Zitto Kabwe: Rais wanaokusifia tu hawakusaidii

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Zitto Kabwe aliweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema anashukuru kuona Rais Magufuli anawasikiliza PIA watu ambao wanamkosoa kwa malengo mazuri kwani wana nia njema na wanatumia uzalendo wao wa hali ya juu kukosoa.

"Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi" Aliandika Zitto Kabwe.

Siku za karibuni Zitto Kabwe aliandika Makala ya mambo kumi ambayo Rais Magufuli hajafanya ndani ya siku 100 na katika makala yake, jambo la nne alizungumzia suala la uingizwaji wa sukari kutoka nje na kusema ni jipu ambalo limeiva na linatakiwa kutumbuliwa.

"Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na serikali haina mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika mpango wa maendeleo serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa sukari ni jipu" Zitto Kabwe

Lakini Rais Magufuli ni kama amesikia kilio cha Mh Zitto Kabwe kwani tayari ametangaza kufutwa kwa vibali vya uingizwaji wa sukari nchini, jambo ambalo Mh Zitto amemshukuru Rais kwa kuliona na kulifanyia kazi na kumuomba pia aliangalie suala la IPTL/PAP nalo bila kulionea kigugumizi chochote.

"Rais Magufuli nakupongeza kwa kuona tusemayo wapinzani wa chama chako. Umetekeleza jambo 1/10 niliyoeleza kuwa hujafanya. Naomba utekeleze na hayo mengine kwa manufaa ya nchi yetu. Hili la IPTL/PAP mbona unalipatia kigugumizi ndugu Rais?

Umetoa agizo kuhusu hili. Shukrani sana" Aliandika Zitto Kabwe.
 
Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi
Kwa hiyo sasa hivi anatekeleza sera za ACT?
 
Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi
Ndo hawa hawa wakitumbuliwa watamgeuka
 
Tatizo ni pale Zito anaposema rais hajafanya lolote ila ameboresha yailyokuwepo. Hivi Zito haoni hii nayo ni credit maana muda bado ni.mfupi tangu achukue nchi. Lazima aanze na yaliyolala kabla ya kushughulikia mapya. Hata hivyo sisemi Magufuli hawezi kukosea ila tunapotaka kukosoa tusiwe biased. Tuseme mazuri alofanya na wapi anatakiwa ku-improve. Haileti maana mtu kuongea kama vile raisi hajafanya lolote.
 
Huyu huwa simwelewagi! Ni kama kinyonga kubadilika badilika.Leo atasifia kesho ataponda!
 
At least ukipita mwaka hatujaona hata kamradi kamoja kamesimama ndo tutapata cha kuongea,now we just watch.....
 
Wajinga wachache wanasahau kama uafadhali huu unaoonekana ni kutokana na ukosoaji wa wapinzani
 
Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi
Nakushukuru Zito kabwe kwa kuanzisha uzi huu! binafsi nilishauweka facebook ila response yake ilikuwa ni kukosolewa na kutukanwa kumbe mimi ndiyo mwenye mapenzi mema na inchi kuliko hao wanaomsifia tu kwa kila jambo. Tatizo letu Tanzania hatuna ajenda ya kitaifa kila jambo limeegemea kwenye mitazamo ya kiitikadi za vyama vyetu matokeo yake hata lingekuwa jema ilimradi linamhusu mtu wa CCM au UKAWA litaonekana si jema hapo ndiyo tatizo lilipo, lakini ingefika wakati tukaachana na itikadi zetu tukaweka utaifa wetu mbele mtu hawezi ona shida kukosolewa kwani hata rais ni binadamu siyo malaika
 
Ukweli lazima usemwe kutokana na maoni ya mtu mmoja mmoja yule anaeona Rais kafanya kitu na kikamgusa wacha amsifie Rais na yule anaona bado Rais hajafanya ipasavyo na yeye aseme na kushauri yale anayodhani yangepaswa kufanywa...Si lazima wote tusifie na si lazima wote tuponde...Binafsi naona Rais anajitahidi sana kugusa matatizo yaliyokuwa yakiwagusa wananchi mfano huduma za afya ameondoa urasimu uliokuwepo mfano muhimbili na hata upatikanaj wa madawa, kuongeza wodi za kulala kina mama wajawazito, na hii amaeanzia Dar nikiamini na mikoa mingine itafuata
 
Rais Wanaokusifia tu hawakusaidii. Umefanya vema kusikiliza tunaokukosoa. Tuna nia njema na tunatimiza uzalendo wa hali ya juu ambao ni kukosoa. Hatusemi wasikusifie, hapana. Wawe na kiasi
cc All members of JF. Hii inawahusu sana baadhi ya watu humu.
 
Kulikuwa na haja ya kusema haya? Inajulikana kuwa upinzani wanakosoa, nani hajui? Wewe kosoa kumjenga na sisi tutasifia kumpa moyo. Wtf!
 
Mimi naamini hata wanaokosoa nao wawe na kiasi. Sidhani kama watu watafanya mashindano ya nani anakosoa zaidi na nani anasifia zaidi.

Kiasi unakipimaje bwana mkubwa?
Hivi ni lini " Mzee" atatangaza mali zake, madeni yake na jinsi alivyovipata?

" Mzee" anatumbua wenzie tu ni nani basi atamtumbua yeye kuhusu nyumba alizoziuza kwa bei cheeee kwa ndugu zake na " kimche.....o"?
 
Bado hajafanya la maana katka elimu bure.Hatutaki muda wa majaribio...kwani alisema kwenye kampeni kuhusu elimu bure...kwa nini watendaji hawakuanza kujipanga..???kwani walikuwa hawajui mtu wao atakuwa Mh Rais au wana mipango ya kumuhujumu...????Ukweli ubakie ukweli...kuna wanafunzi wanakaa chini kwenye udongo.....HAKUNA MADAWATI.
 
Huyu huwa simwelewagi! Ni kama kinyonga kubadilika badilika.Leo atasifia kesho ataponda!

Hiyo ndio Siasa Safi! Hata Nyumbani kwako unaweza ukapatia leo ukakosolewa kesho!
Usikariri kukosoa mtu Siku zote au kupongeza mtu siku zote
 
Back
Top Bottom