanga Tumbo na wengine ambao kweli walikuwa wanamageuzi ambao walimsumbua Nyerere miaka ya sitini wakidai vyama walipotaka serikali ya mpito wakati tunaisubiri katiba mpya ambayo ingetutoa na unyonge wa kuwa na katiba ya chama kimoja. NCCR lengo kubwa lilikuwa kuomba katiba mpya lakini njaa ama tama ya madaraka iliwafanya viongozi wetu watufikishe hapa tulipo. Na siku zote hua nasema hii dhambi itawatafuna sana UKAWA sababu walitusaliti watu wengi tuliowaamini.
Wakiwa wanapigwa virungu hua siawaonei huruma. Mtikila watu walimuona kama kichaa lakini kwangu mimi Mtikila alikuwa na maana zaidi kuliko hawa wachumia tumbo wa CCM na UKAWA

Mtikila alifungua kesi kama tatu za kikatiba ambazo
Kesi za kikatiba ambazo aliwahi kuzifungua ni pamoja na kesi ya kutaka wagombea binafsi kuruhusiwa katika uchaguzi Tanzania, wananchi wa Tanzania Bara kuruhusiwa kwenda Zanzibar bila passport na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano bila kuomba kibali toka kwa Wakuu wa Wilaya ama Polisi. Lakini wakati mchungaji Mtikila anapata misukosuko hakuna hata mwanaisasa mmoja wa upinzani alimuunga mkono. mtikila aliishia kupelekwa gerezani kwa kupigania haki za watanzania za kikatiba lakini sasa tuna watu wanaitwa makamanda wanawekwa ndani kwa kutukana lakini tunawaita ndiyo wapigania haki. Haki gani unaipigania kwa kutukana watu??????

CCM na wabunge wake nao wana share ya kuturudisha nyuma kiamendeleo kwa ku ng'ang'ania katiba ya chama kimoja. Historia inatuambia wanyonge hawawezi kubaki kuwa wanyonge siku zote pale Mtikila mwingine akitokea na kutuhamasisha kama Mtikila alivyofanya miaka ile ya tisini pale viwanja vya jangwani najua fika kutakuwa na Burkina Faso ya Tanzania.

Lakini mpaka hapo atakapotokea Mtikila wa 90s' sioni kama kuna mtu yeyote mwenye mapenzi ya hii Nchi zaidi ya matumbo yao awe CCM ama CCM B ambayo ni UKAWA. Na watu wa kuweza kumpa nguvu Mtikila mwingine wa miaka ya 90 ni sisi lakini sioni kama wapo hapa JF zaidi ya makundi ya ku support chuki binafsi.
 

Nitakujibu kwa ufupi ufupi.

Siku ya kwanza walipotajwa akina Wema,Lissu,Esther Bulaya na Halima Mdee walipiga kelele kuhusu hilo wakisaidiwa na Nape Nnauye lakini waliambulia Matusi toka upande wa CCM,ila yalipokuja matusi kwa Wabunge wa CCM ndipo walipostuka kwamba oh kumbe hii siyo kwa wabunge wa Upinzani hata Chama chetu pia tumo.

Hivyo ninapingana na wewe kwamba hawakutetewa,walitetewa na wabunge wa upinzani pamoja na Nape.

Pili tuwe tunajifunza kutokana na Makosa tuliyokwisha yafanya huko nyuma,bado Upinzani wanajitahidi sana lakini je watanzania/raia tunawasupport??Je ni mara nagapi ndiyo wakwanza kuwatukana kwenye mitandao??

Utakubaliana na mimi kwamba si tu tunahitaji Katiba mpya bali tunahitaji ELimu ya URAIA na HAKI za RAIA.
Tunahitaji elimu ya vyama vingi,tunahitaji kukaa chini na kukubaliana ya kale yamepita tugange yajayo,kama TAIFA tunahitaji reconciliation,wengi wameumizwa na tawala zilizopita,tukae chini tureconcile wote tunahaki ya kuishi Tanzania,hakuna aliyezaliwa Tanzania akazaliwa kwa bahati mbaya,ana sababu ya kuzaliwa na kuwa mtanzania.

Tukubaliane,kuzika tofauti zetu,tuanze moja tukubali wote tumeumia tunahitaji "RECONCILIATION" turudi tuwe wamoja tuondoe tofauti zetu.Tukatae kugawanywa kama peremende au lawalawa.Hatuna sababu ya kumsulubu Manji na Mbowe sababu tu tunawachukia,tutakuwa tunawakosea haki,ni watanzania wanayohaki ya kuishi na kuwa treated fairly.

Tukumbuke tukiendekeza Chuki na visasi tunatengeneza vita ya wenyewe kwa wenyewe.Hswa watawala watakimbilia Geneva kwenye Five star hotels wkilipwa DSA na Umoja wa Mataifa ati wanasuluhishwa wakati kama watanzania tunauwezo wa kusema imetosha.Ni wakati wa wewe na mimi kusema basi
 
Zitto ni mdini sana ndiyo maana alitimuliwa na Lisu na kuambiwa katenda makosa 11.

Hii sasa hatari!!! Zitto udini kaanza lini??? Mm namfahamu Zitto toka tukiwa tunasoma UDSM hata msikitini alikuwa haingii sasa huo udini unaouzungumzia ni wa dini gani? Ikiwa Zitto ni mdini basi Waislam wote ni wadini. Sidhani hata kama swala tano inapatikana kwa Zitto!!!
 
