Zitto Kabwe awa gumzo Tabora, amfunika Lowassa

Zitto Kabwe awa gumzo Tabora, amfunika Lowassa

JOHN WA MARWA

Senior Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
100
Reaction score
61
Niko ndani ya mji wa tabora,nimeshuhudia ushawishi wa mwanasiasa maarufu sana hapa tanzania ndani ya mji wa tabora ndugu zitto zuberi kabwe,hapa mjini tabora bendera za act wazalendo chama ambacho zitto anakiongoza zimetapakaa mji mzima na vijiwe vyote ndani ya tabora ni mijadala kuhusu tukio la kesho kuzindua azimio la tabora,vijana na akina mama wanaonekana kuvutiwa na siasa anazofanya kijana machachali Zitto kabwe,,

Baadhi ya viongozi wa ACT wanaonekana mitaani wakiuza kadi za chama hiki kwa hamasa kubwa sana,hata lowassa alipofika hapa kutafuta wadhamini hakupata mapokeo kama haya aliyoyapata ndugi zitto kabwe.

Kesho jioni kutafanyika mkutano mkubwa wa hadhara wa kuzindua azimio la tabora kitu ambacho kinasubiriwa kwa hamu sana na wananchi wa tabora,hongera mdugu Zitto Kabwe
 
Hivi zoezi la viongozi wa Act kutangaza mali zao liliingia wapi? Ndio tutaweza kupima kama hilo azimio Lina maana ama ni ujinga tu......Mali za Mwigamba , Mtemelwa , Kitila, Msando , Mgwira ........
 
Akiendelea kwa kasi hii wafadhili wake watakata Ruzuku na ndio itakuwa Mwisho wake wa kuonekana hata Jukwaani.
 
Kuna watu hawataki kusikia ukweli kuhusu zitto,hasa chadema,ila zitto ni zaidi ya umjuavyo,ni mwanasiasa makini na anayejiamini,tunaanza nziara kesho,mnyika tangulia kama kawaida yako
 
Kuna watu hawataki kusikia ukweli kuhusu zitto,hasa chadema,ila zitto ni zaidi ya umjuavyo,ni mwanasiasa makini na anayejiamini,tunaanza nziara kesho,mnyika tangulia kama kawaida yako

Hakuna cha watu kutosikia ukweli. Sasa CHADEMA wanahusikaje na Zitto hapo. Yeye yuko kwenye chama chake basi. Acheni CHADEMA iendelee kupiga kazi. Hangaikeni na mambo yenu. Kama ni mpinzani wa kweli, watu ambao hawatapenda kusikia habari zake ni CCM, ambao ndio chama tawala maana wataogopa Zitto kuja kuwaondoa madarakani. CHADEMA sio chama tawala bhana, nawo wanahangaika km SACCOS ya Zitto kushika dola kutoka kwa CCM. Hayo ndio malengo ya chama chochote cha siasa
 
Mkuu hivi Chadema wako wapi maana naona mada zote humu zinahusu uchaguzi wa CCM inakuwaje? Yaani inafika hadi mnaanza kuamini kuwa Zitto anaifunika CCM!

..mimi nadhani ni jambo zuri Zitto kuifunika CCM.

..huu ni wakati ambao vyombo vya habari na watu wote wamejielekeza kuangalia nini CCM wanafanya.

..sasa kama ktk mazingira hayo Zitto ameweza kuwafunika basi ni jambo jema sana kwa ACT.

..CDM nao walikuwa active majuzi kwa operation zao za uhamasishaji walizokuwa wakiendesha nchi nzima.

..It wont take long kabla wananchi hawajazoea hizi kampeni za CCM na kuziona ni kitu cha kawaida, then huo ndiyo utakuwa wakati muafaka kwa CDM kuvamia tena huku mitaani.

..Kwenye siasa TIMING ni kitu muhimu sana.
 
Kuna watu hawataki kusikia ukweli kuhusu zitto,hasa chadema,ila zitto ni zaidi ya umjuavyo,ni mwanasiasa makini na anayejiamini,tunaanza nziara kesho,mnyika tangulia kama kawaida yako
Mkuu ziara CHADEMA wanafanya kila siku si za kuvizia kama hizo zenu bila Ayatullah hakuna ziara.Hicho chama cha mtu mmoja hakifiki kokote.
 
hilo azimio la tabora linasemaje? je zile milioni 700 za kutoka kwa lowasa kwenda act zilishatoka?
 
Yaani UKAWA hawajui hata wanapigana na nani

Kuna mahali UKAWA wanapigana na mtu? Unamaanisha CCM na ACT wote wanapigana na UKAWA kiasi kwamba UKAWA ameshindwa kuamua ngumi ya kwanza itue kwa nani?
 
Hivi zoezi la viongozi wa Act kutangaza mali zao liliingia wapi? Ndio tutaweza kupima kama hilo azimio Lina maana ama ni ujinga tu......Mali za Mwigamba , Mtemelwa , Kitila, Msando , Mgwira ........

kwani ww hujaona kwenye wepsite ya chama ? watu wametangaza mali zao

ingia www.act.or.tz
 
Kwa mda nilioiona hii thread ingalikuwa mwezi ule ungekuta page ya kumi saizi ma ccm yamejitenga baada ya wagombea wao kuanza harakati na pia Zitto kuonekana akiinyemelea Tabora ambayo 100 asilimia ya wabunge ni CCM , sasa ndio ACT imebaki ACT nlisema CCM wanataimingi sasa ndio atajua wanachma wake halisi ni kina nani
 
Back
Top Bottom