Zitto Kabwe Anajenga Hoteli ya Kifahari! [Zitto kafafanua]

Status
Not open for further replies.
Mtoa mada anataka mimi nitoe ushahidi kwa tuhuma alizotoa yeye. Mimi nimekwambia sina si tu hotel Bali hata kiwanja Dodoma sina. Yeye mwenye tuhuma atoe ushahidi kwamba hii ni Mali ya Zitto.

Sio tu Dodoma Bali hata Dar huko anakosema athibitishe kwamba nyumba anayosema ni ya Zitto kweli ni ya Zitto.
 
Hii ni ya mbezi kimara

images

Sasa mbona gorofa moja na ni nyumba ya kawaida kuliko maneno uliyo kuwa ukisema!! Mbongo kweli nuksi
 
Mtoa


Mtoa mada anataka mimi nitoe ushahidi kwa tuhuma alizotoa yeye. Mimi nimekwambia sina si tu hotel Bali hata kiwanja Dodoma sina. Yeye mwenye tuhuma atoe ushahidi kwamba hii ni Mali ya Zitto.

Sio tu Dodoma Bali hata Dar huko anakosema athibitishe kwamba nyumba anayosema ni ya Zitto kweli ni ya Zitto.

Watu kama hawa Zitto wapotezee tu wanamalengo binafsi aidha ya kukuchafua au kukupakaza ukwasi usio nao
 
wakuu, taarifa hizi ni za uhakika kabisa, maana mleta habari anaelewa kwa undani ishu nzima...
Kwa zitto hili ni jambo rahisi tu, aeleze wanajamvi kama ni hoteli yake ya kihalali...basi!

hivi ndugu yangu tatizo hapa nini hasa , kwamba zitto hatakiwi kuwa na kitegauchumi cha hoteli ya nyota tano ambacho kitatoa ajira kwa vijana wetu wanaozurura mitaani pamoja na digrii za na kulipa kodi serikalini, tatizo ni nini??. Kama ni kweli basi anastahili kutiwa moyo na kupongezwa
 
Wakuu, taarifa hizi ni za Uhakika kabisa, maana mleta habari anaelewa kwa undani ishu nzima...
Kwa Zitto hili ni jambo rahisi tu, aeleze wanajamvi kama ni hoteli yake ya kihalali...basi!

Hapa mnatisha? Ataogopa kununua hata baiskeli tu ...!
 
Kama ukithibitisha kwamba si tu Nina ghorofa Bali kiwanja huko Mbezi Kimara nitakupa wewe. Ninashangazwa sana na uwezo wa kudanganya wa Watanzania.

Hako kajumba ka Kimara eti nako kako kha!!
 
Zitto mm naamini kabisa atakuwa anajenga, yule ni fisadi mkubwa sana sema watu hawajashtukia kwa kuwa yupo cdm. cku za mbele mambo yote yatakuwa wazi watu mtashangaa
 
Zitto anajenga ghorofa bila tone la shaka!

Eneo la Kisasa lipo nje kidogo ya mji ukiwa unaingia Dodoma, jirani kabisa na Saint Gaspar Hoteli!...Au kwa wanaojua shule ya King Martin Luther!..
Utabisha sana laki ni huo ndio ukweli..politicians ndio zenu hizi!
 
Ndio maana wazee wetu walipojaribu kuezeka nyumba zao kwa bati walirogwa sana.........WaTz sometimes tuna roho mbaya sana
 
Kale ka jengo ka gorofa moja ndiyo nyota tano? Nilipita pale mwaka jana mwezi wa nane wakanionyesha gorofa moja pale kisasa sasa hii ndiyo hoteli ya kifahali? Anyway kama ndio hiyo mleta mada ana agenda yake.
 
Kwa sasa hoteli hii imefikia ghorofa ya 3, na inakwenda kwa kasi!....

Tunaandaa picha kamili za nyumba hiyo ili wabishi muone!

Na siku moja tutamphotoa akiwa ameenda kuangalia maendeleo! Labda amsusie nduguye!
 
Watu kama hawa Zitto wapotezee tu wanamalengo binafsi aidha ya kukuchafua au kukupakaza ukwasi usio nao

Halafu wakirudi uswahilini wanamwaga mastory kwa washikaji, leo nimempelekesha Zitto huko JF mpaka amenikoma. Kusema kweli, kuna baadhi ya watu wameanza kuliharibu hili jukwaa. Kuna aliyekuja bila ushahidi kuwa sijui Kafulila ana degree ya uongo. Mwingine kaja na gia eti Aggrey Mwanri amesema atagombea urais. Pia yupo anayesema Magufuli alikuwa hataki daraja la Kigamboni lijengwe. Haya yote yanaandikwa bila ushahidi au hata explanation yoyote. Full usanii.
 
Wanajamvi,

Nimepigiwa simu na Ndugu yangu anayeishi Dodoma mjini akinihabarisha kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe anajenga Hoteli kubwa sana ya Nyota 5 Mjini Dodoma, eneo liitwalo KISASA.

Hili ni jambo jema na la maendeleo sana, lakini Je Zitto, hili jambo ni kweli?
Umekuwa unapinga hata kuwa na magari ya kifahari, huku ukisema kuwa hushabikii UTAJIRI, je fedha za kupandisha jengo kubwa na la kifahari kama hilo ni hizihizi za posho zenu, au umekopa benki, au umepewa na mfadhili, au una vyanzo vingine vilivyofichama?

Tafadhali sana Zitto, njoo ujibu kwa kauli yako mwenyewe!

Nawasilisha!

umefanya vizuri pia kuweka possible sources za funds zake, hususani hapo kwenye red.
siku hizi hata messenger kwenye hizi multinationals (kama barrick, etc) ana uwezo wa kukopa bank akajenga au kununua akipendacho!
 
