Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani

Status
Not open for further replies.

rpg

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
3,620
1,476
Kauli hii ameitoa leo katika kongamano la ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii ambapo yeye alikuwa akiongelea majukumu ya bunge katika kusimamia uwajibikaji.

Mambo mengi aliyoongea yalikuwa ni yenye mwelekeo chanya isipokuwa hili la kutupa tahadhari ya kutowaamini wanasiasa, akisisitiza hata wa upinzani.

Nyuma ya kauli hii kumejificha nadharia nyingi kutegemea na mtu atakavyoipokea.

Kwa maana nyingine, kauli hii inaleta hisia kwamba, hata wale wa chama chake tusiwaamini pia.

Kwa kuwa mheshimiwa ni miongoni mwa members hapa, najua ujumbe huu utamfikia. Nilitaka atoe ufafanuzi alikuwa anamaanisha nini kwa kauli yake hii.
 
Ukweli unauma hasa ukijijuwa kuwa una maliza nguvu zako kuamini kitu si cha kuaminika! Mhe Zitto huna haja ya kufafanuwa kwani nani hapa hajaguswa na uongo na uzandiki wa wana siasa? Halafu nani kasema kwenye mchezo mmoja timu pinzani zikacheza mipira miwili tofauti. Wanasiasa wote lao moja na ungewafuatilia kwenye hizo kamati wanapofanya madudu yao kwa umoja wao.
 
Zitto huwa simuamini na haaminiki kutokana na matendo/maneno yake kuonyesha km mtu fulani kigeugeu, lkn hili la kusema tusiwaamini sana wanasiasa naona kama lina ukweli fulani.tuache unafiki.
 
Doubt,doubt everthing arround you,doubt on everybody!!!!
Doubt on your own doubts!!!!!!

Ndo falsafa behind being precautious!!!!!

Yaaani anasema kaeni chonjo mkionacho sicho!!!!
 
Hata hii kauli yake ya kuasa kutokuwaamini wanasiasa mimi Siiami kwa kuwa naye ni Mwana Siasa
 
Zito ni gambaz so hata yeye si wakumuamini kabisa na pia ni mnafki kabisa.
 
Zitto kasema ukweli wa mambo sema nyie waumini wa viongozi mtaweweseka na matusi/kejeli zenu.

Ni utoto kukaa ukaamini kwamba hawa wanasiasa wanayoyasema wanamaanisha!! sehemu kubwa ni uongo na unafiki tu. wanawatumia ili wafike wanakotaka. Kumbukeni enzi za Mrema, Seif n.k. Wako wapi sasa??

Leo wanawafanya mnachukiana kivyama na kuuana/kuumizana wakati wao kesho na kesho-kutwa wakiona mambo hayaendi wahama vyama. CDM utakuta anarudi CCM n.k

Narudia tena ni utoto wa hali ya juu kudhani wanayosema wanasiasa (hata wapinzani) ni kweli. They just manipulate u!!!

Be alert!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom