Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani

Status
Not open for further replies.
kauli ya zito ni ya kinafiki, kwa sababu hata yeye ni mwanasiasa kama anajua hilo kwa nini aliingia katika siasa na kuendelea kukaa humo?

huwezi kuchukia kitu na huku unaendelea kukifanya na hali uwezo wa kutokukifanya bado upo.

na si kweli kuwa siasa ni chafu inategemea na wachezaji wa mchezo huo.
huku kwetu watu ni njaa tu zimewazidi. lakini huko nchi nyingine wanafanya siasa na mambo yanaonekana.
tatizo bongo ni njaa za wanaoifanya siasa na ujinga wa sisi wananchi.
 
Zitto kasema ukweli wa mambo sema nyie waumini wa viongozi mtaweweseka na matusi/kejeli zenu.

Ni utoto kukaa ukaamini kwamba hawa wanasiasa wanayoyasema wanamaanisha!! sehemu kubwa ni uongo na unafiki tu. wanawatumia ili wafike wanakotaka. Kumbukeni enzi za Mrema, Seif n.k. Wako wapi sasa??

Leo wanawafanya mnachukiana kivyama na kuuana/kuumizana wakati wao kesho na kesho-kutwa wakiona mambo hayaendi wahama vyama. CDM utakuta anarudi CCM n.k

Narudia tena ni utoto wa hali ya juu kudhani wanayosema wanasiasa (hata wapinzani) ni kweli. They just manipulate u!!!

Be alert!!

Kweli mkuu MJIMPYA hajawahi kutokea mwanasiasa mkweli Hasa hasa Tanzania hii wanasiasa wote ni wale wale na Lengo kubwa la wanasiasa ni kushika dola kwa namna yoyote ile iwe kwa uovu au kwa wema hapa namaanisha wanasiasa wote chama tawala na upinzani pia
 
Last edited by a moderator:
Kauli ya kutokuwaamini wanasiasa haiwezi kutufanya tusiwaamini wanasiasa na hili ndo kosa tunafanya tunawapa wasioaminika kwa virushwa na kanga na chunvi, wakati wanabeba dhamana ya Nchi yetu na hatima yetu. Wanasiasa muwe waaminifu kauli ya zito naikataa.
 
Zitto Zuberi Kabwe ni mutu ya TISS hata Chadema wenzake wanajua, alitaka kuwavuruga CHADEMA akiwatumia mamluki wenzake akina Mwampamba na Shonza ikashindikana! habari ndio hiyo na ukweli ndio huo!!!!!!!!
 
kweli zitto yuko sahihi kabisa, kila mwanadamu ana mapungufu yake hivyo hakuna anayestahili kuaminiwa isipokua unapaswa ujiamini wewe mwenyewe na Mungu basi!,

Mbona me sioni kama alichokisema zitto ni kitu cha ajabu?, au kwa sababu ni zitto!!

Tanzania tuna issue nyingi za msingi za kujadili, me nadhani tuondokane na huu utamaduni wa kujadili watu na tujikite kwenye kwenye kujadili issues!
 
Huo ndio ukweli wenyewe wanasiasa sio watu wa kuwaamini hata atoke chama gani.

Mlipenda hivyo hivyo msipende hivyo hivyo
 
Zitto kasema ukweli wa mambo sema nyie waumini wa viongozi mtaweweseka na matusi/kejeli zenu.

Ni utoto kukaa ukaamini kwamba hawa wanasiasa wanayoyasema wanamaanisha!! sehemu kubwa ni uongo na unafiki tu. wanawatumia ili wafike wanakotaka. Kumbukeni enzi za Mrema, Seif n.k. Wako wapi sasa??

Leo wanawafanya mnachukiana kivyama na kuuana/kuumizana wakati wao kesho na kesho-kutwa wakiona mambo hayaendi wahama vyama. CDM utakuta anarudi CCM n.k

Narudia tena ni utoto wa hali ya juu kudhani wanayosema wanasiasa (hata wapinzani) ni kweli. They just manipulate u!!!

Be alert!!

Your very right my dear! ZZK is very right too. Hata hao kina slaa sio wakuwaamini 100%. Yuko wapi Amani Kaburu wa kigoma mjini. watu walimuabudu kama Mungu wa CDM. Alikihama chama watu wakapagawa. leo hii ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa Kigoma anakula kuku kwa mrija. Kuweni makini na wanasiasa wanatuhadaha tu. lao moja tu! kupata madaraka!!!!!!!!!. Ukiwa mfuasi kupita kiasi unakua mjinga na maneno ya msingi kama ya ZZK huwzi kuyatafakari!!!!!
 
"Siasa ni mchezo mchafu,unaotaka umaarufu,wanasiasa wengi wa bongo waongo ........." Aliimbaga sugu,kisha na yeye leo ameingia kwenye siasa.kwa kifupi mimi binafsi huwa simuamini mtu,namuamini MUNGU tu,ila kuna baadhi ya wanasiasa huwa nawakubali pale wanapotekeleza mambo yao kwa vitendo,binadamu wengi tupo kama vinyonga hatukawii kubadilika.Mwisho kabisa namunga mkono Mh Zitto.
 
unanilazisha nimwamini mtu anaeuwa watu ili apate wafadhili.zito kesha liona
siwezi kumuamini mwanasiasa.
 
"Siasa ni mchezo mchafu,unaotaka umaarufu,wanasiasa wengi wa bongo waongo ........." Aliimbaga sugu,kisha na yeye leo ameingia kwenye siasa.kwa kifupi mimi binafsi huwa simuamini mtu,namuamini MUNGU tu,ila kuna baadhi ya wanasiasa huwa nawakubali pale wanapotekeleza mambo yao kwa vitendo,binadamu wengi tupo kama vinyonga hatukawii kubadilika.Mwisho kabisa namunga mkono Mh Zitto.

umenikumbusha hio nyimbo. vilevile nakubaliana nawewe hapo chini.
 
Watanzania tayari hatujiamini,tena mtu mwingine anatuingizia maradhi ambayo tayari yapo:kutoaminiana!Mwingine mahali fulani alisema viongozi wa dini tusiwaamini,hata tusipowaamini wanasiasa bado ndo hao watawala,maana ni kama maji usipoyaoga utayanywa,sasa nini kifanyike?tushike mtutu tuwaondoe ama tuwasuse wafanye mambo yao watakavyo?Zitto pia ni mwanasiasa,tukwaminije kwa hiyo kauli?Yawezekana unaisema kwa vile wewe huaminiki na hivyo kuwafanya watanzania waamini kuwa hiyo ndiyo hali ya kawaida tu kwa wanasiasa?Tafadhali elimu yako isitumike kuwatia wananchi roho ya kutowaamini viongozi wao.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom