AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Tarehe 18 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg.Humphrey Polepole alifanya mkutano na waandishi wa habari kufafanua uzushi na uongo uliofanywa na Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini aliyedai kwamba kuna upotevu wa Trillion 1.5 uliogunduliwa katika ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali CAG.
Ndg Polepole amekokotoa kitaalamu na kwa kutumia kanuni za kiuhasibu zinazotambulika kimataifa, hesabu zilizopo katika ripoti na ukweli ukagundulika kwamba hakuna upotevu wa Trillion 1.5 kama Ndugu Zitto alivyodanganya na kupotosha umma.
Zitto ambaya kitaaluma ni mchumi ameshindwa kukokotoa hesabu hizi ndogo za kidato cha kwanza.Ameshindwa kujua kwamba huwezi kukokotoa hesabu wakati wa ukaguzi kwa kutumia mapato ghafi badala ya mapato halisi.
JINSI ZITTO ASIVYOJUA HESABU.
Katika hesabu za Serikali kuna kitu kinaitwa mapato ghafi ambapo mapato hayo ghafi jumla yake yalikua ni Shillingi Trillion 25.3.
Sasa Zitto anasema ukichukua hayo mapato ghafi ya Trilion 25.3 ukitoa fedha ambayo CAG aliikuta kipindi anafanya ukaguzi ambayo ilikua ni Trilion 23.79 unapata Trillion 1.5.
Pesa ambayo Zitto anadai imepotea .
Huu ni uongo na upoyoshaji mkubwa Hiki ni kichekesho kwa mchumi kama Zitto kutojua hesabu hizi za kidato cha kwanza.
Katika kanuni za mahesabu ya ukaguzi huwezi ukakokotoa kwa kutumia mapato ghafi ni lazima uondoe ili upate mapato halisi kisha hayo ndiyo unayakokotoa na matumizi .
UKWELI WA TRLION.1.5 HUU HAPA.
Mapato ghafi ni Trilion 35.3 ndani ya hiyo pesa kuna pesa za kuwapa Zanzibar ambayo ni Billion 2003 na million 920.
Pesa ya Zanzibar huiwezi kuiweka katika Pesa za Jamhuri ya Muungano.Ni makosa kufanya hivyo.
Lakini pia hayo mapato ghafi yalikua yamejumlisha Huduma ambazo Serikali imezitoa lakini pesa haijangia bado ambazo jumla yake ni Billion 687 na Million 300.
Sasa ili upate makusanyo halisi unachukua mapato ghafi unatoa pesa zilizokusanywa kwa niaba ya Zanzibar lakini pia unatoa fedha tarajiwa .
Ukifanya hesabu hapo unapata jumla ya Trilion 24.4
Sasa hata katika ile Trilion. 23.79 haikua timilifu bali kulikuwepo na fedha yetu ya hati fungani ambayo ilikua bado haijaiva na ilipoiva jumla yake ikawa ni Billion 697 na Million 850.
Ukijumlisha Trillion 23.79 na Billion 697 na Million 850 unapata Trillion 24.4.
HESABU IMEBALANCE! HAKUNA FEDHA ILIYOPOTEA
Kwa hili ni kweli kabisa anastahili kukamatwa na kushtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo.
Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka ya 2015 kifungu cha 16 ( Cybercrimes Act of 2015) kinaeleza kuwa endapo mtu akipatikana na hatia ya kuchapisha taarifa za uongo zinazopotosha au siyo sahihi atatumikia adhabu ya kifungo kisichopungua miezi sita jela.
Zitto Kabwe ametoa taarifa hizo za uongo kupitia katika kurasa zake za mitandao ya Facebook ,Twitter na Instagram. Anastahili kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Zitto Kabwe alishawahi pia kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kusimamia mashirika ya umma (POAC) ndo maana sasa napata majawabu kwa nini mifuko ya hifadhi ya Jamii miaka hiyo ilifanya vibaya sana kumbe ilikua inasimamiwa na mtu zero brain kama Zitto.
Wasalaam,
Augustino Chiwinga.