Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

mkimnyima nafasi ndani ya CDM ataenda NCCR -Mageuzi, ili kura zigawanyike na CCM waibuke na ushindi. Habari ndiyo hiyo.
 
khaa! jamani nafikir kama mtanzania yeyote yule mwenye akili timamu anaruhusiwa kugombea uraisi ila shida yangu kwa kijana zito ni bado wakati wako mkuu. subiri kwanza ukue kiakili Tanzanian siyo DARUSO mkuu ingekuwa hivyo hata RUGE na FLAVIANA wangegombea. unahitaj kukua kuonyesha uwajibikaji wako na kuwa na dhamira ya kweli ya kuongoza wala siyo kwenda ikulu kuangalia tausi tu na kuonyesha uchekibobu.

ndio maana wenzio wenye akili wanacheza kwa step sana tu.
 
asitudanganye hapa,alikua anataka kugombea 2015,alidhani wengi watamuunga mkonno na kumpongeza,baada ya kuona watu wengi wanampinga kaamua avunge kuwa hakuwa na nia ya kugombea 2015.Kasoma alama za nyakati.
 
Tunasafari ndefu kufikia ustawi na maendeleo ya kweli kwa sababu wana'sihasa' wetu si watu waaminifu na wakweli.
 
khaa! jamani nafikir kama mtanzania yeyote yule mwenye akili timamu anaruhusiwa kugombea uraisi ila shida yangu kwa kijana zito ni bado wakati wako mkuu. subiri kwanza ukue kiakili Tanzanian siyo DARUSO mkuu ingekuwa hivyo hata RUGE na FLAVIANA wangegombea. unahitaj kukua kuonyesha uwajibikaji wako na kuwa na dhamira ya kweli ya kuongoza wala siyo kwenda ikulu kuangalia tausi tu na kuonyesha uchekibobu.

ndio maana wenzio wenye akili wanacheza kwa step sana tu.


Huyu bwana uongo umemzidi kipimo, c juzi aliwaambia wasanii akiwa kigoma waje 2015 wamuimbie bure coz atakuwa na bajeti ndogo ya mil 200? leo hii anasema nn? Huyu jamani km alivyosema mwenzangu kuwa huko india kaweka kamasi badala ya ubongo, mtu mwenye ubongo kamilifu hawezi leo kusema hili na kesho anakana hilo hilo.

Pia anavyosema yy haamini ktk kuombwa au kutumwa na wananchi, hii ni kumchafua Dr slaa moja kwa moja kwa kuwa 2010 Kamati kuu ilimuomba agombee, huyu bwana ni wa kuwa nae makini sana
 
000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000

Hiyo iliyofanya hapa, has no credibility, you are not even 0.000001% of the CDM voters, kwa hivyo you dont play any role in the decision making, please let the true system do its work. Zitto is the only light at the end of the tunnel for CDM. Dr.SLA n Mbowe are the down fall for CDM.
Zitto kakutuma?
 
la yeye kuwa na dhamira ya kuwa Rais liko waazi
kila mtu analiona bila hata yeye kulitangaza
kama alikuwa hana uhakika na mwaka gani
basi asingetangaza now...

Anazidi kutuonyesha tu asivyo uhakika. Karibu kila mtoto at some point anakuwa na ndoto za kuwa rais.
 
Hivi huyu Zitto bado anadhani atapata nafasi ya kukoroma kwa wa TZ? He is down the slope.

Naona anahangaika kuingiza mambo ya urais ili ionekane anachukiwa kwa hilo. Kwani Urais ndo ulikata umeme?

Kwake mimi nina mambo mawili tu. 1. nahisi alikula rushwa kwa muda mrefu, baada ya kuwa ameaminiwa na wa TZ kwa sababu ya hali ya kisiasa tuliyokuwa nayo kwamba CCM imeshakuwa kero. Sasa hivi haamini kama ana drop. Kumbuka hapa JF aliwahi kujitapa kwamba ame master parliamentary politics. Sasa master wetu ajuwe anaondoka.

2. Huyu jamaa kama hakula rushwa na huyo Januari wake basi wote hawafai. Ni dhaifu wasiokuwa na upeo wa kibinadamu. Hawawezi kuwa ktk nafasi zao kwa kipindi chote hicho halafu wasifahamu upuuzi wa Tanesco. Kwa maana nyingine hawakustahili kuwa viongozi wa kamati hizo na tukiendelea hawafai kuwa wabunge na yeye anayelilia urais, apotelee mbali!

Muhongo anaingia miezi michache anapata taarifa hizo za ufisadi, lakini yeye alikuwepo kwa miaka hiyo yote bila kufahamu kinachofanyika? au alikuwa bize akisoma vitabu kutafuta theories za uchumi kama Mwigulu Nchemba?

Sasa eti anarudia utetezi wa nyimbo za wasanii. Haya aliyojadiliana na Januari. Sawa lakini hayo ndo yatufanye tusahau ufisadi wake?
 
