Zitto Kabwe: Miaka minne ya Magufuli deni la Taifa limeongezeka sawa na miaka 10 ya Kikwete

Unajua kabla ya ku comment ungemuuliza Zitto atoe uchambuzi wa matumizi ya hiyo mikopo iliyochukuliwa wakati wa kikwete na ya wakati wa Magufuli. Ndiyo maana tuna akili tumepewa na Mungu tuzitumie kama kuna mpotoshaji akitokea tuweze kuzitumia.

Mfano Tanzania ilikua vituo vya afya 77 tangu Uhuru ina maana Nyerere, Mwinyi, Mkapa na rafiki yake zitto Jakaya Kikwete wote hao katika miaka zaidi ya 50 walijenga vituo 77. Huyu mnayemsema leo katika miaka yake minne madarakani kajenga vituo 352. Katika hivyo Hospitali za Halmashauri zipo 9, Vituo vya afya vipo 304 na zahanati 39. Amekaratabati Meri 3, anajenga meri mpya ziwa victoria. Anajenga reli anajenga bwawa la umeme. Amenunua ndege n.k Hivyo kimahesabu anaweza kukokotoa na ukakubali. Sasa tuambie hizo za miaka 10 ya kikwete ipi miradi mikubwa aliifanya?????

Ukizingatia makokotoo kama hayo hutaweza kudanganywa na wapiga zumari kama kina zitto.

acha kumezeshwa propaganda hospitali za kata zimejengwa sana na JK
 
Adui namba moja wa maendeleo ya nchi yetu ni ccm na watu wake. Siku ya kuwaondoa hawa mchwa, hakika kila Mtanganyika na Mzanzibari atafurahia matunda ya Uhuru wa nchi yake.
Sawa Ni adui lakin maendeleo ya kweli s kwa kukopa wakati tuna rasilimali nying Sana ambapo tunatakiwa tulipwe mishahara bila kufanya Kaz yeyote

Wazee,omba omba,wajengewe makaz yakutosha nyumba ziwe bwerere kabisa.

Lakini tulishazoea kukopa kopa.hatuna washaur au wachum wenye kuleta tija katika taifa
 
Ndugu zitto mdini sana uyu kijana
mkoa wa kagera una upungufu wa matundu ya choo 2232 kwa ajili ya shule za msingi. ni upuuzi kuamini kwamba ndege ni maendeleo. social assessment need iliyofanyika DODOMA inaonesha kwamba hata pakiwa makao makuu patakuwa na upungufu mkubwa wa huduma za kijamii. kiongozi kichaa anaamua kupeleka makao makuu Dodoma kisa alisema nyerere miaka hiyoooooo. vichaa wenzake wanakenua maeno wakimshangilia kwa kuimba nyimbo za taarabu kama wafanyavyo pale chimwaga.
ni aibu karne ya 21 mtu kuacha kujibu hoja na kukimbilia udini. shame on you
 
Miradi ipi hiyo inayokopewa pesa wakati mnasema ndege, SGR na Stiegler mnajenga kwa pesa za ndani?!!
Pesa zetu ni pamoja na mikopo ya mashart nafuu. Pesa zetu za ndani ndio zitakazolipa.
Taahira pekee ndiye hajaelewa kuwa ukikopa unakuwa umetangulia kutumia Pesa utakayoikusanya baadaye. Ngoja niishie hapa katika kukuelewesha
 
Ndio tatizo la kuwa na akili za kushikiwa!! Yale yale anaulizwa mbona deni linakuwa anasema bado ni stahimilivu!! Dunia nzima nchi zinakopa lakina hawakatai!! Hapa serikali inakopa kwa kuficha ficha ila wenye akili wanajua tu ila wale nyumbu kama wewe wazee wa praise team ni kawaida yenu!! Hoja kama hatukopi kulingana na matamko ya serikali hilo deni linakuwaje kubwa kwa kasi hiyo? Ukope mkopo wa kibiashara kwa kujenga reli ambayo baada ya miaka 20 ndio itaanza kuleta faida?!!
Serikali gani isiyokopa? Hapa zito kacheza na akili zenu nyie maahira msiojua kupelemba mambo. Rais na Watanzania wanaposema Pesa zetu wenyewe wanatofautisha na misaada.
Pesa zetu wenyewe ni pamoja na mikopo, makusanyo ya kodi, magawio ya hisa nk. Mkopo maana yake ni kutangulia kuitumia Pesa utakayoikusanya baadaye.
Sina kauli iliyosema tunajenga kwa kwa Pesa za makusanyo ya ndani tu. Hata hivyo pia kiwango cha makusanyo ya ndani yanaamua tukope kiasi gani.
Hivyo zito asitegemee makusanyo ya bilioni 800 atakopa sawa na mwenye makusanyo ya tir 1.5
 
ZITTO KABWE: MIAKA MINNE YA MAGUFULI DENI LA TAIFA LIMEONGEZEKA SAWA NA MIAKA 10 YA KIKWETE.

Na: Suphian Juma

Wakati Serikali ya Magufuli inajinasibu kuwa ya wanyonge na kwamba Rais Magufuli ndiye Rais pekee kupata kutokea tangu tupate Uhuru na kwamba kama kuna tatizo kubwa la kitaifa halijatatuliwa na yeye awali hii, hapatatokea Rais mwingine atakayekuwa na ubavu wa kulitatua; Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT wazalendo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hususani Twitter ameonesha takwimu na hivyo kusikitishwa na ongezeko la Deni la Taifa lisilomithilika.

Hapa nimewasogezea mtiririko wa 'tweets' (posts) nne ambazo Zitto ameziandika kupitia Twitter leo Sept 27, 2019.

1. Deni lote la Taifa ( Ndani na Nje ) limeongezeka kutoka shilingi Trilioni 43 mwaka 2015 Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mpaka shilingi Trilioni 65 mwezi Julai 2019! Ongezeko la Deni kiasi cha shilingi Trilioni 22, sawa na kukopa 5.5tr/mwaka, 0.5tr/mwezi, 17bn/Siku.

2. Serikali ya Awamu ya Tano imefikisha Deni la Nje USD 22 bilioni ndani ya miaka 4 tangu iingie madarakani. Serikali ya Rais John Magufuli katika miaka 4 imeliingiza Taifa katika Deni la USD 7 bilioni sawasawa na Deni lote lililokopwa katika miaka 10 ya Rais Jakaya Kikwete.

3. Serikali ya Awamu ya 4 ilipoingia Madarakani Deni la Taifa la Nje lilikuwa USD 8 billioni ( Novemba 2005 ). Wakati inaondoka madarakani, miaka 10 baadaye, Deni la Nje lilikuwa limefikia USD 15 bilioni ( Novemba 2015 ). Ongezeko la USD 7 bilioni.

4. Septemba 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna ajira mpya kiivo. Hakuna nyongeza ya mishahara kisheria, wafanyakazi wanalia kila siku. Wanaopanda vyeo hawalipwi mishahara ya vyeo vyeo vipya ( wafanyakazi wa Umma wanalia kila siku ). Masikini waliostaafu miaka 2 iliyopita mpaka leo hawajalipwa. HATUDANGANYIKI.

Kwakuwa Watanzania sio wajinga, nadhani ni vyema sasa tukatafakari kwa kina suala hili, tukizingatia tunavyozidi kuwa maskini kila uchwao tofauti na miaka iliyopita kabla ya 2015. Na kwamba kama dhumuni la kuwa na Serikali na Rais Mpya ni kuwa na maisha bora, na dhumuni hili halijatimia, je bado tutamchagua tena Magufuli 2020 au badala yake tutahakikisha tumchagua Rais Mpya, Serikali Mpya na Chama kimya Ikulu ili kuirejesha NCHI kwenye MISINGI ya MATUMAINI kwa VITENDO?

TUTAFAKARI.

ACT wazalendo tupo nanyi DAIMA!

Suphian Juma
Sept 27, 2019
Singida.View attachment 1217215
Inawezekana sana kuwa deni la Taifa likawa kubwa kuliko kipindi cha JK, lakini katika kipindi cha miaka minne ya JP pesa[pamoja na mikopo] kwa ajili ya maendeleo zimefanya kazi kubwa na za kuonekana kuliko kipindi chote cha uhai wa nchi yetu.
'Love him Hate but facts remains to be facts.
 
Kazi gani?
 