Soma tena hujaielewa vizuri mada.Mleta hoja kaanza na maoni yake then akatuweka post iliyowekwa na Zitto Facebook
Alichoandika Zitto ni kipi na alichoandika mtoa mada ni kipi kwa mujibu wako?

Nitajuaje kwamba wewe ndiye uliyeelewa na mimi sijaelewa kama ulivyoandika, na si vinginevyo?
 

Hilo nimeliona. Kuna wakati alitoa list ya vitabu anavyosoma kwa mwaka, ile list haikuwa realistic. Tunaofanya kazi na kupenda kusoma tunajua vitabu vya non-fiction deep type ya "Capital in The 21 Century" kama vile (kitabu kikubwa kuliko biblia unaweza kukitumia kuweka mlangoni ili mlango usijifunge) si vya kusoma 52 au zaidi kwa mwaka, labda kama unasoma summary na review, yeye kaandika kwamba kavisoma vyote. Mbunge mwenye kazi nyingi kusoma hivyo si rahisi, labda kama anasoma kwa kurukaruka chapters.

Inaonekana kusoma kwake hakumsaidii kutokujikanganya.

Alama moja ya kuwa na werevu ni kutojikanganya (non-contradiction).

Alama moja ya kurudia vitu unavyokariri bila kuelewa ni kujikanganya.

Zitto anapompinga Magufuli kwa sababu zile zile ambazo zinamfanya amsifie Putin, anajikanganya na kutuonyesha kwamba, ama anatuhadaa, ama anakariri anachosoma na kukirudia bila ya kuwa na werevu wenye kina.

Hayo yote mawili ni mabaya sana kwa kiongozi wa kitaifa.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sasa inakuwaje Zitto ampinge Magufuli na kumpenda Putin wakati wote wamoja tu?
 
Mkuu Al-Watan,naamini hujamuelewa Mh. Zitto. Rudia kusoma tena kwa umakini. Kuna maoni ya mleta uzi kwanza,halafu ndio akaweka maandishi ya Zitto.
 
Sasa inakuwaje Zitto ampinge Magufuli na kumpenda Putin wakati wote wamoja tu?
Anayempenda Putin ni mwanzisha uzi ambaye ameanza kwa kuweka maoni yake na akamalizia kwa kuweka andiko la Zitto.
Mkuu napata shida kuelewa uelewa wako.
 
Anayempenda Putin ni mwanzisha uzi ambaye ameanza kwa kuweka maoni yake na akamalizia kwa kuweka andiko la Zitto.
Mkuu napata shida kuelewa uelewa wako.

Hii post nzima kuielewa ni lazima ujivue werevu na kufikiri kama mtu asiyejua kuandika kwanza.

Mana haielezi vizuri wapi maneno ya mleta mada yameanzia na kuishia na wapi maneno ya Zitto yameanzia na kuishia. Na unaweza kuona kwamba mleta mada alipoandika kwenye mabano (Nakuwekea hapo chini).. kuwa ndiyo mwisho wa alichoandika mleta mada na mwanzo wa alichoandika Zitto na kutoelewa nani kaandika nini.

Je, maneno ya

Ndiyo maana inakuwa vigumu mimi kuielewa na wewe kuelewa uelewa wangu.

Sasa hapa unajuaje alichoandika Zitto ni kipi na alichoandika mtoa mada ni kipi? Mwanzo na mwisho wa kila mmoja wa hawa wawili unaujuaje?

Kama Zitto anampinga Putin na Magufuli, then that is consistent.

But how do you know that from reading this incoherent patchwork?

Soma tena

 
Joel Nimeenda mwenyewe kumsoma Zitto huko FB, maana naona ukimsoma mtoa mada, kwa uandishi wake usio na kituo wala kanuni, unaweza kufikiri Zitto anampongeza Putin, kitu ambacho si kweli.

Nimeona Zitto anamfananisha Putin na Magufuli, which is sensible and consistent with logical thinking.
 
Akhsante mkuu Al-Watan,nimependa uamuzi wako wa kwenda kumsoma Zitto mwenyewe huko FB. Nakupa kongole. Humu JF kwa kweli siku hizi mkuu lazima tuwe waangalifu sana tunapochangia maana kuna watu wanapenda kuandika,wanacho cha kuandika ila hawawezi kuandika,na si kosa lao kwani uandishi ni kipaji na ni taaluma. Tuvumiliane na tuchukuliane.
 


Si umeona enheeee, nakiri kabisa kuwa huyu kijana bado hajitambui na ndiyo maana wenzake wanamcheka. Anapingana na Magufuli, kisha hapo hapo anakuja kumsifia Putin kufanya yale anayofanya Magufuli.
 
Magufuli Ni Second Nyerere Anaweza Kukosea Mengi kwasababu yeye sio Malaika Lakini Wizi,Hapana..

Hawezi Kuiba hata Tzs100/=..
Hiv kujenga uwanja chato huo sio wizi , kujenga Bandar ya samaki huko ziwa Victoria baadala ya mikoa ya mtwara au tanga huo sio wizi, afu huwez kumfananisha hayati baba wa Taifa na maguful hata kidogo yule Mzee hakuna kiongoz wa kumfikia kwa hapa bongo alitenda Mema mengi . hawa wengine wezi tu
 

[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Si umeona enheeee, nakiri kabisa kuwa huyu kijana bado hajitambui na ndiyo maana wenzake wanamcheka. Anapingana na Magufuli, kisha hapo hapo anakuja kumsifia Putin kufanya yale anayofanya Magufuli.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…