Licha ya kuonesha uwezo katika maeneo kadhaa, watu wengi wana mashaka juu ya uadilifu wako, utashi, hekima, busara na mshikamano wako na viongozi wenzio na chama. Je katika matukio yafuatayo yaliyotia shaka juu ya uadilifu na dhamira yako, unayatolea maelezo gani:

1) Wakati wa kampeni za uchaguzi za 2010 wakati viongozi wenzio wa CHADEMA wakiwa wanahangaika kutafuta kura, wewe ulionekana maeneo kadhaa ukifanya mikutano ya siri na RA. Mikutano hiyo iliyokuwa na manufaa kwa chama, Taifa au kwako binafsi? Ilikuwa na faida kwa kiasi gani, na mlikuwa mkiongelea nini?

2) Wakati viongozi wenzio wa CHADEMA mwaka 2010 wakisulibiwa na jeshi la polisi na TISS, wewe ulithibitika wakati wote ukiwa na mawasiliano ya karibu na viongozi wa juu wa TISS. Mawasiliano yako ya daima na viongozi wa TISS, yalikuwa ni kwaajili ya manufaa ya Taifa, yako binafsi, wapiga kura wako au viongozi wenzako wa CHADEMA? Na kwa nini wewe pekee yako ndani ya CHADEMA, unaonekana kutopata misukosuko yoyote kutoka polisi? Nini uhusiano wako na TISS na viongozi wake?

3) Kwa nini mwaka 2010 uliamua kumpigia kampeni JK badala ya mgombea wa chama chako Dr. Slaa?

4) Kwa nini kila mara umeonekana kutaka madaraka ya kila nafasi inapopatikana?

5) Kwa kujitathmini mwenyewe unadhani ni nini mapungufu yako (ambayo ni lazima uyafanyie kazi) na nini nguvu zako? i.e. your strengths and weaknesses.

6) Kila mara umezungumzia nafasi ya vijana katika uongozi wa Taifa, je, unazungumzia vipi mchango wa ujana katika uongozi bora? Unazungumzia vipi utendaji mbovu wa mawaziri vijana walioteuliwa na JK katika serikali yake (ref. Ngeleja, Maige na Malima) hata kulazimika kuwateua wazee (ref. Prof. Muhongo & Mgimwa) ili kuokoa jahazi lililowashinda vijana? Je, ujana ni sifa inayoweza kuliokoa Taifa au zaidi ni moral satifaction kuliko faida tunayoweza kuipata?


Tukio la 6 hapo juu limenifurahisha sana, kwani dhana inayoanza kujengeka ya eti VIJANA, VIJANA VIJANA ni ya kibaguzi sana, hata hao wazee wangetubagua kiasi hii sidhani kama tungeweza.Zitto lazima abadili rythm ya neno vijana bora aseme watanzania
 
Zito Kabwe akiwa anajiamini kabisa amesema yeye sio mla rushwa, anaichukia rushwa haipendi na ni kati ya wabunge na viongozi wanaopiga vita rushwa kutoka rohoni/moyoni mwake.

Ameomba kila mwenye hisia, tuhuma au hata tetesi za ushahidi kuhusu rushwa kwake yeye aende kutoa utetezi wake na ushahidi wake kwenye tume zilizoundwa.

Zito amesema anashirikiana na chama kukijenga na kuhakikisha kinashika dola.

Zito amesema sio lazima yeye awe Raisi ila anaupenda na kuutaka uraisi na kama chama chake kitamkubalia kukupeperusha bendera atafurahi sana.

Vile vile kasema angefurahi umri wa kugombea uraisi kwenye katiba mpya ushushwe kutoka 40 mpaka 35 sio kwababu tu anataka kugombea kwani ni muafaka kwa Tanzania ya leo.

Vile vile amesema yeye hana mali kama watu wengi wanavyomhisi, anajenga nyumba kwao kigoma hana hummer wala range na anaishi maisha ya kawaida kabisa.

Ameonyesha kakomaa kisiasa na anamalengo, ikumbukwe kila binadamu anaudhaifu ila tupime (weakness and strength)

Ameonyesha kuwa CDM hakuna makundi.
Amekataa kuelezea mishahara na posho za mbunge amesema aulizwe Makinda hapa hata mimi sijui kwa nini mshahara sio siri isipokuwa TZ.

Kazi kubwa ya CDM sasa iwe ni kujenga chama na kuhimili kukua kwa chama.
 
Hio inajulikana akikua ataacha mambo ya kitoto na hii ni ishara ya kuanza kukua kiakili
 
Hizi habari nyingine bwana hatari tupu. Yaani mtu anajitungia tu maneno yake na kuyarusha JF. Na kwasababu JF imejaa watu wa kuchangia chochote hata kama kimetoka uvunguni, basi ndiyo hivyo tena watu wachangia tu uzi.
 
Kasema wapi na lini? maana humu sasa itaanza habari, chanzo hatukijui, mm huyu jamaa namkubali lkn akitokeza tena TUNTEMEKE mara Shose Genda huelewi nani ni nani ndo maana mm nakimbia hizi story sasa
 
Back
Top Bottom