Zitto Kabwe: Sitopoteza muda kuwajibu waliotunga email feki

Status
Not open for further replies.
Wacha ri muvi...rienderee...tuombe uzima tu kwasababu hizi ajali nazo zinatufyeka kama ebola...kitaeleweka tu...mchele upi...pumba zipi....
 
Kama ndio kwanza unasikia uwepo wa gazeti hilo inamaana wewe ni mbumbumbu na hujui mambo mengi hivyo ulipaswa kukaa kimya. Ina maana hujui pia kwamba chama hicho kipya kinajihusishba na mambo ya KAFARA?

Singo mpya hiyo, mmehama kwenye usalit mara ccm b mnatapata kama kuku, na bado mwaka huu mtazaa tu
 
halafu eri kubenea anashanda tuzo ya mwanadishi bora wa habari za kiuchunguzi wakati hata uzushi wa kwenye photoshop nao anaandika.
siku hizi haandiki tena issues,anaandika watu(character assassination).ama ni fedha za mbowe anahonga synovate.
 
Huwa hatuishi kulalamika kila siku tunaonewa , tunaonewa na chama tawala. Utasikia oooh CCM wezi, CCM mafisadi, CCM wao kwanza na tunalalamika kwelikweli ooh CCM wameharibu elimu yetu oooh CCM shaghalabaghala kila siku yaani haiwezi kupita siku hakuna malalamiko juu ya chama tawala chama alichokianzisha baba Wa taifa hili ambae twamuheshimu sana karibia watanzania wote.

TUNALALAMIKA TUNAHITAJI NINI?

Utasikia tunahitaji chama kingine hiki kimechoka kimeshindwa kutatua matatizo ya umma yaani ya wananchi na kimefanya maisha yamekuwa magumu sana. Ukiendelea kuuliza utaambiwa ni chama cha mafisadi kinatumia rasilimali kwa ajili ya wachache na wengi wamebaki na maisha magumu sana.
Utasikia chama hiki kina viongozi wengi wachumia tumbo, wafanyabiashara oooh utasikia chama sasa sio cha wafanyakazi na wakulima bali cha wafanyabiashara. Ukufika hapo usiendelee kuuliza utaambiwa mengi sana na watanzania hawa!
Kinachonifurahisha mimi na suala la zuri wanataka mabadiliko kupitia sanduku la kura na ukienda katika mitandao ya Simu hasa watsupp watu wameunda magroup ya majimbo wanaotoka na yakiwa na kauli mbiu kabisa wengine, KIBOVU HAKIPITI MWAKA HUU, WANANCHI KWANZA, TUNAHITAJI MABADILIKO ili mradi tu mambo yaende na yawe!

Pamoja na hari hiyo na kulalamika kote huko watanzania tumekuwa hatujui tunahitaji nini kutoka chama tawala na wala hatujui tufanye nini ili kupata tunachohitaji kutoka chama tawala.

KWANINI?

1: CHADEMA walikuja na kuwa chama cha matumaini sana tu na kutoa focus ya kuleta mabadiliko na watu walianza kuimba na kusema huu ni mpango Wa Mungu na CHADEMA kinakuja kukomboa Watanzania. Kilichotokea na kinachosikitisha sana ni pale Watanzania hawa badala ya kuungana kujua wanahitaji nini wafanyeje wamekuja na kauli ACT wazalendo chama kinachokuja kukomboa watanzania.
Hapa ndio msingi wa swali langu WATANZANIA TUNAJITAMBUA? tutaendelea kuimba hizi nyimbo mpka lini? Wengi hapa ni wasomi wanajua maana ya DIVIDE AND RULE na wengine ni maprofessor na walimu wazuri wamekubali dhana hii iendelee kutotufikisha tunapopahitaji.
Najiuliza tutaendelea kuwa katika kipindi cha mpito mpaka lini? Cha kusubiri kuondokana na huu tunaouhita uonevu, tunajua kama tunaonewa? Tumechagua njia sahihi ya sanduku la kura kipi kinachotugawa? kipi kinachotupofusha? Kwanini tumekubali kusalitiana na tunaanangaliana pasipo kuambiana ukweli? Kwanini kwa pamoja hatujaamua kuondokana na Yale tunayoyaona ni matatizo yanayoikwamisha nchi yetu.

Nasikitika sana kuona Mtanzania anaendelea kufikiria kipindi cha mpito tena wakati mwafaka umefika 2015 wakufanya maamuzi sahihi kwa Yale tunayo yalalamikia kama kweli yapo!
Kushindwa kuungana pamoja na kushindwa kujitambua kwetu ni kumaanisha hatusikii machungu ni kuendelea kusema kuwa ni sahihi chama tawala na serikali yake kilichofanya kuhusu Rasimu ya katiba, EPA, ESCROW, Buzwagi, Richmond, Elimu, madaraka yakupokezana, ajira na mengineyo.
Tusipofanya maamuzi ya kile tunacholalamikia wakati huu kwa upofu Wa kutoona ukweli kwa upofu Wa ushabiki Wa MTU mmoja au kwa manufaa ya MTU mmoja ni kutokujitambua.

Kama tumeamua Watanzania tuachane na vyama vipya tuungane kupitia muungano Wa UKAWA na vyama visivyotaka muungano huu tuviache kabisa vifanye siasa yao pamoja na CCM sisi tuamue kutumia sanduku la kura kufuta kile tunachokilalamikia miaka yote. Hizi porojo Rushwa ndogo ndogo na kuwa kipofu kwa ukweli uliopo ni matusi makubwa sana.

WATANZANIA TUJITAMBUE TUTAENDELEA KUWA KATIKA KIPINDI CHA MPITO MPAKA LINI?
 
Halafu eri KUBENEA anashanda tuzo ya mwanadishi bora wa habari za kiuchunguzi wakati hata uzushi wa kwenye photoshop nao anaandika.

Kama anauhakika ni photoshop, si aende mahakamani akalipwe fidia na tuone!! anaogopa nini? huko ndo kitajulikana..sio majukwaani kuwalisha ujinga kuficha ukibaraka kwa kujiita ujiiita uzalendo...unaafiki mtupu..kutaja mali bila kutaja wafadhili wa chama..unafiki mtupu..very soon all dark things, will be revealed
 
Halafu eri KUBENEA anashanda tuzo ya mwanadishi bora wa habari za kiuchunguzi wakati hata uzushi wa kwenye photoshop nao anaandika.

Kama ni Photoshop wahusika si wamkomeshe Kubenea kwa kumfikisha mahakamani? Mbona alipoambiwa anafukuzwa chama alikimbilia mahakama? Kwanza mnaokanusha ni nyie wapambe yeye kwenye kuujua ukweli anashangaa email wameipataje?
 
Kuna watu bado wana akili mgando,sasa Zito aache kufuatilia vitu vya maana hasa kipindi hiki cha uchaguzi wewe unasema kwann halipeleki gazeti mahakamani kama taarifa ya mawio ni ya uongo. Kumbuka magazeti yanatumiwa na watu na hili mawio linatafuta umaarufi take note.
 
Ha!nimekuja fasta ili nione kama kuna jipya kumbe ni habari toka kwenye gazet uchwara la saed kubenea.Nani asiyemjua kuwa ni mwanahabari wakipekee kwakukubali kuidhalilisha taaluma yake kwa kukubali kuhongwa na wahafidhina.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom