Zitto Kabwe asimulia alichokutana nacho hospitalini mkewe akijifungua

Mi nilifikiri kitu gani sijui.... Bwanamdogo kaishiwa Sera ameanza tafuta mileage kwa vitu vya kitoto!
 
Sound good lakini kaka Zitto atambue kuwa, pamoja na mke wake kwenda kujifungulia kwenye hospitali ya hadhi ya juu.. Nadhani ni Sali int.

Bado walalahoi wanaowalipa marupurupu yote hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu, achilia mbali ukosefu wa dawa na miundombinu chakavu na finyu , bado ukosefu wa wataalamu wabobezi kama zilivyo hospital nyingine hapa mjini.

Suala la damu ni jambo dogo sana kulinganisha na huo mlima anaokutana nao mtanzana wa kawaida(80%of our popn)
 
Acheni ushabiki wa kijinga!
yaani damu imeokoa maisha ya mtu then unakurupuka tu na kusema ni jambo dogo?
tutangulize uhai mbele, panapo stahili pongezi na tupongeze.
Zitto katimiza wajibu wake
 
Leo December 27 2016 mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe na mke wake wamepata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Josina – Umm Kulthum.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa facebook amesimulia alichokutana nacho hospitalini saa chache kabla ya mke wake kujifungua, haya ni maneno yake….

Usiku wa kuamkia tarehe 26 Desemba 2016 mke wangu alipata uchungu wa uzazi. Nikampeleka hospitali moja hapa Masaki. Hakuweza kujifungua siku hiyo bali tulikaa hospitali mpaka tarehe 27 Desemba, saa moja dk 45 asubuhi alipojifungua mtoto wetu wa kike Josina- Umm Kulthum.

Masaa ya jioni tarehe 26/12/2016 nikiwa napiga soga na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa na shemeji yangu mmoja mbele ya hospitali, wakaja watu 3. Watu hao mmoja mwanaume na wengine wanawake walikuwa na mtoto mdogo.

Mwanaume huyu alikuwa amembeba mtoto akiwa na taharuki kubwa na mama mmoja mtu mzima na mwingine wa umri wa miaka 30 hivi walikuwa wakilia. Wakaingia hospitalini kwa kasi. Tukaambiana pale kuwa huyu binti atakuwa mahututi. Tukaendelea na soga.

Mara kina mama wale wakatoka, wanapiga mayowe “mtoto hana damu” na ilitakiwa damu ya haraka Group A+. Wenzangu hawakuwa group hilo au group linaloweza kupeana damu. Mimi sikuwa najua/kukumbuka Group langu.

Nikawaambia kina mama wale kuwa ngoja nijaribu kupima group langu na pia kuona kama damu yangu inaweza kuokoa maisha ya mtoto yule malaika za mungu. Nikaingia maabara nikapima. Baada ya dakika 10 Hivi nikaitwa kuambiwa damu yangu ni group sawa na mtoto yule na kwamba ni safi inafaa wanitoe muda ule ule ili kumuwahi mtoto. Nikatoa nusu lita muda ule ule.

Baadaye nikaenda kumjulia Hali mtoto yule, nikaambiwa anaitwa Rahma. Ana umri wa miaka 2 na miezi 3. Nikawatakia kheri wazazi wake ( kumbe yule mwanaume ndie baba wa mtoto na msichana mama yake. Yule bi mkubwa nadhani ni bibi ya Rahma, sina hakika).

Leo asubuhi baada ya mke wangu kujifungua, nikaenda kumwona Rahma wodini. Nimemkuta anaendelea vizuri, anakula na kuongea. Mola ampe umri mrefu zaidi yeye na wazazi wake. Amwondolee maradhi na akue katika maadili mema ya dini.

Namshukuru mola kuniweka mahala sahihi na wakati sahihi hivyo kuweza kufanya ibada hii ya kumsaidia binti Rahma. Lau kama sikuwa nimechagua jina la binti yangu mapema, ningemwita Rahma. Hata hivyo inshallah Rahma atakuwa dada yake Umm Kulthum-Josina.

Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika.

Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka Wiki ya kwanza ya Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote.

Aidha nimepata somo kubwa kwamba ni muhimu Sana kujua Group lako la damu na kuwa na kumbukumbu nalo kwani inaokoa muda pindi damu ikitakiwa kwa haraka. Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ‘ blood group ‘ yangu. Nawasihi Watanzania wenzangu na mie msiojua blood group, mjue sasa kwani hatujui Siku wala Saa.

MUNGU MWENYEZI AKUBARIKI SANA MHESHIMIWA MBUNGE ZITO KABWE.
Hospitali zote za Serikali zina taratibu ktk Huduma ya Damu salama kupitia Benki ya Damu.

Nadhani kwa Masaki hiyo itakuwa Private hospital ambayo sijui utaratibu wao kuhusu huduma ya Damu salama kwa wagonjwa

Hongera Mh Zito kwa kupata binti Mungu ampe mema ya nchi.
 
