Nakushukuru Zito kabwe kwa kuanzisha uzi huu! binafsi nilishauweka facebook ila response yake ilikuwa ni kukosolewa na kutukanwa kumbe mimi ndiyo mwenye mapenzi mema na inchi kuliko hao wanaomsifia tu kwa kila jambo. Tatizo letu Tanzania hatuna ajenda ya kitaifa kila jambo limeegemea kwenye mitazamo ya kiitikadi za vyama vyetu matokeo yake hata lingekuwa jema ilimradi linamhusu mtu wa CCM au UKAWA litaonekana si jema hapo ndiyo tatizo lilipo, lakini ingefika wakati tukaachana na itikadi zetu tukaweka utaifa wetu mbele mtu hawezi ona shida kukosolewa kwani hata rais ni binadamu siyo malaika