Zitto Kabwe asimulia alichokutana nacho hospitalini mkewe akijifungua

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,342
2,000
Usiku wa kuamkia tarehe 26 Desemba 2016 mke wangu alipata uchungu wa uzazi. Nikampeleka hospitali moja hapa Masaki. Hakuweza kujifungua siku hiyo bali tulikaa hospitali mpaka tarehe 27 Desemba, saa moja dk 45 asubuhi alipojifungua mtoto wetu wa kike Josina- Umm Kulthum.

Masaa ya jioni tarehe 26/12/2016 nikiwa napiga soga na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa na shemeji yangu mmoja mbele ya hospitali, wakaja watu 3. Watu hao mmoja mwanaume na wengine wanawake walikuwa na mtoto mdogo. Mwanaume huyu alikuwa amembeba mtoto akiwa na taharuki kubwa na mama mmoja mtu mzima na mwengine wa umri wa miaka 30 hivi walikuwa wakilia. Wakaingia hospitalini kwa kasi. Tukaambiana pale kuwa huyu binti atakuwa mahututi. Tukaendelea na soga. Mara kina mama wale wakatoka, wanapiga mayowe "mtoto hana damu" na ilitakiwa damu ya haraka Group A+.

Wenzangu hawakuwa group hilo au group linaloweza kupeana damu. Mimi sikuwa najua/kukumbuka Group langu. Nikawaambia kina mama wale kuwa ngoja nijaribu kupima group langu na pia kuona kama damu yangu inaweza kuokoa maisha ya mtoto yule malaika za mungu. Nikaingia maabara nikapima. Baada ya dakika 10 Hivi nikaitwa kuambiwa damu yangu ni group sawa na mtoto yule na kwamba ni safi inafaa wanitoe muda ule ule ili kumuwahi mtoto. Nikatoa nusu lita muda ule ule. Baadaye nikaenda kumjulia Hali mtoto yule, nikaambiwa anaitwa Rahma. Ana umri wa miaka 2 na miezi 3. Nikawatakia kheri wazazi wake ( kumbe yule mwanaume ndie baba wa mtoto na msichana mama yake. Yule bi mkubwa nadhani ni bibi ya Rahma, sina hakika).

Leo asubuhi, 27 Desemba 2016 baada ya mke wangu kujifungua, nikaenda kumwona Rahma wodini. Nimemkuta anaendelea vizuri, anakula na kuongea. Mola ampe umri mrefu zaidi yeye na wazazi wake. Amwondolee maradhi na akue katika maadili mema ya dini. Namshukuru mola kuniweka mahala sahihi na wakati sahihi hivyo kuweza kufanya ibada hii ya kumsaidia binti Rahma. Lau kama sikuwa nimechagua jina la binti yangu mapema, ningemwita Rahma. Hata hivyo inshallah Rahma atakuwa dada yake Umm Kulthum-Josina. Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika.

Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka Wiki ya kwanza ya Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote. Pia nimepata somo kubwa kwamba ni muhimu Sana kujua Group lako la damu na kuwa na kumbukumbu nalo kwani inaokoa muda pindi damu ikitakiwa kwa haraka. Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ' blood group ' yangu. Nawasihi Watanzania wenzangu na mie msiojua blood group, mjue sasa kwani hatujui Siku wala Saa.

*****Heri ya mwaka mpya 2017 *****

Zitto Kabwe
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,763
2,000
Umefanya jambo kubwa la kheri inshallah umepaya twawabu na heri yako akhera! Hongera kwa kupata mtoto pia bwana wewe mnafiki wa kiwango cha juu kutokea hapa nchini......ZZK ni fitna na mnafiki mchumia tumbo! Hilo tu mengine unafanya uzuri sana

Usiku wa kuamkia tarehe 26 Desemba 2016 mke wangu alipata uchungu wa uzazi. Nikampeleka hospitali moja hapa Masaki. Hakuweza kujifungua siku hiyo bali tulikaa hospitali mpaka tarehe 27 Desemba, saa moja dk 45 asubuhi alipojifungua mtoto wetu wa kike Josina- Umm Kulthum.

