Zitto Kabwe: Mkoa wa Kagera ni Mkoa Masikini Zaidi Tanzania

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
KUTOKA KAGERA

- 51% ya wakazi wake wanatumia chini ya TZS 1,644 kwa siku ( mstari wa umasikini Tanzania ni TZS 49,320 kwa Mwezi ).

- Pato la Wastani la Mtu wa Kagera ni TZS 1.2M kwa Mwaka. Mtu wa Ruvuma na Iringa ana Pato la Wastani mara 3 zaidi ya mtu wa Kagera.

- Mwaka 1994 Kagera ilishika nafasi ya 12 kati ya Mikoa 21 nchini kwa hali ya Uchumi, Mwaka 2022 inashika nafasi ya 26 kati ya Mikoa 26, yaani Ndio Mkoa masikini zaidi nchini.

Iweje Mkoa wa Kagera uwe masikini zaidi? Ni Mkoa wenye ardhi iliyopandwa kahawa kuliko Mkoa wowote nchini, ni Mkoa wenye utajiri mkubwa wa ardhi na hali ya hewa, ni Mkoa uliokaa kimkakati kijiografia ( unapakana na Nchi nyingi zaidi za Afrika Mashariki kuliko Mkoa mwengine wowote), una rasilimali madini kama Nickel na una wasomi wengi zaidi kuliko mikoa mingi ya Tanzania! Kwanini uwe Mkoa masikini zaidi?

Kuna sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

1. Uchumi wa mkoa huo unategemea sana kilimo ambacho kinategemea mvua. Hivyo, ukame au mvua zinazopungua zinaweza kusababisha upungufu wa chakula na mapato kwa wakazi wa mkoa huo. Hii pia inasababishwa na sera zilizopitwa na wakati kuhusu masoko ya mazao ya Kilimo na haswa kahawa kiasi cha wakazi wa Kagera kupeleka kahawa Uganda.

2. Miundombinu ya barabara na reli katika mkoa huo ni duni, hivyo kufanya usafirishaji wa mazao na bidhaa kuwa mgumu na gharama kuwa kubwa. Licha ya kuwa Mkoa huu uliathiriwa sana na vita vya Kagera hapakuwa na mpango Maalumu wa kuhuisha Uchumi wa Kagera baada ya vita na Ndio maana kumekuwa na mdororo wa Uchumi wa Mkoa huu.

3. Elimu na afya ni changamoto kubwa katika mkoa huo. Huduma za afya na elimu zinapatikana kwa kiwango kidogo, hivyo kusababisha wakazi wa mkoa huo kuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.

4. Kagera ilipata athari kubwa ya tetemeko la ardhi mwaka 2016 ambapo nyumba nyingi na miundombinu iliharibiwa na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi na uchumi wa mkoa huo.

5. Sera mbovu za Serikali ya CCM ambazo hazizingatii muktadha wa kimaeneo katika shughuli za Uchumi. Kwa Mfano Mfumo wetu wa utawala wa Viongozi ‘kuletwa’ kutoka Juu unaondoa ubunifu na uwajibikaji hivyo mikoa kutotumia fursa zao kwa ukamilifu na kukosekana ushindani wa mikoa kimaendeleo.

Chama cha ACT Wazalendo kinadhamiria kurejesha heshima ya Mkoa wa Kagera kwa kuugeuza kuwa Kituo cha Biashara na Viwanda kwa Nchi za EAC. Vile vile kushawishi Mradi wa Kabanga Nickel kufungamanishwa na shughuli za Uchumi za Watu wa Kagera.
 
Badala aongelee kwao kigoma kwa mafukara anajadili ya jiran
Screenshot_20231018_145904_WhatsApp.jpg

Wahaya mnaponzwa na SIFA za kijinga na dharau. Nilifikiri mungebadilika baada ya vita vya Kagera, maana enzi zile ukikutana na Mhaya JKT au Sekondari anajitambulisha kama Mganda Kyaka. Baada ya Iddi Amin kuwapa kichapo ndiyo mkaanza kuukubali Utanzania
 
View attachment 2785390
Wahaya mnaponzwa na SIFA za kijinga na dharau. Nilifikiri mungebadilika baada ya vita vya Kagera, maana enzi zile ukikutana na Mhaya JKT au Sekondari anajutambulisha kama Mganda Kyaka. Baada ya Iddi Amin kuwapa kichapo ndiyo mkaanza kuukubali Utanzania
Haya! anzeni kutoa na sababu za KIDINI tena, maana yake sisi Watanzania kutokana na elimu duni na mitazamo finyu, mkoa ukiwa waskini utaskia wale ni 'wachawi, dini flani, wavivu' etc. Watu tunasahau kuwa maendeleo kama maendeleo huletwa na serikali, watu binafsi huwa wanachangia tuu! Ndio maana hata huko mnakosifia maendeleo hakuna mtu binafsi alijenga barabara au hospitali!
 
