Zitto Kabwe unamaanisha nini hapa?

Huyo unaye msujudia ndo atakuchanganya ova zege. Eg 'mgogoro wa zenji nitautatua' Mara 'wana mamlaka yao, wautatue wenyewe'
 
Honest uwa naumia sana pale ninapoona mwanasiasa, ama kwa kuelewa au kutokuelewa anapotosha umma kwa makusudi

Suala la Russia na Putin pamoja na matajiri (Oligarchs) mara nyingi limekuwa likipotoshwa na mataifa ya magharibi kwa maslahi yao binafsi, nasikitika nawe mh mbunge unayejipambanua kuwa ni mwana demokrasia mahiri,
Nawe unaangukia katika mkondo huo potofu

Turejee katika mada yetu,baada ya kuvunjika kwa Soviet union ( USSR) katika miaka ya mwanzoni wa tisini, na kuzaliwa kwa Russia fedelation, kama wengi tunavyojua kuna mageuzi makubwa sana yalitokea kiuchumi, ambapo walitoka kuwa state own economy kwenda kuwa free market economy

Ambako kwa kutumia mwaya huo watu wachache waliokuwa na mahusiano ya karibu ya Rais wao wa wakati huo, mlevi Boris Yelstin walitumia mwaya huo kwa kununua makampuni mengi hasa mafuta, ambayo yalikuwa yanamilikiwa na Serikali kwa bei ya kutupa
Na hapo ndio likawa chimbuko kubwa la kuifanya Russia kuwa ni moja ya taifa lenye mabilionea wengi hapa duniani

Hiyo ikawa ni moja ya fursa kubwa sana, iliyotumiwa na mataifa ya kimagjaribi hasa Marekani na kibaraka wake mkubwa Uingereza kuanza kujiingiza moja kwa moja katika uchumi wa Russia
Hasa ukizingatia Russia ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa sana wa natural resources kama gesi na mafuta

Hatua hiyo ilipelekea Russia, ambayo wakati fulani ilipata kuwa moja ya nchi zenye nguvu kubwa sana ya kijeshi, kupoteza ushawishi wake katika siasa za kimataifa

Hilo lilikuwa ni moja ya kosa kubwa sana kufanywa na Bwana Boris Yelstin, bahati nzuri aligundua kosa lake, wakati moja aliwahi kukiri katika kitabu chake
Kitu kilichomfanya kutafuta mtu madhubuti na imara, atakaye kuwa mrithi wake, ndipo alipomuibua Bwana Vladimir Putin ( former KGB, shirika la ujasusi la USSR na baadaye RUSSIA)
kumfanya waziri nkuu wake na baadaye Rais

Alipoingia madarakani moja ya jambo alilofanya Putin, ni kuwaita hao matajiri wa Russia ambao kiukweli utajiri wao mwingi ulitokana na Rushwa na ufisadi, na kuwaomba wasahau ya nyuma ila waungane naye na kuijenga Russia mpya yenye nguvu kama zamani
Na aliwaambia anawajua wote na ni kwa namna gani walipata utajiri wao, ukizingatia alikuwa ni jasusi wa zamani

Kwa hatua hiyo baadhi ya matajiri( oligarchs) walikubaliana naye mfano Roman Abrohonovic ila baadhi walimpinga kwa nguvu zote wakiamini baadhi ya maslahi yao binafsi yatakoma mfano kina Mikhail Khodorkovsky, ambao walianza mbinu za kusupport upinzani na kumwamisha Putin, na kweli aliwashughulikia

Hivyo basi Putin sio dikteta kama unavyodhani ila ni kwa sababu amezuia maslahi ya mataifa ya magharibi hasa Marekani, na kuifanya Russia sasa kuanza kuheshika duniani

Acha kupotosha umma
 
Una maana Lowasa angeshinda hangetengeneza oligarchy yake na kufyonza na kukamua hazina ya nchi?
 
Mtaji wa oligarchy ya namna hiyo ni ujinga na kwa sababu ndani ya taifa letu mtaji huo umetamalaki, Magufuli anaanza na mtaji uliojitosheleza.
 
Mtaji wa oligarchy ya namna hiyo ni ujinga na kwa sababu ndani ya taifa letu mtaji huo umetamalaki, Magufuli anaanza na mtaji uliojitosheleza.
Kabisa. Watanzania tuna ujinga wa kiwango kisicho na mpinzani...
 
