Nashindwa kukuelewa unapomtetea Mzungu aliekutawala kimabavu karne na karne na kukuibia maliasili yako! bila shaka una damu ya kizungu! huenda ama Mama ako ni Mzungu au Baba ndio mzungu!
Mimi simtetei Muarabu au Mzungu bali nazungumza kwa ushahidi kwamba kati ya Mzungu na Mwarabu ninani alietutawala Tanganyika? sasa Kama Zito Kabwe anawalaumu Wazungu kwa uthibitisho wa kutuibia mali zetu! wewe mbona unaigeuza issue hiyo kwa waarabu?
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe mbunge wa Kigoma Kusini na Waziri Kivuli wa CHADEMA amewalaani wazungu kwa utapeli na uporoji mkubwa wanaoufanya dhidi ya Waafrika! nadhani umefika wakati kwa Serikali yetu kuamka na kua macho na Wazungu wote wanaoingia nchini mwetu kwani hawana nia nzuri na nchi yetu!
habari zaidi kuhusu hoja za Zito gonga hapa: Home
I salute you Zitto Zuberi Kabwe!! My worry is what impacts will it have thereafter!! Do they real listened to you??
Si Zitto wala mtu yeyote atakayenifungia kwenye box la kuwaza anavyowaza yeye kwamba eti wezi wazungu ndio adui wa maendeleo yetu. Kama unataka kuongea suala la maendeleo uende kwa upana na ujadili kwa haki pasipokuwa na hidden agendas ama hila kama za Zitto.
Ukipata nafasi tuwasiliane kwenye private boxes tuanzishe threads mbili. Moja ilinganishe athari hasi na chanya kati ya ujio wa Wazungu na waarabu katika tanganyika. Usikubali kukaririshwa mambo.
Thread nyingine tujadili ubora na udhaifu wa utawala wa Wazungu na CCM. Siasa za kukariri bila kufanya analysis hazitufikishi tunapotaka kufika.
katika mijadala ya asubuhi ya kituo cha televisheni cha startv jumapili iliyopita, wageni waalikwa katika mjadala ule walimulalamikia mh.zitto kwa kukurupusha hoja ambazo anashindwa kuzisimamia.kudhibitisha hili ni kuwa katika bunge lililopita alisema atawataja walioficha pesa uswizi kama serikali haitawataja lakini wiki mbili zilizopita mh. Zitto amesikika kupitia startv hiyohiyo kuwa hatawataja.
Hatujakaa sawa anaibuka na habari za kuwalaumu wazungu kwa wizi. Njia bora ilikuwa mh. Zitto anahakikisha tunajisafisha sisi kwanza kwa kuwashughulikia wezi tunaowajua na kuziba mianya ya wizi kama mh.zitto alivyokuwa amenuia huko bungeni ndipo sote kwa pamoja tuwageukie wazungu wezi.
Kitendo hiki cha mh.zitto kuwarukia wazungu wakati hili la kuwashughulikia wezi wa ndani kinatoa tafsiri mbaya sana juu yake juu nia aliyokuwa nayo kuhusu tuhuma alizozitoa bungeni za pesa za wizi zilizofichwa uswisi, binafsi naona zitto anataka kutumia mwanya huu wa kuwashambuliwa wazungu kufifisha suala zima alililojiapiza kushiriki kulikabili yaani suala la watanzania kuficha pesa za wizi uswisi na kwingineko.
Zitto kuruka ruka na hoja ambazo azisimamii bado anazidi kudororesha imani ya raia wa tanzania kuwaamini vijana katika shughuli za kuikwamua nchi yetu kutoka kwenye lindi la matatizo mengi ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kadhalika.
Kwa mara nyingine namtahadharisha zitto aache mtindo wake huu wa kudidimiza nia ya watanzania ya kuwaamini vijana kuwa na uwezo wa kukwamua nchi yao kwani yeye bado anabeba taswira ya mwanasiasa kijana. Kama hawezi kujirekebisha basi ajiuzulu masuala yote ya siasa na aendelea na shughuli zake nyingine.
---mpigakelele
Amesema kweli wana Jf sema amependelea. Amerika, Waarabu na hao WAASIA wote lengo kummumiza Mwafrika.
Ukipata nafasi tuwasiliane kwenye private boxes tuanzishe threads mbili. Moja ilinganishe athari hasi na chanya kati ya ujio wa Wazungu na waarabu katika tanganyika. Usikubali kukaririshwa mambo.
Tatizo ni wageni,wala si wazungu pekee,kama alivyoainisha Zitto!je Mheshimiwa anataka kutuamini waarabu na waamerica ni watu safi na pia wanatupenda sana?
Habari kamili....
Zitto ambaye ni
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, alisema hayo wakati akihutubia mkutano wa masuala ya
ushirikiano wa uchumi kati ya Ujerumani na nchi za Afrika...
...
Zitto alisema kuwa nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikiporwa maliasili zake na
baadhi ya kampuni za kimataifa kupitia ukwepaji kodi pindi zinapokuja kuwekeza
barani humo...
..Alitaka mataifa rafiki kama Ujerumani kusaidia mataifa ya Afrika
katika juhudi za kukataa uporaji unaofanywa na mataifa yenye sera kama za
Uswisi.
CHANZO: NIPASHE
O.k kwahiyo akienda Uarabuni atazungumzia masuala ya ugaidi na ufilauni!!Tujaribu kuangalia tukio husika
Sidhani kama kwenye huu mkutano alitakiwa azungumzie kila kitu, amelenga yale anayoamini Ujerumani kama mwanachama wa umoja wa ulaya anaweza kusaidia
O.k kwahiyo akienda Uarabuni atazungumzia masuala ya ugaidi na ufilauni!!
Hapa nakubaliana na wewe nilichokuwa nakataa mimi ni kuwaona wazungu pekee kama maadui zetu wakati asilimia kubwa ya wageni ni maadui zetu.Mimi binafsi sina mahaba na mzungu, muarabu wala mkoloni mweusi wote lao moja hakuna rafiki yetu kati ya hao.
Hapa nakubaliana na wewe nilichokuwa nakataa mimi ni kuwaona wazungu pekee kama maadui zetu wakati asilimia kubwa ya wageni ni maadui zetu.
Uporaji? We Zitto acha unafiki! Ni nani mporaji kati ya viongozi wetu na wazungu? Mfano rafiki yako Idrisa alipopora fedha za rada mbona hukupiga kelele! Na huyo katibu wa chama chako cha magamba kinachokupa kichwa anapopora meno ya tembo mbona hupigi kelele? Na mtoto wa huyo rais wako anayekupa kichwa anapopora mbona hupigi kelele. By the way kwani wazungu hutushikia bunduki? Mikataba kama ile ya madini si nyie mliipitia?Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe mbunge wa Kigoma Kusini na Waziri Kivuli wa CHADEMA amewalaani wazungu kwa utapeli na uporoji mkubwa wanaoufanya dhidi ya Waafrika! nadhani umefika wakati kwa Serikali yetu kuamka na kua macho na Wazungu wote wanaoingia nchini mwetu kwani hawana nia nzuri na nchi yetu!
habari zaidi kuhusu hoja za Zito gonga hapa: Home