Zitto Kabwe unamaanisha nini hapa?

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,766
5,904
Kuna Post Kaiweka Zitto Kwenye Ukurasa wake wa facebook(Nakuwekea hapo chini)..

Kwangu mimi kwa namna yeyote Ile Putin ni kiongozi bora Mno kwenye karne ya sasa na mfano wa kuigwa,Ameirudisha Russia Kwenye Mstari Na Inaheshimika Na kusikilizwa Duniani Kuliko Alivyoikuta..

Hivyo Kama Zitto Kabwe Amemaanisha chochote Kile Akidhani Ni kibaya 'KAFELI' Putin ninkiongozi Bora..

Post ya Zitto Kabwe Facebook..

"Msomeni Putin mumwelewe. Niliwaambia mwezi July. Narudia tena msomeni Putin na vita yake na Oligarchs ( MATAJIRI )

Putin aliingia kwenye madaraka mpweke akiwa hana kundi lake. Duma ( Bunge) lilijaa watu ambao hawakumwunga mkono na Warasimu wote walikuwa hawana uhusiano naye. Siasa zilikuwa zimeshikwa na matajiri ( oligarchs) na kuamua watakacho. Alisimika utawala wake kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwemo;

- aliteua watu wake wa karibu aliofanya nao Kazi huko St. Petersburg, pia watu aliotoka nao eneo moja na alioamini nao Dini moja.

- Alihakikisha Matajiri wote wanashughulikiwa na kuwafunga au kuhama Nchi. Yeyote ambaye alimtilia mashaka alimtoa Serikalini au kwenye Mashirika ya Umma hata ikibidi kwa tuhuma za kutungwa na wengine WALIPOTEZWA kabisa.

- Aliwapa fursa za utajiri watu wake wa karibu na kujenga ' new oligarchs ' kupitia zabuni za Serikali na Miradi mikubwa mikubwa ya Miundombinu aliyoanzisha kwa haraka alipoingia madarakani
Alifanya haya kuimarisha UTAWALA wake. Msomeni Putin mpanue maarifa".
 
Waingereza walisema "a little knowledge is dangerous indeed".

Mtu anaandika kama mtoto wa sekondari ya chini mwenye utashi wa juu na uelewa wa kati.

Polite societies ought to shun Machiavellianism and dictatorships, at least publicly.
 
Plain and clear...Magufuli anatengeneza oligarchy yake...watapiga deals humo mpaka nchi ikauke...Kikwete na oligarchy yake waliinyonya nchi, Magufuli na yake wataifyonza, wataikamua na mwisho wataikausha kabisa.
[HASHTAG]#gomagufuligo[/HASHTAG] [HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG]
 
Magufuli Ni Second Nyerere Anaweza Kukosea Mengi kwasababu yeye sio Malaika Lakini Wizi,Hapana..

Hawezi Kuiba hata Tzs100/=..
 
I have the same feeling about awamu hii
 
Magufuli Ni Second Nyerere Anaweza Kukosea Mengi kwasababu yeye sio Malaika Lakini Wizi,Hapana..

Hawezi Kuiba hata Tzs100/=..
Magufuli hana falsafa ya kisiasa anayoijua au kuifuatilia, Nyerere alikuwa na falsafa ya kisiasa aliyoijua, kuiishi na kuiandika kirefu.

Kama Mwinyi alisema kumfananisha yeye na Nyerere ni kuufananisha mlima Kilimanjaro na kichuguu, basi kumfananisha Magufuli na Nyerere ni sawa na kumfananisha mchwa mfu mmoja anayekaa kwenye kichuguu hicho na mlima Kilimanjaro.
 
Waingereza walisema "a little knowledge is dangerous indeed".

Zitto anaandika kama mtoto wa sekondari ya chini mwenye utashi wa juu na uelewa wa kati.

Polite societies ought to shun Machiavellianism and dictatorships, at least publicly.

Zitto kusema anampenda Putin- unless anafanya satire kwa Magufuli- na kumpinga Magufuli, ni contradiction.
Ulichokielewa wewe usilazimishe kuwa ni uelewa wa wote.Panua maarifa
 
Back
Top Bottom