Kabisa. Watanzania tuna ujinga wa kiwango kisicho na mpinzani...
Hebu fikiria hili...mtu na akili zake timamu anashangilia uvunjwaji wa Katiba ya nchi na mtu aliyeapa kuitetea na kuilinda, mtu na akili zake timamu anasikia raha jirani yake kuteswa na vyombo vinavyotakiwa Kikatiba kumpa ulinzi, mtu na akili zake timamu anaposifia utawala kuwanyanyasa wawakilishi wao waliowachagua...ni zaidi ya ujinga, ni uenda wazimu!
 
baada ya magufuli kufeli kila idara ataanza kukwapuaa mali za umma
 
Soma tena hujaielewa vizuri mada.Mleta hoja kaanza na maoni yake then akatuweka post iliyowekwa na Zitto Facebook
 
Anachowanyia wafanya biashara magufuli ndicho kinachomsukuma Zitto aandike. Thanks Zitto wachache tunakuelewa kabisa
 
Magufuli Ni Second Nyerere Anaweza Kukosea Mengi kwasababu yeye sio Malaika Lakini Wizi,Hapana..

Hawezi Kuiba hata Tzs100/=..
Watanzania sasa hivi wamekuwa masikini zaidi, hii ni aina fulani ya wizi pia. Au maisha ya wananchi yameimarika zaidi leo chini ya awamu ya 5?

Mkulu amezikusanya zote kutoka mifukoni mwa wadanganyika na kuwaacha wadanganyika na mifuko iliyotoboka.Pia anawaambia "mwafaa!"

Wadanganyika kiuchumi wanamuona Kikwete malaika. Usipokubali kuliwa .........

Wizi uko wa aina nyingi....
 

Najua tulikosea lakini bado dhana ni ile ile tunahitaji MABADILIKO Kiuchumi,kisayansi na kisiasa.Tunahitaji UHURU wa kuongea,kukosoa,kupata taarifa na kuwa mwanachama wa Chama chochote cha siasa mradi huvunji sheria za nchi.

Tunahitaji Rais ambaye ni Mvumilivu,mwenye busara,hekima na upendo ambaye haangaishwi na tuvijineno tusikokuwa na maana.Anayejali watanzania bila kujali itikadi,kabila,dini,rangi au ukanda.

Tunahitaji Rais ambaye kwake UBAGUZI,CHUKI,na VISASI havipo ndani ya moyo wake.Inshort tunahitaji Rais anayemuogopa Mungu na anaonyesha kumuogopa Mungu kiukweli.
 

Zitto ni mtu anayeenda kusoma higlights za kitabu au Makala maalum kisha anakariri vitu na kufanya kuwa msimamo wake wa kisiasa. Kwa kweli ninaposikia maoni yake uwa nacheka sana maana he never makes any sense Zaidi ya kujisusha kisiasa. Mtu gani anaendesha maisha kwa kukariri vitu kila kukicha?
 
Huyo unaye msujudia ndo atakuchanganya ova zege. Eg 'mgogoro wa zenji nitautatua' Mara 'wana mamlaka yao, wautatue wenyewe'


Endelea kumsujudu Zitto tu, utakuja kunitafuta huku ukilia. Zitto si mwanasiasa aliyekomaa, he never makes sense kwa ayasemayo....yeye anakariri tu vitu hata kama haelewi vina maana gani na ndiyo maana anajichanganya. Mfuatilieni tu labda abadilike leo hii baada ya kusoma huu ujumbe wangu.
 

Nimeipenda hiyo kauli na ndiyo baadhi yetu humu ndani tuna mawazo kama hayo tofauti kubwa ni kwamba watu kama wewe na mimi tukisema kitu ambacho hakiungi mkono moja ya makundi haya mawili hatujibiwi kama wewe ulivyonijibu mimi bali tunatukanwa. Mimi nilichokisema hapo kinatofautiana kidogo sana na ulichokisema lakini kuna watu wamenitukana. Angalia hapo chini nilichojibiwa
Mbase1970 said:
Kwasababu hiyo hiyo ndiyo iliwapa watanzania wakati mgumu wakati UKAWA ilipompitisha mwana CCM mwingine awe mgombea urais wakaona bora waendelee na wale CCM A. Hatutapata mabadiliko kwa siasa hizi zilizopandikizwa na CCM mpaka tutakapoamka na kutumia akili zetu tulizopewa na Mungu kuliko kutumiwa na wanasiasa wa CCM na UKAWA maana wote ni walewale tofauti wamebadilisha rangi ya uniform zao kutokakijani mpaka magwanda na wengine wamebaki na mashati ya kijani. hawa wa mgwanda mengine ni vinyonga hatuujui uwezo wao wa ulafi ukoje kama ni zaidi ya hawa tulionao ama wana unafuu... Mungu anajua maana tumeshalaanika
Click to expand...
Hizo pumba. Kale na mkeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…