Ni kumuabisha Kikwete wa miaka 10 kumlinganisha na Magufuli wa miaka 4.
Kuna watu wanaamini Awamu nyingine hazikufanya mambo kama awamu hii. hawa wamemeza ndoano ya propaganda

AWAMU YA NNE ilifanya mengi kwa mfano

1.Barabara alozojenga JK mmezisahau?
2.Umeme kinyerezi 1
3.Bomba la gesi
4.UDOM
5.Mloganzila hospital
6.Jakaya Kikwete Health Institute
7.Barabara za Mwendokasi Dar
8.Ajira za kila mwezi
9.Nyongeza za Mishahara ya wafanyakazi
10. Vivuko alivyokuwa akifungua Magufuli akiwa kama waziri wa ujenzi
11.Repair ya viwanja vya ndege
12.Hospitali za kata
13.Madaraja ya Kigamboni, Malagarasi etc
14. Mradi wa maji ruvu chini
15. Airport Terminal III
16.Majumba ya maaskari kila kona ya nchi
17.Kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaopata mkopo elimu ya juu

Hayo mambo yalifanywa na serikali ya Magufuli?
 
Tunapesa keshi sisi hatunaga machezo
ZITTO KABWE: MIAKA MINNE YA MAGUFULI DENI LA TAIFA LIMEONGEZEKA SAWA NA MIAKA 10 YA KIKWETE.

Na: Suphian Juma

Wakati Serikali ya Magufuli inajinasibu kuwa ya wanyonge na kwamba Rais Magufuli ndiye Rais pekee kupata kutokea tangu tupate Uhuru na kwamba kama kuna tatizo kubwa la kitaifa halijatatuliwa na yeye awali hii, hapatatokea Rais mwingine atakayekuwa na ubavu wa kulitatua; Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT wazalendo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hususani Twitter ameonesha takwimu na hivyo kusikitishwa na ongezeko la Deni la Taifa lisilomithilika.

Hapa nimewasogezea mtiririko wa 'tweets' (posts) nne ambazo Zitto ameziandika kupitia Twitter leo Sept 27, 2019.

1. Deni lote la Taifa ( Ndani na Nje ) limeongezeka kutoka shilingi Trilioni 43 mwaka 2015 Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mpaka shilingi Trilioni 65 mwezi Julai 2019! Ongezeko la Deni kiasi cha shilingi Trilioni 22, sawa na kukopa 5.5tr/mwaka, 0.5tr/mwezi, 17bn/Siku.

2. Serikali ya Awamu ya Tano imefikisha Deni la Nje USD 22 bilioni ndani ya miaka 4 tangu iingie madarakani. Serikali ya Rais John Magufuli katika miaka 4 imeliingiza Taifa katika Deni la USD 7 bilioni sawasawa na Deni lote lililokopwa katika miaka 10 ya Rais Jakaya Kikwete.

3. Serikali ya Awamu ya 4 ilipoingia Madarakani Deni la Taifa la Nje lilikuwa USD 8 billioni ( Novemba 2005 ). Wakati inaondoka madarakani, miaka 10 baadaye, Deni la Nje lilikuwa limefikia USD 15 bilioni ( Novemba 2015 ). Ongezeko la USD 7 bilioni.

4. Septemba 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna ajira mpya kiivo. Hakuna nyongeza ya mishahara kisheria, wafanyakazi wanalia kila siku. Wanaopanda vyeo hawalipwi mishahara ya vyeo vyeo vipya ( wafanyakazi wa Umma wanalia kila siku ). Masikini waliostaafu miaka 2 iliyopita mpaka leo hawajalipwa. HATUDANGANYIKI.

Kwakuwa Watanzania sio wajinga, nadhani ni vyema sasa tukatafakari kwa kina suala hili, tukizingatia tunavyozidi kuwa maskini kila uchwao tofauti na miaka iliyopita kabla ya 2015. Na kwamba kama dhumuni la kuwa na Serikali na Rais Mpya ni kuwa na maisha bora, na dhumuni hili halijatimia, je bado tutamchagua tena Magufuli 2020 au badala yake tutahakikisha tumchagua Rais Mpya, Serikali Mpya na Chama kimya Ikulu ili kuirejesha NCHI kwenye MISINGI ya MATUMAINI kwa VITENDO?

TUTAFAKARI.

ACT wazalendo tupo nanyi DAIMA!

Suphian Juma
Sept 27, 2019
Singida.View attachment 1217215
 
Jamani hebu tueleweshane hapo. Deni likiongezeka huku pesa hizo zinafanya miradi mingi inayoonekana tatizo liko wapi? Si ni kama kukopa bank. Shida kwa maoni yangu ni kama deni likitumika vibaya ndio tumcharure Uncle Magu. Tupeane elimu wadau labda mimi naelewa vibaya

Miradi ipi Mkuu ?

kwani hela zetu za ndani zinafanya nini?
 