That was such an Angelic act Zito, U are a very good man be blessed! Hongera sana Kwa mtoto, Jina Ulilonipa Limenikumbusha yule Dada Mpigania Uhuru wa Frelimo nadhani alikuwa pia ni Mke wa kwanza wa Samora Machel Kabla Josina hajafariki ghafla. Na pia waliishi pamoja Tanzania kwa Muda

josina_marching.jpg

Hizi picha alikuwa Nachingwea, Inasikitisha huyu Dada alikufa akiwa na Miaka 25, Alikufa baada ya Kugundulika ana Kansa ya Ini, Mwalimu Nyerere na Samora walimpeleka Urusi, Alishariwa asifanye kazi ngumu. Lakini akaenda Msumbiji kwenye maeneo ambayo Frelimo walikuwa wameyadhika Ili kusaidia maswala ya Jamii na Wabawake. Muda mwingi slitumia miguu kusafiri. Mwezi wa 3 1971 hali yake Ikawa mbaya sana, Akarudi Dar es salaam, Akitambua hatima yake, Akiwa mpakani na Tanzania akatoa bastola yake na kumkabidhi mpiganaji mwenzake akaomba apelekewe Samora ili isaidie kwenye mapigano. Basi akarudi Dar es salaam, Tarehe 5 April Akazidiwa sana Akapelekwa Muhimbili ambako alifariki Tarehe 7 April, Na amezikwa Makaburi ya Kinondoni. Wenye kupenda Historia ya Dada huyu Aliyezaliwa Josina Samora Muthembu 1945-1971 Akiwa na Umri wa Miaka, Mnaweza Kulitembelelea Kaburi lake Kinondoni.
Pia walioana na Samora Machel huko Tunduru na kuzaa Mtoto mmoja na Samora aliyeitwa Samora Junior au Samito.
Hivi sasa Siku ya Wanawake Mozambique ni Tare 7 April Kukumbuka Kifo chake!
 
Kwani kulikua na ulazima wa kusema alicho fanya wengine ukimsaidia mtu inabaki kuwa siri yako
Mimi sioni shida Ni jambo lililomfurahisha kuweza kusimulia tukio lililomtokea, Mbona kuna wanaosimulia kama jinsinwalivyolewa jana. Mbona magazetinyanasimulia Matukio kila siku na hatuoni ni ajabu. Hata Kama ni mimi nimejikuta niko mahali akaja mtoto mgonjwa na anahitaji Damu ikatokea group yangu ni sawa na yake na nikaweza kumpa damu na Kubwa zaidi akapona Ningesimulia Muujiza huo! Sioni kama zitto amefanya Ubaya wowote
 
Hii stori yote ni kiki inatafutwa.

Mosi ni kuipaisha ACT na utaratibu wake wa damu. Kwamba yeye kawekwa sehemu sahihi ili atekeleze sera za ACT. Propaganda.

Pili ni kutuonyesha kuwa yu mzima maana kulikua na vijistori kuhusu huu ugonjwa wa kisasa. Kuna mtu au watu wanarushwa roho hapa.

Hata hivyo hospitali nyingi damu unayojitolea sio hiyo anayopewa mgonjwa. Maana naambiwa damu ina mchakato mwingi sana hadi ifae kutumika.

So km mtu yu salama, damu aliyotolewa huingia benki ya damu ya hospitali husika na kiwango hitajika hutolewa kwenye ambayo ni salama. Kwa hospitali iliyo Masaki nahisi ni ya kisasa sana kukosa benki ya damu. Wenye kujua wataelezea zaidi.

Tatu, kutujuza kuwa kapata mtoto. Wa kike na jina alilompa. Hapa mke anapewa airtime ili ainjoi kuzaa na mheshimiwa sana. Na wanasiasa wasio na watoto wanatandikwa bakora. Huenda mtoto anawekewa mazingira ya uceleb.

Nne, ujitanabaisha kuwa yeye ni mtu wa msaada. Kutoa tu damu kajimilikisha hadi huyo Rahma. Sasa ni dada yake Ummy.

Kuhusu wao ACT kujitolea damu kila Mei, vipi kuhusu wanachama wao ambao ni Mashahidi ya Jehova?
 
Ungekaa kimya tu.....sasa tofauti yake na wewe ni ipi?

Hata wewe tutatafsiri kuwa unatafuta kiki.
 
Muhimu kwa Zitto kwenye hii heroic tale is how he became 'have a go hero' when there was no one else to save the day; not to discredit is humane act.

Lakini kama mwanasiasa mwenye namba ya simu ya Kigangwala kwanini asingemtangiwa na kumwambia maajabu aliyojionea hospitali iliyo sajiliwa kutoa huduma ya afya aina 'blood bank' maana kama siyo yeye huyo Rahma uhai wake si ungekuwa tete sasa hivi na wangapi washapoteza maisha kwa sababu ya uzembe wa hiyo hospitali kushindwa kufanya balancing za flow zao za blood bank; if you ask me jamaa wanatakiwa watandikwe faini ya nguvu kwanza kabla ya mengine huu ni upuuzi usio kubalika kabisa.

Haya muhimu 'oh-no' awayataki wao wanataka kazi rahisi za kwenda kuangaika na kina Dr Mwaka na kupiga picha wamevaa track suits wanakimbia kupambana sijui na magonjwa yanayo epukika what a useless lot.
 
Mi nilifikiri kitu gani sijui.... Bwanamdogo kaishiwa Sera ameanza tafuta mileage kwa vitu vya kitoto!
ondoa siasa wewe, hapo ndo mnaharibu hii nchi, nyie kila kitu mumeweka siasa, miaka 50 bado tu mnajiita watoto, au ni senescence period, akiki inarudi kuwa ya kitoto
 
Mimi sioni shida Ni jambo lililomfurahisha kuweza kusimulia tukio lililomtokea, Mbona kuna wanaosimulia kama jinsinwalivyolewa jana. Mbona magazetinyanasimulia Matukio kila siku na hatuoni ni ajabu. Hata Kama ni mimi nimejikuta niko mahali akaja mtoto mgonjwa na anahitaji Damu ikatokea group yangu ni sawa na yake na nikaweza kumpa damu na Kubwa zaidi akapona Ningesimulia Muujiza huo! Sioni kama zitto amefanya Ubaya wowote
ndugu, tatizo la hawa wenzetu siasa wameweka mbele kuliko utu, mbona wao wanatuma mipicha na nguobzao za vyama ati wapo bukoba kukagua majengo yalioathiriwa na tetemeko?
 
Back
Top Bottom