Zitto Kabwe: Taifa lina nyufa

Zitto Kabwe: Taifa lina nyufa

Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
547
Reaction score
183
Akiwa mtu wa mwisho kuchangia katika hotuba ya wizara/mambo ya ndani bwana Zitto Kabwe alisema watanzania wanaishi kwa umoja na wanashirikiana katika kila jambo kwani wanashirikiana katika mambo mengi na wanaochochea udini ni viongozi hasa wanasiasa kwani mtu huzungumzia udini katika majukwaa ya siasa huku watu elfu tano wakiwa mbele yao na kama ilivo bungeni mtu anazungumzia suala la udini na anaona fahari kwa manufaa yake binafsi.

Akaongeza kuwa, serikali haipo tayari kuchukua hatua kwa yoyote anayesemwa anatumia udini kwa manufaa yake...huku wakiwa na uwezo huo.Pia akaiasa serikali kuchukua hatua sasa badala ya matamko tuu.

Kweli hili ni la kweli kabisa.
#NYUFA
TAIFA LINA NYUFA

NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998. Alisema:

"Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanias"

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni "irresponsible" vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU KABWE Z. ZITTO

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-"point fingers" kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-"expose" , tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa "Agent Provacateur", watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni "very irresponsible" tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia "grievances" zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka na bomu. Turuhusu "honest discussions" miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na kauli za chuki "hate speeches". Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na "hate speeches" nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante
 
Hatua ilikuwa ni kuifungia radio iman kifungo cha milele na sio miezi kadhaa tu, dhambi yao haivumiliki lakini kwa uislamu wa zitto hawezi kutamka hilo
 
udini ulianzia pale yule mtoto mdogo alipokojolea msahafu bila kujua analofanya lina madhara gani-- reaction iliyotokea pale kwa waumini na shuluhisho la viongozi wetu; udini ukakua kuhusu sakata la uchinjaji kitoweo abapo mchungaji mmoja akapoteza maisha on the process suruhisho lililotolewa pale na viongozi wetu ndiyo tatizo. tusitafute mchawi, nyumba ikiteteleka basi lawama zote lazima ziende kwa wazazi hasa baba mwenye nyumba.
 
Akiwa mtu wa mwisho kuchangia katika hotuba ya wizara/mambo ya ndani bwana Zitto Kabwe alisema watanzania wanaishi kwa umoja na wanashirikiana katika kila jambo kwani wanashirikiana katika mambo mengi na wanaochochea udini ni viongozi hasa wanasiasa kwani mtu huzungumzia udini katika majukwaa ya siasa huku watu elfu tano wakiwa mbele yao na kama ilivo bungeni mtu anazungumzia suala la udini na anaona fahari kwa manufaa yake binafsi.Akaongeza kuwa, serikali haipo tayari kuchukua hatua kwa yoyote anayesemwa anatumia udini kwa manufaa yake...huku wakiwa na uwezo huo.Pia akaiasa serikali kuchukua hatua sasa badala ya matamko tuu.

Kweli hili ni la kweli kabisa.

UKIJARIBU KUANGALIA HEKIMA iliyopo katika mchango wa ZZK jana bungeni!! unaweza usifikirie kama anatoka katika chama kilekile na mbumbumbu GODBLESS LEMA... kaongea ukweli mchungu,ambao hakuna aliye na uwezo wa kuusimamia wala kuuongea. katoa lawama kwa kila anayestahili na hata yeye amukuwa tayari kubeba lawama kwa nafasi yake.. na kwa sababu ni watz wachache walio na uzalendo na ukweli kama ZZK, basi tutarajie matusi na kejeli juu yake bila uchambuzi wa mantiki toka kwa wachangiaji.
this guyzzk is presidential material no wonder hata adui zake wanamkubali
 
Zito kasema ukweli kwa mfano huyu mwenyekiti wa wazazi wa CCM taifa amekuwa anatoa matamshi ya hatari sana jukwaani kuhusu CDM kuwa ni chama cha kikabila na cha kidini, mimi binafsi kama mwana CCM sikubaliani na viongozi wa hulka za hatari kama hawa kwani ndizo zinazoleta chuki na kujenga matabaka ndani ya nchi yetu. Nawasihi viongozi wa kisiasa waache tabia na kauli zinazochochea chuki kwa watanzania bila sababu. Na tuwakatae viongozi wa sampuli hii.
 
Ndoa ya BAKWATA NA SERIKALI IVUNJWE ILI WAISLAM TUUNDE CHOMBO CHETU HURU AMBACHO KITAKUWA NA BARAKA KUTOKA KWA WAISLAM WOTE KULIKO HII BAKWATA AMBAYO NI KAMA TAASISI YA CCM. Kwahl nampongeza Zitto.
 