Masaa ya jioni tarehe 26/12/2016 nikiwa napiga soga na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa na shemeji yangu mmoja mbele ya hospitali, wakaja watu 3. Watu hao mmoja mwanaume na wengine wanawake walikuwa na mtoto mdogo. Mwanaume huyu alikuwa amembeba mtoto akiwa na taharuki kubwa na mama mmoja mtu mzima na mwengine wa umri wa miaka 30 hivi walikuwa wakilia. Wakaingia hospitalini kwa kasi. Tukaambiana pale kuwa huyu binti atakuwa mahututi. Tukaendelea na soga. Mara kina mama wale wakatoka, wanapiga mayowe "mtoto hana damu" na ilitakiwa damu ya haraka Group A+.

Wenzangu hawakuwa group hilo au group linaloweza kupeana damu. Mimi sikuwa najua/kukumbuka Group langu. Nikawaambia kina mama wale kuwa ngoja nijaribu kupima group langu na pia kuona kama damu yangu inaweza kuokoa maisha ya mtoto yule malaika za mungu. Nikaingia maabara nikapima. Baada ya dakika 10 Hivi nikaitwa kuambiwa damu yangu ni group sawa na mtoto yule na kwamba ni safi inafaa wanitoe muda ule ule ili kumuwahi mtoto. Nikatoa nusu lita muda ule ule. Baadaye nikaenda kumjulia Hali mtoto yule, nikaambiwa anaitwa Rahma. Ana umri wa miaka 2 na miezi 3. Nikawatakia kheri wazazi wake ( kumbe yule mwanaume ndie baba wa mtoto na msichana mama yake. Yule bi mkubwa nadhani ni bibi ya Rahma, sina hakika).

Leo asubuhi, 27 Desemba 2016 baada ya mke wangu kujifungua, nikaenda kumwona Rahma wodini. Nimemkuta anaendelea vizuri, anakula na kuongea. Mola ampe umri mrefu zaidi yeye na wazazi wake. Amwondolee maradhi na akue katika maadili mema ya dini. Namshukuru mola kuniweka mahala sahihi na wakati sahihi hivyo kuweza kufanya ibada hii ya kumsaidia binti Rahma. Lau kama sikuwa nimechagua jina la binti yangu mapema, ningemwita Rahma. Hata hivyo inshallah Rahma atakuwa dada yake Umm Kulthum-Josina. Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika.

Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka Wiki ya kwanza ya Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote. Pia nimepata somo kubwa kwamba ni muhimu Sana kujua Group lako la damu na kuwa na kumbukumbu nalo kwani inaokoa muda pindi damu ikitakiwa kwa haraka. Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ' blood group ' yangu. Nawasihi Watanzania wenzangu na mie msiojua blood group, mjue sasa kwani hatujui Siku wala Saa.*****Heri ya mwaka mpya 2017 *****

Zitto Kabwe

Chanzo:Mwananchi
 
lebara

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
647
1,000
Mungu akupe rehema zake ndugu zito hapa nilipo sijui kundi langu la damu
 
2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,032
2,000
Umefanya jambo kubwa la kheri inshallah umepaya twawabu na heri yako akhera! Hongera kwa kupata mtoto pia bwana wewe mnafiki wa kiwango cha juu kutokea hapa nchini......ZZK ni fitna na mnafiki mchumia tumbo! Hilo tu mengine unafanya uzuri sana
kwanini basi usingesubiri post inayohusiana na fitna ukayasema hayo ya ubaya wake!
muungwana sifa yake ni kumtakia kheri mwenzie na pale penye mapungufu husema kwa staha ili azingatie stara ya mwenzie! we unajuaje kama zzk katubu huo unafiki? n
naamini ktk tafsiri zako za uchumia tumbo na unafiki nomba tujiulize haya....!
ni nani asiye na dhambi ya uchumiaji tumbo hapa nchini? nani si mnafiki ktk wanasiasa mlete tumuone!
 
Jack Beur

JF-Expert Member
Feb 26, 2010
221
250
Sidhani kama ni protocol kutoa damu muda huo huo na kuruhusiwa kumpatia mhitaji, kuna wagonjwa ambayo hayawez kuonekana kwenye vipimo vya maabara muda huo huo labda kama uko kwenye highly equipped health facility, so sidhan kama story ya mh ni kweli , kama ni kweli bas ni hatar kwa afya za wagonjwa.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,980

8-12 hours
 
NAHINGA

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
1,019
1,500
Sidhani kama ni protocol kutoa damu muda huo huo na kuruhusiwa kumpatia mhitaji, kuna wagonjwa ambayo hayawez kuonekana kwenye vipimo vya maabara muda huo huo labda kama uko kwenye highly equipped health facility, so sidhan kama story ya mh ni kweli , kama ni kweli bas ni hatar kwa afya za wagonjwa.
hatari kabisa mkuu...nimesoma hii habari nilisismka mwili,,nyakati za kupewa au kutoa damu na kuiweka haraka haraka bila vipimo vya kina umepita...Hapa tujifunze kuwa hatufuati taratibu..
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,863
2,000
Ufipa wako bize kutafuta uhuru wa kutukana matusi mitandaoni na kuuza chama, badala ya kutatua shida za wananchi kama alivyofanya mh Zito.