Sio donor fund projects kama danida, jica, au USaid. Ni pesa amabazo hata tukikopa ni lazima tuzilipe. Zinatoka adb au wb. Tuna miradi nzima ya barabara, meli, vivuko, umeme, maji, afya, utalii, bandari, viwanja vya ndege. Kodi inayokusanywa haifikii hizo gharama.
Basi asiseme amechota chunguni!
 
Pesa zetu ni pamoja na mikopo ya mashart nafuu. Pesa zetu za ndani ndio zitakazolipa.
Taahira pekee ndiye hajaelewa kuwa ukikopa unakuwa umetangulia kutumia Pesa utakayoikusanya baadaye. Ngoja niishie hapa katika kukuelewesha
Tahira ni wewe na hao wapumbavu wenzako mnaoshindwa kutofautisha kati ya mkopo na pesa yako mwenyewe!
 
Kuna watu wanaamini Awamu nyingine hazikufanya mambo kama awamu hii. hawa wamemeza ndoano ya propaganda

AWAMU YA NNE ilifanya mengi kwa mfano

1.Barabara alozojenga JK mmezisahau?
2.Umeme kinyerezi 1
3.Bomba la gesi
4.UDOM
5.Mloganzila hospital
6.Jakaya Kikwete Health Institute
7.Barabara za Mwendokasi Dar
8.Ajira za kila mwezi
9.Nyongeza za Mishahara ya wafanyakazi
10. Vivuko alivyokuwa akifungua Magufuli akiwa kama waziri wa ujenzi
11.Repair ya viwanja vya ndege
12.Hospitali za kata
13.Madaraja ya Kigamboni, Malagarasi etc
14. Mradi wa maji ruvu chini
15. Airport Terminal III
16.Majumba ya maaskari kila kona ya nchi
17.Kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaopata mkopo elimu ya juu

Hayo mambo yalifanywa na serikali ya Magufuli?
Sasa mbona mlitudanganya kuwa Ni dhaifu na mpenda Raha Kama Vasco dagama? Tena mkatuwekea na picha akiwa anabembea Jamaica, kumbe waongo tu, shenzi zenu
 
Kwani awamu ya 4 zilifanyika shughuli gani za kiuchumi zinazoonekana kwa macho haya ya mwili?!!......mbona ilitkopa fedha nyingi sana!!!!
Kuna member humu ndani kakudharau sana na kukuita bogus na hapa unathibitisha uwezo wako mdogo Wa kufikiri! Ni kweli unajihakikishia kwa dhati ya moyo wako kuwa awamu zilizopita hazikujenga miradi yoyote inayoonekana kwa macho?
Basi wewe sio kipofu Wa macho tu bali na ubongo!
Udom, upanuzi Wa uwanja Wa ndege Wa jkn, daraja LA mkapa na malagarasi, hospitality ya mloganzila Barbara za lami zilizosimamiwa na Hugo unayemwabudu na kumtukuza kuliko muumba wako, sekondari za kata na vingine Vingi vilishushwa kutoka mawinguni?
Ficha unafiki wako sometime unatia aibu! Haiyumkini umekosa hata Wa kukuoa kwa hii tabia yako ya kinafiki!
 
Kitu watu wengi wasicho Kijua ni kwamba Mkapa hakukopa Bali alilipa madeni,na ndiyo kiongozi wa pili kupewa na nyerere,Baada ya hapo viongo wanaofuata ni kiki kwa kwenda mbele.ndiyo maana hili halitangazwi akapewa sifa zake
 
ZITTO KABWE: MIAKA MINNE YA MAGUFULI DENI LA TAIFA LIMEONGEZEKA SAWA NA MIAKA 10 YA KIKWETE.

Na: Suphian Juma

Wakati Serikali ya Magufuli inajinasibu kuwa ya wanyonge na kwamba Rais Magufuli ndiye Rais pekee kupata kutokea tangu tupate Uhuru na kwamba kama kuna tatizo kubwa la kitaifa halijatatuliwa na yeye awali hii, hapatatokea Rais mwingine atakayekuwa na ubavu wa kulitatua; Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT wazalendo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hususani Twitter ameonesha takwimu na hivyo kusikitishwa na ongezeko la Deni la Taifa lisilomithilika.

Hapa nimewasogezea mtiririko wa 'tweets' (posts) nne ambazo Zitto ameziandika kupitia Twitter leo Sept 27, 2019.