Hatua ilikuwa ni kuifungia radio iman kifungo cha milele na sio miezi kadhaa tu, dhambi yao haivumiliki lakini kwa uislamu wa zitto hawezi kutamka hilo

Ndio maana dhambi ya udini itaendelea kuitafuna nchi hii.Mbona humsemi Mh.Mkosamali ambae nae aliongea kama Mh.Zito?Kwa kua Mkristu mwenzio sio.Au ndo yale yale .....Mfumo Kristu.Kwamba Ukristu kwanza Tanzania baadae.Ww na Nivea lenu moja,na mpo wengi humu.Mnalishwa maneno,mnafikirishwa.Ama kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Tenda haki ndugu yangu na ufanye Uadilifu."Jitieni nira yangu,MJIFUNZE kwangu kwa maana mm ni MNYENYEKEVU wa moyo......".Haya unayosema bila ushahidi unajifunza kwa nani?
 
UKIJARIBU KUANGALIA HEKIMA iliyopo katika mchango wa ZZK jana bungeni!! unaweza usifikirie kama anatoka katika chama kilekile na mbumbumbu GODBLESS LEMA... kaongea ukweli mchungu,ambao hakuna aliye na uwezo wa kuusimamia wala kuuongea. katoa lawama kwa kila anayestahili na hata yeye amukuwa tayari kubeba lawama kwa nafasi yake.. na kwa sababu ni watz wachache walio na uzalendo na ukweli kama ZZK, basi tutarajie matusi na kejeli juu yake bila uchambuzi wa mantiki toka kwa wachangiaji.
this guyzzk is presidential material no wonder hata adui zake wanamkubali

Kuna tofauti kubwa kati yao.
 
"dini zipo lakini udini haupo"
"makabila yapo lakini ukabila haupo"

hizi ni baadhi ya kauli zinazotolewa na watu katika kujiridhisha kana kwamba fikra za binadamu hazikui bali zinabakia kama zilivyokuwa sijui miaka 50 iliyopita ambapo tukikubaliana hivyo basi tutakuwa watu wa ajabu. Humanity is growing!
Hali halisi iliyopo sasa inadhihirisha kuwa ukabila, udini, upendeleo nk vinaanza kujitokeza ...ina maana ni kama mbegu zilizokuwa hazijamwagiwa maji na sasa zimepata 'unyevunyevu' na zinaanza kuchipua na kukaa kimya au kutoyaongelea haya haina maana ndio yanaisha!
Katiba ya nchi, za vyama vya siasa na taasisi nyingine hakuna zinapoonyesha kuwa haya mambo yawepo lakini yapo. Kwa maana hiyo kuyashinda sio kutoyaongelea bali kusimamia misingi ya uwepo wetu kama taifa (katiba) na kuwa strict kwa atakayeivunja.
Kwa maana kama sheria zisipofanya kazi ni wazi masheikh watayaongelea misikitini, maaskofu watayaongelea makanisani, wanasiasa watayaongelea majukwaani, wafanyabiashara watayaongelea kwenye biashara zao nk. Suala ni kuyaongelea kwa msimamo na misingi ipi kwa maana hata hapo Mh. anaongelea hilo hilo na tunamsikia.
'busara' za kukaa kimya zitapelekea hata wale wenye nia nzuri ya kulinusuru taifa wasijue kinachoendelea au wasipate pa kutolea ushauri wao.
 
CHADEMA inanufaika na mgawanyiko wa kidini ndio maana wanashadidia!

Subili uchaguzi ukifika uone madhara ya kuingia kwenye uchaguzi ukiwa na mgogoro na jamii fulani, 2005 CUF walikua na kashfa kama hiyo CCM waliposimamisha muilsam mambo yalikua magumu kwa CUF. Kama CDM hawajaanza kuangalia hili suala kwa undani subiri 2015 CCM wasimamishe mgombea wao uje uone mambo yatakavyokua.
 
Hatua ilikuwa ni kuifungia radio iman kifungo cha milele na sio miezi kadhaa tu, dhambi yao haivumiliki lakini kwa uislamu wa zitto hawezi kutamka hilo

Redio imani imeanzishwa lini na kelele za waislam kunyanyaswa, kubaguliwa na kukandamizwa kumeanza lini? Toa mfano wa uchochezi au uzushi wake usikurupuke
 
UKIJARIBU KUANGALIA HEKIMA iliyopo katika mchango wa ZZK jana bungeni!! unaweza usifikirie kama anatoka katika chama kilekile na mbumbumbu GODBLESS LEMA... kaongea ukweli mchungu,ambao hakuna aliye na uwezo wa kuusimamia wala kuuongea. katoa lawama kwa kila anayestahili na hata yeye amukuwa tayari kubeba lawama kwa nafasi yake.. na kwa sababu ni watz wachache walio na uzalendo na ukweli kama ZZK, basi tutarajie matusi na kejeli juu yake bila uchambuzi wa mantiki toka kwa wachangiaji.
this guyzzk is presidential material no wonder hata adui zake wanamkubali

