Zitto Kabwe: Serikali isikimbizane na wamachinga

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Kiongozi wa kudumu wa chama cha ACT Wazalendo na mbunge wa zamani wa Kigoma ameishauri serikali kuacha mara moja kukimbizana na wamachinga na badala yake wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi katika kushughulikia swala hilo.

Zito Kabwe amesema hamna mtu anayependa kuwa machinga na hamna mtu anayependa kufanya biashara kwenye jua huku akinyeshewa na mvua mbali ni maisha tu yanawafanya watu wawe hivyo kutokana na kukosekana kwa ajira kwa vijana nchini.

====

MwananchiHabari ZaidiKitaifa
Zitto ashauri namna ya kumaliza sintofahamu ya wamachinga
FRIDAY OCTOBER 22 2021

Dar es Salaam. Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema ubunifu zaidi unahitajika katika kumaliza suala la wamachinga ambao hivi sasa Serikali imeanza kuwahamisha kutoka maeneo yasiyoruhusiwa.

Septemba 13 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan aliwataka wakuu wa mikoa nchini kuwapanga wamachinga katika maeneo stahiki bila kusababisha vurugu. Amesema licha ya Serikali kutoa fursa kufanya biashara kama njia ya ajira kwao, wamekuwa wakifanya kazi katika maeno tofauti na wakati mwingine kuziba maduka ya watu.

Mchakato huo umeanza kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, ambako hivi sasa baadhi ya maeneo yaliyokuwa yanayotumiwa na wamachinga kufanya shughuli zao yamekuwa wazi baada ya kuondolewa kwa nyakati tofauti ambapo baadhi ya wamachinga wamekuwa wakilalamikia hatua hiyo.

Zitto ambaye ni mbunge wa zamani wa majimbo ya Kigoma Kaskazini na Mjini kwa nyakati tofauti, ameeleza hayo hivi karibuni wakati wa mahojiano yake na kituo kimoja cha redio kuhusu masuala mbalimbali ya siasa na mwenendo wa Serikali.

Katika maelezo yake Zitto, amesema suala la wamachinga linatokana na changamoto za shughuli za kiuchumi, akidai kuwa Taifa linazalisha vijana wengi kuliko uchumi wa kutengeneza ajira.

Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa sababu zinazosabisha vijana kuingia kwenye nguvu kazi, lakini hakuna ajira.

“Wanaamua kujiajiri wenyewe katika shughuli za umachinga, ni wajibu wa Serikali kutengeneza mazingira mazuri ili wafanyabishara kufanya shughuli zao bila bughuza.Nimesikia Kariakoo juzi watu wameondolewa na kuna malalamiko ya kwamba baadhi yao walikuwa wanapanga hadi kwenye njia za waenda kwa miguu.

“Ndio maana wanatakiwa kujenga mazuri ili wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao kwa ufanisi, nilipokuwa mbunge wa Kigoma kulikuwa na changamoto ya kina mama wa kata ya Mwanga kufanya biashara ya samaki barabarani nyakati za jioni. Lakini walikumbana na changamoto ya kufukuzwa,” amesema Zitto.

Amesema kutokana changamoto hiyo, baraza la madiwani la Kigoma Ujiji likatafuta suluhisho la kutenga mtaa mmoja unaofungwa kila siku kwa ajili ya kutoa fursa ya kina mama hao kufanya shughuli zaio kwa ufanisi ili kujiingizia kipato.

“Ni suala linalohitaji ubunifu zaidi badala ya kukimbizana na wamachinga, Serikali inatakiwa kukaa pamoja na wafanyabiashara hao sio viongozi wao pekee bali wenyewe ili kujadiliana nao na kuweka utaratibu bora wa kufanya shughuli zao,” amesema.

Katika mahojiano hayo, Zitto ameishauri Serikali masuala mbalimbali pia katika kumaliza sintofahamu ya wamachinga ikiwemo kuwekeza zaidi katika kilimo cha kisasa kitakachowavutia vijana na kupunguza wimbi la watu kutoka vijijini kuhamia mjini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo umachinga.

“Pia Serikali iimarishe viwanda vidogo vidogo ili kuleta ufanisi pamoja uwepo wa teknolojia itakayowavutia vijana wengi kukimbilia katika sekta hii,”amesema Zitto


Chanzo: Mwananchi
 
Kiongozi wa kudumu wa chama cha ACT Wazalendo na mbunge wa zamani wa Kigoma ameishauri serikali kuacha mara moja kukimbizana na wamachinga na badala yake wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi katika kushughulikia swala hilo.
Zito Kabwe amesema hamna mtu anayependa kuwa machinga na hamna mtu anayependa kufanya biashara kwenye jua huku akinyeshewa na mvua mbali ni maisha tu yanawafanya watu wawe hivyo kutokana na kukosekana kwa ajira kwa vijana nchini.

Zitto tuache kwanza tusafishe uchafu mijini, haya kayaongee nchini Zanzibar ambako wewe ni sehemu ya sirikali.
 
Zitto tuache kwanza tusafishe uchafu mijini, haya kayaongee nchini Zanzibar ambako wewe ni sehemu ya sirikali.
Kama umeshindwa kusafisafisha machangudoa utaweza machinga?
Ulikuwa na umri gani enzi za Kikwete?
 
Maghufuli aliharbu Sana kuwatia watu hofu , machinga hawakuwa hv mwaka 2014 ulikuwa huwagusi kizembe , but soon things will turn around ..wacha tuone
 
Machinga waondolewe kisheria na sheria zipo wazi kabisa kwenye hili hakuna anayeonewa, labda Kama jiji wanatumia Kama kichaka Cha kupora Mali hili ndio tulikemee!!

Wapewe maeneo ya masoko ya kudumu milele na milele.

Mkiendelea kuwapeti peti Kuna siku mtawakuta kwenye jengo la bunge na kwenye kambi za Jeshi wamepanga Nyanyachungu.

Wakimbizane na nani? Wakati waliua upinzani 2020 machinga wakikenua meno eti acha wale joto la jiwe 😄😄😄😄
 
Mm ni machinga lkn zoezi hili naliunga mkono. Kama machinga wangeendelea kuachwa wazagae kama ilivyokuwa baada ya miaka 5 kuanzia sasa barabara zote za lami zisingepitika kwa magari.

Tuishi kwa mipangilio
 
Huyu mnafiki mzito alipokuwa mwenyekiti PAC hakuna alichofanya zaidi yakuhongwa fedha, magari nk. na kujidai hajui wizi na machafu yaliyoendelea.

Nimtu wa hivihivi na hovyohovyo kuliko watu wanavyodhani! Huwa anapiga domo ili apewe position za juu lakini Ku compromise na mafisadi ni dakika.

Marafiki zake walikuwa kina lowassa,mkono nk. yaani matajiri wenye fedha zamashaka!!!
 
Machinga waondolewe kisheria na sheria zipo wazi kabisa kwenye hili hakuna anayeonewa, labda Kama jiji wanatumia Kama kichaka Cha kupora Mali hili ndio tulikemee!!

Wapewe maeneo ya masoko ya kudumu milele na milele.

Mkiendelea kuwapeti peti Kuna siku mtawakuta kwenye jengo la bunge na kwenye kambi za Jeshi wamepanga Nyanyachungu.

Zitto aache siasa uchwara hizi zimeshapitwa na wakati
Njaa haina baunsa, siku ikiwafika usalama wa Makalla utakuwa mashakani
 
Hatua ya kwanza kuwaondoa, hatua ya pili waoneshwe maeneo mapya ya kufanyia biashara zao, ya tatu wapangiwe namna nzuri ya kulipa kodi waje kuboreshewa na maeneo yao ya biashara, tusikariri maisha hakuna haja kurudi nyuma, riziki ya mtu hupangwa na Mungu, sio mwanadamu.
 
Back
Top Bottom