Hakika Zito ni kiongozi makini.
Samahani mkuu, kuuliza sio dhambi. Hivi wewe ulishawahi kupata matatizo ya akili siku za nyuma? Kama ni ndio rudi kwa check up itakusaidia kukuweka sawa.
Nisamehe lakini, nimejitolea tuu kukusaidia maana ugonjwa ni ugonjwa tuu.
 
Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
521
500
Leo December 27 2016 mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe na mke wake wamepata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Josina – Umm Kulthum.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa facebook amesimulia alichokutana nacho hospitalini saa chache kabla ya mke wake kujifungua, haya ni maneno yake….

Usiku wa kuamkia tarehe 26 Desemba 2016 mke wangu alipata uchungu wa uzazi. Nikampeleka hospitali moja hapa Masaki. Hakuweza kujifungua siku hiyo bali tulikaa hospitali mpaka tarehe 27 Desemba, saa moja dk 45 asubuhi alipojifungua mtoto wetu wa kike Josina- Umm Kulthum.

Masaa ya jioni tarehe 26/12/2016 nikiwa napiga soga na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa na shemeji yangu mmoja mbele ya hospitali, wakaja watu 3. Watu hao mmoja mwanaume na wengine wanawake walikuwa na mtoto mdogo.

Mwanaume huyu alikuwa amembeba mtoto akiwa na taharuki kubwa na mama mmoja mtu mzima na mwingine wa umri wa miaka 30 hivi walikuwa wakilia. Wakaingia hospitalini kwa kasi. Tukaambiana pale kuwa huyu binti atakuwa mahututi. Tukaendelea na soga.

Mara kina mama wale wakatoka, wanapiga mayowe “mtoto hana damu” na ilitakiwa damu ya haraka Group A+. Wenzangu hawakuwa group hilo au group linaloweza kupeana damu. Mimi sikuwa najua/kukumbuka Group langu.

Nikawaambia kina mama wale kuwa ngoja nijaribu kupima group langu na pia kuona kama damu yangu inaweza kuokoa maisha ya mtoto yule malaika za mungu. Nikaingia maabara nikapima. Baada ya dakika 10 Hivi nikaitwa kuambiwa damu yangu ni group sawa na mtoto yule na kwamba ni safi inafaa wanitoe muda ule ule ili kumuwahi mtoto. Nikatoa nusu lita muda ule ule.

Baadaye nikaenda kumjulia Hali mtoto yule, nikaambiwa anaitwa Rahma. Ana umri wa miaka 2 na miezi 3. Nikawatakia kheri wazazi wake ( kumbe yule mwanaume ndie baba wa mtoto na msichana mama yake. Yule bi mkubwa nadhani ni bibi ya Rahma, sina hakika).

Leo asubuhi baada ya mke wangu kujifungua, nikaenda kumwona Rahma wodini. Nimemkuta anaendelea vizuri, anakula na kuongea. Mola ampe umri mrefu zaidi yeye na wazazi wake. Amwondolee maradhi na akue katika maadili mema ya dini.

Namshukuru mola kuniweka mahala sahihi na wakati sahihi hivyo kuweza kufanya ibada hii ya kumsaidia binti Rahma. Lau kama sikuwa nimechagua jina la binti yangu mapema, ningemwita Rahma. Hata hivyo inshallah Rahma atakuwa dada yake Umm Kulthum-Josina.

Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika.

Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka Wiki ya kwanza ya Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote.

Aidha nimepata somo kubwa kwamba ni muhimu Sana kujua Group lako la damu na kuwa na kumbukumbu nalo kwani inaokoa muda pindi damu ikitakiwa kwa haraka. Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ‘ blood group ‘ yangu. Nawasihi Watanzania wenzangu na mie msiojua blood group, mjue sasa kwani hatujui Siku wala Saa.

MUNGU MWENYEZI AKUBARIKI SANA MHESHIMIWA MBUNGE ZITO KABWE.
 
Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
521
500
Jana December 27 2016 mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe na mke wake walipata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Josina – Umm Kulthum.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom