Mkuu wala Akili haitachoka na wala usitegemee hilo kwa sababu mimi naamini Tanzania bora ni ile itakayo weza kuimarisha muungano. Tena ikiwezekana hadi EAC iwe nchi moja kama zilivyo USA au Canada. Tuwe na serikali moja kubwa na nyinginezo ndogo na hakuna mambo yasokuwa ya Muungano. Nguvu ya nchi hizo imetokana na muungano wao ambao kwa ukubwa tu sisi EAC tujumuishe wote pamoja ni sawa na states mbili tu za Marekani au Canada.Mzee Mkandara akili inachoka
Kama wao wameweza unganisha nchi zaidi ya 12 kwa Canada na Marekani zaidi ya 50 sisi hizi 2 tunalilia kugawana umaskini kama tunavyokumbatia umaskini kugawama urithi wa mali waloacha wazazi wetu. Na lini ulosikia watu wakitajirika kwa kugawana mirathi kama sio mmoja kudhulumu wengine ama wote wameumbuka!
Siwezi kuungana na mawazo ya kuigawa Tanzania kwa maslahi ya wachache. Katiba bora imegeuzwa kuwa mpango wa wachache kugawanamadaraka. Hizi fikra za kina Jussa na Lissu wabakie nazo na tunawaachia UKAWA maana Chadema ndio hivyo. Nawafuata watu kama Nyerere, Abdulrahman Babu, Ghadaffi, Nkurumah na kadhalika.