Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Nasoma nyaraka za Bajeti naona Serikali imepanga fedha kubadilisha mtambo wa IPTL kwenda kuwa wa Gesi. IPTL ni kampuni binafsi ambayo inamilikiwa kiutapeli na kampuni ya PAP kufuatia wizi wa fedha za akaunti ya TEGETA Escrow iliyokuwa Benki Kuu. Serikali inayopambana na ufisadi inawezaje kutoa fedha za umma kuwapa kampuni ya kifisadi?
Hawa PAP walikuja nchini na briefcase, wakachota fedha BOT wakahonga maafisa wa Serikali, Wabunge, Majaji, Mawaziri, Maafisa Usalama. Wakapewa mtambo bure. Wanalipwa kila mwezi tshs mabilioni ya capacity charges. Sasa wanafadhiliwa na Serikali kugeuza mtambo wao kuwa wa Gesi Asilia.
Rais analalamika kila siku nchi kuwa shamba la Bibi. Rais litazame hili la IPTL tafadhali. Kweli Serikali inatenga fedha kuifadhili kampuni hii? Maazimio ya Bunge yanasiginwa namna hii?... (from Zito Kabwe Facebook page).
Nijaribu kufikiri tu: Hivi wahujumu uchumi ni watumishi hewa tu!?, Mafisadi ni watumishi wa umma tu!? Wanaorudisha maendeleo ya nchi kwenye madini, hawa IPTL, gesi, makaa ya mawe, na hawa wanamitandao ya mawasiliano hawapo!? Wao ni wasafi!?
Mbona hawatumbuliwi!? Mbona wanapewa ruzuku wakati hata yeye alishawahi kusema hii kitu sio Afya kwa Taifa!? Mbona kama nao anapendelea!? Mbona kama wanyonge wanazidi kunyongwa!?
Hivi kweli haki yao watapewa!? any way, ngoja tusubiri tuone.