Mheshimiwa Zito hizo sababu ulizotoa siyo sababu ya huo unaoita umaskini wa Wana kagera. Vipimo ulivyotumia ni vya GDP na hicho siyo kipimo Cha kipato Cha mtu mmoja mmoja.
Kitakacho pandisha GDP ni uwekezaji unaoendana na miundo mbinu inayojengwa na serikali pamoja na wawekezaji wa jumla, Barabara nzuri, viwanda vya mazao ya viwanda na kilimo, taasisi za vyuo vya elimu ya juu, huduma za usafirishaji kama vile Meri ndani ya ziwa Victoria za kwenda Mwanza-kenya na Uganda, ndege, reli ya SGR ya kwenda Rwanda na Burundi.
Kurekebisha sera mbovu za uuzaji wa mazao ya mkulima hasa kahawa. Uganda ambayo ni pua na mdomo na Tanzania wananunua kahawa karibia Bei ya mara mbili ya Tanzania. Nk
 
Hamna bana!! Nyinyi tatizo ni attitude yenu tu ndiyo inawaponza. Mnajisikia sana, hata ambaye hajafika Sekondari anataka aongee Kiingereza ili kumuonyesha mtu kuwa yeye kasoma. Kwenye maofisi mnapendeleana sana kupeana vyeo kikabila. Kwani Serikali imeifanyia nini Njombe au Ruvuma ambazo ziko juu yenu?
 
KUTOKA KAGERA

- 51% ya wakazi wake wanatumia chini ya TZS 1,644 kwa siku ( mstari wa umasikini Tanzania ni TZS 49,320 kwa Mwezi ).

- Pato la Wastani la Mtu wa Kagera ni TZS 1.2M kwa Mwaka. Mtu wa Ruvuma na Iringa ana Pato la Wastani mara 3 zaidi ya mtu wa Kagera.

- Mwaka 1994 Kagera ilishika nafasi ya 12 kati ya Mikoa 21 nchini kwa hali ya Uchumi, Mwaka 2022 inashika nafasi ya 26 kati ya Mikoa 26, yaani Ndio Mkoa masikini zaidi nchini.

Iweje Mkoa wa Kagera uwe masikini zaidi? Ni Mkoa wenye ardhi iliyopandwa kahawa kuliko Mkoa wowote nchini, ni Mkoa wenye utajiri mkubwa wa ardhi na hali ya hewa, ni Mkoa uliokaa kimkakati kijiografia ( unapakana na Nchi nyingi zaidi za Afrika Mashariki kuliko Mkoa mwengine wowote), una rasilimali madini kama Nickel na una wasomi wengi zaidi kuliko mikoa mingi ya Tanzania! Kwanini uwe Mkoa masikini zaidi?

Kuna sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

1. Uchumi wa mkoa huo unategemea sana kilimo ambacho kinategemea mvua. Hivyo, ukame au mvua zinazopungua zinaweza kusababisha upungufu wa chakula na mapato kwa wakazi wa mkoa huo. Hii pia inasababishwa na sera zilizopitwa na wakati kuhusu masoko ya mazao ya Kilimo na haswa kahawa kiasi cha wakazi wa Kagera kupeleka kahawa Uganda.

2. Miundombinu ya barabara na reli katika mkoa huo ni duni, hivyo kufanya usafirishaji wa mazao na bidhaa kuwa mgumu na gharama kuwa kubwa. Licha ya kuwa Mkoa huu uliathiriwa sana na vita vya Kagera hapakuwa na mpango Maalumu wa kuhuisha Uchumi wa Kagera baada ya vita na Ndio maana kumekuwa na mdororo wa Uchumi wa Mkoa huu.

3. Elimu na afya ni changamoto kubwa katika mkoa huo. Huduma za afya na elimu zinapatikana kwa kiwango kidogo, hivyo kusababisha wakazi wa mkoa huo kuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.

4. Kagera ilipata athari kubwa ya tetemeko la ardhi mwaka 2016 ambapo nyumba nyingi na miundombinu iliharibiwa na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi na uchumi wa mkoa huo.

5. Sera mbovu za Serikali ya CCM ambazo hazizingatii muktadha wa kimaeneo katika shughuli za Uchumi. Kwa Mfano Mfumo wetu wa utawala wa Viongozi ‘kuletwa’ kutoka Juu unaondoa ubunifu na uwajibikaji hivyo mikoa kutotumia fursa zao kwa ukamilifu na kukosekana ushindani wa mikoa kimaendeleo.

Chama cha ACT Wazalendo kinadhamiria kurejesha heshima ya Mkoa wa Kagera kwa kuugeuza kuwa Kituo cha Biashara na Viwanda kwa Nchi za EAC. Vile vile kushawishi Mradi wa Kabanga Nickel kufungamanishwa na shughuli za Uchumi za Watu wa Kagera.
hajakosea, amesema kweli kabisa. kinachowaokoa ni matoke, wanakuwa na chakula ila mfukon hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom