Zitto Kabwe: Tundu Lissu asema ''sikati tamaa na watanzania''

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Sikati tamaa na Watanzania - Lissu

Tangu jana Jumapili, Februari 11, 2018 niko kikazi nchini Ubelgiji, kwa ziara ya Kichama na Kiuwakilishi, nikikutana na wabunge wa vyama vya Kijamaa vyenye uwakilishi katika Bunge la Ulaya hapa Brussels, tukijadili kwa upana kuhusu masuala ya Demokrasia na nafasi ya vyama vya Kijamaa ulimwenguni katika kuhakikisha uwepo wa Demokrasia pana. Pia ziara yangu inahusisha kazi za Uwakilishi kama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, na Diwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia chama cha ACT Wazalendo, nikizungumza na taasisi mbalimbali juu ya maendeleo ya wananchi ninaowawakilisha.

Jana jioni pia nilipata fursa ya kumsabahi Mbunge, Kiongozi mwenzangu wa kisiasa, na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, TLS, ndugu Tundu Lissu anayeendelea na matibabu hapa Ubelgiji. Nimefurahi kumwona Lissu akiwa anaendelea vizuri, na afya yake kuzidi kuimarika. Nikilinganisha na hali niliyomwona nayo jijini Nairobi, Septemba, mwaka jana, ni dhahiri kwamba Mwenyezi Mungu amepitisha uwezo wake na kumponya mja wake.

Nimezungumza naye mambo mengi, hasa kuhusu Nchi yetu, na pia kuhusu dunia kwa ujumla. Miongoni mwa mambo ambayo tumeyazungumza na ninaona ni muhimu kuyaweka wazi ni yafuatayo:

Mosi: Suala la Gharama za matibabu yake. Lissu anasikitika kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo sio tu halimhudumii Lakini pia hata stahili zake za msingi kama Mbunge hapewi. Licha ya kutibiwa kwa misaada ya wasamaria wema, lakini ana mahitaji mengine kama mwanadam na wajibu kama mzazi. Sheria ya Bunge imeweka wazi kuwa Mbunge anapokuwa ametibiwa nje ya nchi Bunge humgharamia maisha yake.

Tangu Septemba, 2017 Bunge halijampa Mbunge wa Singida Mashariki haki zake za kisheria. Bunge limesukuma wajibu huo kwa Serikali, Wizara ya Afya na linasema kuwa linasubiri urasimu wa Serikali. Inasikitisha sana. Ikumbukwe kuwa mmoja wa wataalamu waliosaidia Lissu kupata huduma ya kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Mkoa ya Dodoma, mara tu baada ya kupigwa risasi, ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.

Mzunguko ambao unafanywa na Bunge kuhusu suala lililo wazi kabisa la kugharamia maisha ya Mbunge aliye kwenye matibabu linatia simanzi sana. Ninamsihi Spika wa Bunge, achukue hatua kwenye jambo hili, Bunge litimize wajibu wake kwa Mbunge wake kwa mujibu wa sheria. Kuendelea kuvuta miguu katika suala hili kunaleta hisia mbaya, na kunajenga taswira mbaya ya Bunge letu.

Pili: Suala la uchunguzi wa shambulio lake. Mpaka sasa ni miezi mitano imepita tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi, na hakuna taarifa yeyote kuwa mamlaka za uchunguzi zimewakamata wahusika au kuonyesha tu juhudi za kuwatafuta wahusika. Jambo hili linatoa taswira mbaya sana juu ya vyombo vyetu vya uchunguzi, linajenga chuki na linaondoa imani ya wananchi kwa vyombo hivyo.

Ombi la Lissu kwangu ni kuwa tuendelee kupaza sauti ili uchunguzi ufanyike na kuwakamata wahusika waliomshambulia. Iwapo watu hawa hawatachukuliwa hatua wataendelea kuumiza watu wengine. Jeshi la Polisi linapaswa kueleza umma limekwama wapi kwenye uchunguzi wa tukio hili baya kabisa kuwahi kutokea katika nchi yetu, la mbunge kushambuliwa kwa risasi katika eneo la Bunge, akihudhuria vikao vya bunge.

Ni jambo la aibu kubwa kwa nchi yetu kuwa Mbunge anashambuliwa mchana kweupe na vyombo vya uchunguzi vinashindwa kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwakamata wahusika. Kitendo cha Serikali kukataa kuchunguza shambulio hili ni ishara kuwa Serikali inawajua waliomshambulia Lissu, na hivyo imeamua kuwalinda. Jambo hili ni baya sana kwa ustawi wa haki katika nchi yetu.

Tatu: Lissu ameniambia kuwa sasa anapata muda mrefu wa kutosha wa kujisomea vitabu, na yeye hupenda kusoma kitabu chochote ili kuwa na MAARIFA mapana zaidi. Nami nimempa zawadi ya vitabu kadhaa, kikiwemo kitabu cha Thomas Picketty cha CAPITAL in 21st Century ambacho nimemsihi akisome kwa kina kwani kitamsadia kuelewa namna tofauti ya kipato kati ya wenyenacho na wasionacho ilivyoongezeka duniani kote.

