Zitto kabwe matatani tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto kabwe matatani tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 2, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Zitto matatani
  I
  Safari ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe nchini Hispania katika mkutano wa kuwakilisha shirika lisilo la kiserikali la Majirani Wasio na Mipaka (NWB) la mjini hapa, imezua mtafaruku mkubwa miongoni mwa viongozi na wanachama wa shirika hilo. Mtafaruku huo unatokana na kitendo cha baadhi ya wanachama kuhoji sababu za Zitto kuliwakilisha shirika hilo katika mkutano huo wakati Mbunge huyo hana nafasi yoyote ndani ya shirika hilo.

  Hayo yalibainika katika mkutano mkuu wa shirika hilo uliofanyika juzi mjini hapa na katika kujadili hoja hiyo, wajumbe walitoa azimio la kutotambua uwakilishi wa Mbunge huyo kwenye mkutano huo. Katika maazimio yao, wajumbe wa mkutano huo, walisema chochote kitakachofanywa na Mbunge huyo katika safari na mkutano huo kisihusishwe kwa namna yoyote na shirika hilo.

  Akisoma maazimio hayo, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Pashal Likutuye, alisema pamoja na maazimio hayo, pia wajumbe walilaani kitendo cha Mwakilishi wa Shirika la VSF la Hispania, John Shaaban, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Shaban Mambo (Chadema) kumteua Zitto bila kuitaarifu Bodi ya NWB. Hivi sasa Shaban amefukuzwa nchini kutokana na mtafaruku huo na kufanya kazi nchini bila kibali, sambamba na kukiuka taratibu za hati zinazomruhusu kuishi nchini.

  Mwanachama mwingine, Saidi Maulid, alidai kuwa kwa kiasi kikubwa uteuzi wa Zitto kuliwakilisha shirika hilo Hispania uliegemea kwenye maslahi ya kisiasa kuliko hali halisi, na kuhoji kama shirika hilo halina watu wanaokidhi vigezo vya kuhudhuria mkutano huo na kuliwakilisha shirika badala ya Zitto. Akijibu hoja hiyo, Mwakilishi wa VSF ambayo inatoa ufadhili kwa NWB, Mambo alidai kuwa yeye binafsi ndiye aliyemteua Zitto kuhudhuria mkutano huo.

  Mambo alidai kuwa sababu kubwa iliyomfanya amteue Zitto ni kutokana na mradi mkubwa wa utalii unaotarajiwa kuanza mkoani Kigoma na kwamba anahitajika mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja kwa ajili ya wananchi wa Kigoma. Katika hatua nyingine, mkutano huo ulitoa azimio la kumtaka Naibu Meya huyo kuacha kuingilia mambo ya ndani ya NWB kwa vile yeye si kiongozi wala mwanachama wake. Akihitimisha mjadala huo, Mwenyekiti wa Bodi ya NWB, Iddi Ndabhona, alitoa mwito kwa watu kufuata sheria, kanuni na miongozo ya kiutendaji ya shirika hilo.

  Ndabhona alisema kamwe Bodi yake haitakubali watu wachache wajichukulie madaraka ya kufanya mambo kwa niaba ya shirika bila Bodi kuhusishwa na kutoa baraka kwa jambo hilo kufanyika. Hivi sasa kumezuka mtafaruku mkubwa kati ya NWB na wafadhili hao VSF hata kusababisha kusimamishwa ufadhili huo hali ambayo imeanza kuliathiri shirika hilo. Kwa upande wake, Zitto alikiri kuliwakilisha shirika hilo Hispania ambako lilijadili masuala ya utalii. ''Ni kweli nimeshakwenda hiyo safari ambayo hata hivyo nilijilipia mwenyewe nauli ila malazi ndiyo nililipiwa na barua zao za kunialika ninazo.''

  Alisema shirika hilo limekuwa likitoa misaada Kigoma lakini kwa taarifa alizonazo ni kwamba uongozi wake umekuwa katika mgogoro ambao ulifikia hadi kumfikisha mwenzao, Shaban, Uhamiaji kwa madai kuwa anafanya kazi nchini bila kibali jambo ambalo yeye (Zitto) alizungumza na Uhamiaji akaachiwa. ''Labda kwa hilo ndio wamenikasirikia, lakini ninachosema sitaki kabisa wanihusishe na ugomvi wao, mimi kweli si mwanachama wa shirika hilo lakini ni Mbunge ninayewakilisha wananchi, hivyo safari hiyo imekuwa na manufaa kwa jimbo langu hususan upande wa utalii,'' alisema Zitto.

  Alisema hana ugomvi wowote na mwanachama wa shirika hilo na kama ni hiyo safari, hakwenda kwa manufaa yake, bali kwa manufaa ya wananchi jambo ambalo limemfanya mpaka sasa awe anadaiwa na wakala wa usafiri wa Interline dola 1,400 za Marekani za nauli ya safari hiyo. Aliwataka viongozi wa shirika hilo kuacha kuzozana na badala yake watafute mwafaka ili kutowasababisha wafadhili kukimbia kwa maslahi ya wachache.
   
Loading...