Uko sahihi pamoja na ZZK, ni ukumbusho kwa wenye akili tu
 
Hata nukuu mnaiba za biblia! Hivi kitabu chenu kina shida gani hata hamkitumii? Ndio maana watoto wenu wanawapa watoto wetu wakikojolee, sababu ni kwamba mmekalia kutumia biblia kukashifu ukristu kisha hapa unataka kunukuu kutafuta amani! Huyo Nivea wala mi simjui, ninamjua Yesu aliyenikomboa na kunifanya nisiwe mnafiki. Nimemsema Zitto kwa sababu ni muislamu na awaambie waislamu wenzake. Mkosamali akiwasema si mtampiga mawe. Makafiri wakubwa nyie!
jf siku hizi ni kama BUNGE la TANZANIA watu mizigo ni wengi sana by Ndygai
CC: maranduhussein
 
Kwa hiyo mmeona mnapiga kelele na hakuna anayewasikiliza upuuzi wenu so mmeamua kuua mapadri, kuchoma makanisa na kumwinda balozi wa papa! du! Uislamu na ugaidi ni chanda na pete

Unakumbuka mauaji ya Mwembechai waliuawa viongozi wangapi wa kiislamu? Unakumbuka misikiti imewahi chomwa Tunduru? Unakumbuka Qur'ani imechanwa na kukojolewa mara ngapi? Unakumbuka waislamu Zanzibar 2001 waliuwawa wangapi na Mkiristo mwenzenu? Yatosha kwa leo. Inabidi kila mmoja aangalie matukio haya kama mtanzania na si kama muislamu ama mkiristo.
 
udini ulianzia pale yule mtoto mdogo alipokojolea msahafu bila kujua analofanya lina madhara gani-- reaction iliyotokea pale kwa waumini na shuluhisho la viongozi wetu; udini ukakua kuhusu sakata la uchinjaji kitoweo abapo mchungaji mmoja akapoteza maisha on the process suruhisho lililotolewa pale na viongozi wetu ndiyo tatizo. tusitafute mchawi, nyumba ikiteteleka basi lawama zote lazima ziende kwa wazazi hasa baba mwenye nyumba.

Hayo yalikuwa matokeo ya udini uliokuwa unajengeka kimya kimya ndani ya jamii. Siku zote tusilaumu tulipoangukia,mtulaumu tulipojikwaa ili kisiki tulichojikwaa tuking'oe
 
baadhi ya makada wa ccm ambao ni wabunge na mawaziri hawapo tayari kukemea mtu yoyote wa chanma chao anapotoa kauli za udini au kukiuka maadili, husubiri mtu kutoka upande wa kushoto aongee ndipo uone wanatoa kauli za kusema na kulaani alichosema mtu wa upande wa kushoto, mfano nchimbi anapomzungumzia mh.lema kule arusha wakati wengi wa chama chake huongea mara nyingi majukwaani na hawamkosoi.....!
 
Ukweli huwa ni mgumu sana kukubalika, lakini time will tell!
 
Unakumbuka mauaji ya Mwembechai waliuawa viongozi wangapi wa kiislamu? Unakumbuka misikiti imewahi chomwa Tunduru? Unakumbuka Qur'ani imechanwa na kukojolewa mara ngapi? Unakumbuka waislamu Zanzibar 2001 waliuwawa wangapi na Mkiristo mwenzenu? Yatosha kwa leo. Inabidi kila mmoja aangalie matukio haya kama mtanzania na si kama muislamu ama mkiristo.

Mauaji ya mwembechai na Zanzibar ni waislamu dhidi ya nguvu za dola. hakuna kanisa limewahi kutuma waumini wake kwenda kuua waislamu. Hili limetokea kwa waislamu tu, kuwatuma waumini wake kwenda kuua padri, na kumwinda balozi wa papa! Na hata quran inapokojolewa, huwa mnaitoa wenyewe mkidai mkojoleaji atageuka kuku! Sasa vitoto vya kikristu ni vijiniasi na huwa vinawaaibisha na uongo wenu maana kama ingekuwa kweli vingeshageuka mijusi
 
udini ulianzia pale yule mtoto mdogo alipokojolea msahafu bila kujua analofanya lina madhara gani-- reaction iliyotokea pale kwa waumini na shuluhisho la viongozi wetu; udini ukakua kuhusu sakata la uchinjaji kitoweo abapo mchungaji mmoja akapoteza maisha on the process suruhisho lililotolewa pale na viongozi wetu ndiyo tatizo. tusitafute mchawi, nyumba ikiteteleka basi lawama zote lazima ziende kwa wazazi hasa baba mwenye nyumba.
Hasa baba dhaifu
 
Back
Top Bottom