mtanzania1989
JF-Expert Member
- May 20, 2010
- 4,066
- 6,760
Acha siasa nyepesi, serikali imeshakuhakikishia ndege yetu si miongoni mwa "terrible teen", wewe unaendelea tu neno la Mange na Zitto, muda utawaumbua tu.Sasa kama na hawa wameanza mambo haya hatuna wa kumuamini ndani ya ccm
Zitto ameishiwa siku hizi, hana tofauti na Mange tu, mnunuzi serikali anakwambia ndege yetu sio miongoni mwa "terrible teen", muuzaji na yeye data zake zinaonyesha hivyo hivyo, yeye third part anaendelea kung'ang'ania ni terrible teen, hakuna cha kumsaidia zaidi ya kuacha muda uje kumuumbua tu.
Acha siasa nyepesi, serikali imeshakuhakikishia ndege yetu si miongoni mwa "terrible teen", wewe unaendelea tu neno la Mange na Zitto, muda utawaumbua tu.
Mahakama za mafisadi zipo kwanini musimshitak??Bora huyu walau zimekuja ndege mbovu, angekuwa yule boss wenu wa mafisadi tungeambulia vumbi tu!
Siasa nyepes zp mkuu hilo suala lipo usubir ni muda tu utaongeaAcha siasa nyepesi, serikali imeshakuhakikishia ndege yetu si miongoni mwa "terrible teen", wewe unaendelea tu neno la Mange na Zitto, muda utawaumbua tu.
Sasa kama siyo terrible teens ni ndege za aina gani? Mbona Serikali haisemi ni series ipi ya Dreamliner?Acha siasa nyepesi, serikali imeshakuhakikishia ndege yetu si miongoni mwa "terrible teen", wewe unaendelea tu neno la Mange na Zitto, muda utawaumbua tu.
hawakuwa JPM na PS wa wizara ya fedha peke yao ongeza na Daudi Bashite....
Zitto ameishiwa siku hizi, hana tofauti na Mange tu, mnunuzi serikali anakwambia ndege yetu sio miongoni mwa "terrible teen", muuzaji na yeye data zake zinaonyesha hivyo hivyo, yeye third part anaendelea kung'ang'ania ni terrible teen, hakuna cha kumsaidia zaidi ya kuacha muda uje kumuumbua tu.
kama ndege aliyonunua Magu na Mwanae dotto ni boeing 787-8 LIN 20 hiyo ni terrible teens. hata ukidhikiri uchi haitabadili ukweliZitto ameishiwa siku hizi, hana tofauti na Mange tu, mnunuzi serikali anakwambia ndege yetu sio miongoni mwa "terrible teen", muuzaji na yeye data zake zinaonyesha hivyo hivyo, yeye third part anaendelea kung'ang'ania ni terrible teen, hakuna cha kumsaidia zaidi ya kuacha muda uje kumuumbua tu.
sasa mnunuzi mwenyewe ni dereva wa lori, tutegemee nn tena hapoANAANDIKA ZITTO KABWE: SERIKALI INAFICHA JAMBO KUHUSU DREAMLINER 787-8
“Serikali inaficha jambo kuhusu Dreamliner 787-8, Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli. Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Hivi sasa kuna ushindani mkubwa kati ya Kampuni ya GE ya Marekani na Kampuni ya Rolls Royce Uingereza kuhusu nani apate biashara ya injini hiyo.
Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi. Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.
Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili. Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei. Bahati mbaya Sana mazungumzo hayo yalimhusisha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao. Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya.
Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu. Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.
Zitto Kabwe
3/5/2017
Zitto ameishiwa siku hizi, hana tofauti na Mange tu, mnunuzi serikali anakwambia ndege yetu sio miongoni mwa "terrible teen", muuzaji na yeye data zake zinaonyesha hivyo hivyo, yeye third part anaendelea kung'ang'ania ni terrible teen, hakuna cha kumsaidia zaidi ya kuacha muda uje kumuumbua tu.
Mkuu,hi comment anzishia uzi wake unaojitegemea.Nafikiri tunamiss point. Kwanza tungehoji ununuzi wa ndege moja tu ya aina hiyo. Ikiwa kweli biashara itachanganya na ATCL ikapata wateja wa kujaza ndege hiyo kwa route anayoisema Mh Rais (route ya Marekani hadi Kilimanjaro), je kukitokea tatizo watatumia ndege gani kuhudumia njia hiyo? Kumbuka pia kuwa ndege zina matengenezo yake kwa mujibu wa ratiba ya matengenezo na mengine uchukua hadi zaidi ya wiki mbili. Je kipindi hicho watatumia ndege gani. Hii ni moja ya sababu nyingi ya mashirika ya ndege kuanguka. Unajitanua au kuanzisha njia ambazo huwezi kuzihudumia kwa wakati wote (sustainably). Natumaini Mdhibiti (TCAA) watawashauri vyema kabla ya kujiingiza kwenye route. Ndiyo maana kuna kanuni ambayo inaonyesha kuwa ikiwa huduma unazozitoa kwa safari zinahitaji ndege 2 wanatakiwa wawe na ndege 3 kutoa huduma hiyo kwa uendelevu (yaani mara 1.5).
Natumai pia kuwa kuanzisha njia na safari za Marekani, ATCL watafanya uchambuzi yakinifu kwa makini kwani sidhani kama safari hizo zitakuwa za faida. Lakini hata hivyo siyo rahisi kama inavyoelezwa ili ATCL waweze ruhusiwa kuingia katika soko la Marekani. Ni mchakato mrefu ambao unahusisha uwezo wa nchi kusimamia usalama wa usafiri wa anga (kwa mujibu wa viwango vyao vinavyosimamiwa na FAA). Ni juzi tu Kenya wamepitishwa baada ya mchakato wa muda mrefu ulioanza karibu miaka kumi iliyopita.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Zito mwenyewe bombadia kabla hazijaanza kutumia alikuwa anaziponda kwel, lakini kwa sasa kila leo anazipanda.....tena hadi lift anagongea!