Pia tulibadilishana mawazo na juu ya mbinu za mapambano ya kuleta mabadiliko nchini kwetu. Lissu ameniambia maneno yafuatayo “Wananchi wanajua wanataka nini, sisi Viongozi ndio tupo nyuma na Wananchi wapo mbele kimawazo. Jambo moja lipo wazi sana kwangu nalo ni kuwa sikati tamaa na Watanzania“. Mwisho wa kunukuu.

Nimemtakia kheri na kumuombea apone haraka.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Brussels
Ubelgiji
Februari 12, 2018
 
-Ni jambo la aibu kubwa kwa nchi yetu kuwa Mbunge anashambuliwa mchana kweupe na vyombo vya uchunguzi vinashindwa kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwakamata wahusika. Kitendo cha Serikali kukataa kuchunguza shambulio hili ni ishara kuwa Serikali inawajua waliomshambulia Lissu, na hivyo imeamua kuwalinda. Jambo hili ni baya sana kwa ustawi wa haki katika nchi yetu.
 
Pili: Suala la uchunguzi wa shambulio lake. Mpaka sasa ni miezi mitano imepita tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi, na hakuna taarifa yeyote kuwa mamlaka za uchunguzi zimewakamata wahusika au kuonyesha tu juhudi za kuwatafuta wahusika. Jambo hili linatoa taswira mbaya sana juu ya vyombo vyetu vya uchunguzi, linajenga chuki na linaondoa imani ya wananchi kwa vyombo hivyo.
Haki ingekuwa inatendeka kwa uzembe huu wa makusudi uliofanywa wahusika wangekuwa wameshatumbuliwa kwa kushindwa kuwajibika ila kwa kuwa aliyefanyiwa ni Lissu wa upinzani wahusika wameachwa waendelee kula kuku kwa mrija.
 
Kama una mambo yako ya kufanya - fanya tu - hapa Tanzania siasa ni unafiki mtupu, uadui na kila aina ya ubaya. Na mbaya zaidi ni pale unapoenda tofauti na mtu mwenye kuweza kuamlisha wengine wakutende vibaya.
Mungu anajua ..
 
Yote yana mwisho...........Ugua pole Lissu, walitaka roho yako Mungu hakuwa tayari kuwapa, jiuguze kwa chochote kidogo utakachopata toka kwa wana Wa Mungu.......usisononeke moyo ukawapa Miungu ya shaba nafasi ya kukuzodoa........Kama Mungu alikuponya na risasi, jua kabisa hatakuacha uaibike kwa kukosa hela ya matibabu.
 
-Ni jambo la aibu kubwa kwa nchi yetu kuwa Mbunge anashambuliwa mchana kweupe na vyombo vya uchunguzi vinashindwa kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwakamata wahusika. Kitendo cha Serikali kukataa kuchunguza shambulio hili ni ishara kuwa Serikali inawajua waliomshambulia Lissu, na hivyo imeamua kuwalinda. Jambo hili ni baya sana kwa ustawi wa haki katika nchi yetu.
Wanawapa sababu watu kuhisia serikali inahusika bila sababu za msingi. Chombo cha upelelezi kinatakiwa kutoa mrejesho wa mara kwa mara ili angalau kuonekane juhudi zinazofanyika. Hii ya kusema upelelezi hausemwi umepitwa na wakati kwa sasa, maana watu wanaona nchi nzingine inavyofanyika panapotokea matukio kama haya.
 
Tangu lini muuwaji akajichunguza na kujifunga mwenyewe!? Jamani, tafuteni mbinu nyingine ya kuwabaini hawa magaidi wa TZ bila msaada wa Serikali hii Ovu la sivyo, mapovu yatawatoka hadi yatawakauka! Hivi karibuni Mh.Zitto, ameilaumu TISS na udhaifu wake, ssa hii Taasisi pamoja na Police wanaweza kuchunguza swala hili la kupotea kwa watu na kupiga hovyo, watu Risasi!? Mambo mengine nikupoteza muda kuyaongelea bila matendo ya moja kwa moja. Anyway, ninampongeza Mh. Zitto kwa kujali kumtembelea Mh. Lissu Hospital
 
Mungu wa mbinguni ninakushukuru baba kwa ajali ya maisha ya mja wako tundu lissu,, ninakuomba baba usimpungukie kaaa naye uendelee kumuimarisha afya yake iwe njema,, Mungu wa haki hakika wewe wawajua watesaji wa lissu nakuomba baba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako,, maana kisasi ni juuu yako Mungu,, ninaomba na kushukuru katika jina lako Mungu.
 
Back
Top Bottom