1. Deni lote la Taifa ( Ndani na Nje ) limeongezeka kutoka shilingi Trilioni 43 mwaka 2015 Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mpaka shilingi Trilioni 65 mwezi Julai 2019! Ongezeko la Deni kiasi cha shilingi Trilioni 22, sawa na kukopa 5.5tr/mwaka, 0.5tr/mwezi, 17bn/Siku.

2. Serikali ya Awamu ya Tano imefikisha Deni la Nje USD 22 bilioni ndani ya miaka 4 tangu iingie madarakani. Serikali ya Rais John Magufuli katika miaka 4 imeliingiza Taifa katika Deni la USD 7 bilioni sawasawa na Deni lote lililokopwa katika miaka 10 ya Rais Jakaya Kikwete.

3. Serikali ya Awamu ya 4 ilipoingia Madarakani Deni la Taifa la Nje lilikuwa USD 8 billioni ( Novemba 2005 ). Wakati inaondoka madarakani, miaka 10 baadaye, Deni la Nje lilikuwa limefikia USD 15 bilioni ( Novemba 2015 ). Ongezeko la USD 7 bilioni.

4. Septemba 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna ajira mpya kiivo. Hakuna nyongeza ya mishahara kisheria, wafanyakazi wanalia kila siku. Wanaopanda vyeo hawalipwi mishahara ya vyeo vyeo vipya ( wafanyakazi wa Umma wanalia kila siku ). Masikini waliostaafu miaka 2 iliyopita mpaka leo hawajalipwa. HATUDANGANYIKI.

Kwakuwa Watanzania sio wajinga, nadhani ni vyema sasa tukatafakari kwa kina suala hili, tukizingatia tunavyozidi kuwa maskini kila uchwao tofauti na miaka iliyopita kabla ya 2015. Na kwamba kama dhumuni la kuwa na Serikali na Rais Mpya ni kuwa na maisha bora, na dhumuni hili halijatimia, je bado tutamchagua tena Magufuli 2020 au badala yake tutahakikisha tumchagua Rais Mpya, Serikali Mpya na Chama kimya Ikulu ili kuirejesha NCHI kwenye MISINGI ya MATUMAINI kwa VITENDO?

TUTAFAKARI.

ACT wazalendo tupo nanyi DAIMA!

Suphian Juma
Sept 27, 2019
Singida.View attachment 1217215

Mropokaji mwingine na data za kupikwa. Kama haya ni kweli kwa nini hayaongelei Bungeni? The guy is bogus.
 
Kwani awamu ya 4 zilifanyika shughuli gani za kiuchumi zinazoonekana kwa macho haya ya mwili?!!......mbona ilitkopa fedha nyingi sana!!!!
Acheni kufuru, binafsi nakubali utendaji kazi wa jpm, lakn jk kafanya mengi kwa uwezo wake ni wakati wa awamu ya 4 mikoa yote ya iliunganishwa kwa Lami, na barabara nyingi zilijengwa, zahanati na hospital zilijengwa…unafikiri km jk asingekuwa anawaza kuhusu kuwabebesha vizazi vijavyo mzigo was madeni, angeshindwa kukopa afanye miujiza? Mnakera kila mradi fedha za ndani kumbe mnakopa
 
Kuna member humu ndani kakudharau sana na kukuita bogus na hapa unathibitisha uwezo wako mdogo Wa kufikiri! Ni kweli unajihakikishia kwa dhati ya moyo wako kuwa awamu zilizopita hazikujenga miradi yoyote inayoonekana kwa macho?
Basi wewe sio kipofu Wa macho tu bali na ubongo!
Udom, upanuzi Wa uwanja Wa ndege Wa jkn, daraja LA mkapa na malagarasi, hospitality ya mloganzila Barbara za lami zilizosimamiwa na Hugo unayemwabudu na kumtukuza kuliko muumba wako, sekondari za kata na vingine Vingi vilishushwa kutoka mawinguni?
Ficha unafiki wako sometime unatia aibu! Haiyumkini umekosa hata Wa kukuoa kwa hii tabia yako ya kinafiki!
Bwashee unateseka sana.

Sasa huyo Zitto wako haoni shughuli inayofanyika awamu hii hadi ajifanye anashangaa.
Watu wanajua huyo Zitto " wako" alivyokuwa anapiga hela pale bandarini kwa nafasi yake ya boss PAC ambazo ni mkopo na kusababisha gati zisijengwe.

Hizo akili zako za Mbege wapelekee wenzio pale ufipa!
 
Back
Top Bottom