Wakati mwingine uongo na uzushi wa kipuuzi Kama huu ukiachwa kuna watakaoamini. Sio tu kujenga Hotel, sina hata kiwanja Dodoma. Sitegemei kuwa na kiwanja Dodoma wala kujenga Dodoma.

Nimezushiwa mengi sana


1. Nina nyumba Masaki

2. Nina 900m StanBic

3. Nina kiwanda cha kokotoNa mengine mengi sana.

Yote hayo sio ya kweli na kuna watu wanayaamini.

1. Sina biashara yeyote hapa Tanzania

2. Sina nyumba yeyote Dar. Nina shamba la Ekari tatu tu Mbutu na halijaendelezwa toka mwaka 2004.

3. Ninaishi flats za kupanga Tabata4. Sina na wala sijwahi kuwa natamaa ya utajiri katika maisha yangu. Property isn't my thing kabisa.

JF Mtu akileta accusations dhidi ya mtu mwingine tafadhali aje na ushahidi wa mfano picha ya nyumba, ushahidi wa umiliki ambao ni rahisi sana kupata CDA kwa DODOMA au Wizara ya Ardhi.

Tuache umbeya tuseme kweli. Sikatai Kusemwa kwa ya kweli. Ninajifunza sana kwa critics za ukweli. Lakini uzushi Kama huu unaumiza

Kila la kheri


Hakika kama aliyejibu hapo ni Zitto tukitumia kanuni ya logistic kutafuta ukweli dhidi ya kauri hiyo ambayo dhahiri kwa kuzingatia sifa na umuhimu wa Kijana Zitto kwenye siasa zetu za sasa kama ungeniambia kutengeneza assumption ya accusation hiyo ningesema ni true.

Vigezo ni kama ifutavyo nikitumia Red kama indicator kujustfy maelezo yako
1:Umejibu uzushi wa kipuuzi, dhahili kama ni face to face na mtu mwonekano wako utakuwa umekasirika.Na kwa mtu wa kariba yako ambae umeshakutana na mambo mengi ambayo umesingiziwa na hakika ukawa innocent [Chukulia ujio wa chati yako Bungeni] ukuonyesha woga wala kukasirika kwa kuwa ndani ya moyo wako ni dhahili ulikuwa dhahili sahihi na usafi wa moyo hivyo ukuwa na jaka moyo lolote na ukweli huo kizungu tunasema ukuwa guilt conscious kama ambavyo,unalo kwa sasa ndio maana unajibu ukiwa na hasira kwa mujibu wa maandishi haya labda ukanushe kuwa hiyo hapo juu sio Identity yako ndani ya JF.

Zitto ni msomi mzuri na kiswahili kwa kijana yoyote toka KG hasa mitaa yote ambayo wana ujiji wanakujua na pia kiswahili kwao hakina tofauti na kiswahili cha wanabagamoyo au kariakoo Dar es Salaam na unajua walikufunza kiswahili fasaha kwa kuwa wanachotafautina wana ujiji na wanakarikaoo ni lafudhi,kwani wakati wanaujiji ungependa kuwasikliza wanavyozungumza, wanakarikaoo wanaboa.Nimetumia kuyaeleza hapo juu ili usije sema ujui kutumia maneno ya kiswahili na kwamba mtu akitamka neno mpuuzi au upuuzi uwa tunamppiama kuwa yuko kwenye aina gani ya mood.

Zitto kuna sababu gani ya wewe kukasilika kwa jambo ambalo wewe alikuhusu japo umetajwa na wewe unajijua dhahili wewe ni msafi na hata kama una nyumba si haramu wewe kumiliki nyumba na hata kama u tajiri si halamu wewe kuwa tajiri.U haramu wa nyumba yako au uatajiri wako utakuwa valued kwa jinsi nyumba au utajili ulivyopatikan.Hivyo nashanga kuna sababu gani ya wewe kukasirika.Na Je kama unakasirika nini kinachokukasirisha?

2:Kuna watakaoamini.
Hakika ili nalo Zitto unanipa assumption nyingine kuwa ni vipi wewe uamini watu wataamini mambo ya kuambiwa na jamii forum yakiwa ya uongo wakati unajua dhahili wewe na mtoa habari hii, wewe ni public figure hivyo sisi tunakuamini wewe zaidi kuliko tunavyomwamini mtoa habari.Hivi mpaka wanakigoma wanakupa tiketi ya kuwawakilisha bungeni mwetu imani yao kwako imegeuka lini wadanganyike leo kuwa wewe na tatizo tajwa.Sipati picha ebu nisaidie kuniaminisha iweje niamini maneno au habari hii au vinginevyo kunacha ziada lejea hapo juu.Kwa picha nyepesi ni sawa na kusema leo hii uambiwe Mwalimu Nyerere alimilki hotel ya Kitalii Uswis au Zimbabwe hakika,Je Zitto kwa ujumbe huo hakika Watanzania wataamini.

3:Sitegemei kuwa na kiwanja
Ili nalo Ndugu Zitto ni ishara ya kuhamaki,ambako sipati picha kwa uzoefu wangu wa kukuona kwenye hoja motomoto za kitaifa imekuwaje leo kwa hoja ndogo sana kama hii umekurupuka na majibu yenye kasoro lukuki kama hizi.Ebu twambie siku tukisikia umemilki kibanda cha chumba kimoja na sebure au shamba la eka moja lenye vitalu viwili vya zabibu tujiulize imekuaje kwa imppossible tobecome possible kwa zitto.Hili nalo watanzania wenye macho yao watakusubilia kwa macho yote kwa kuwa umeshawaambia na watakuwa macho kuliko ambavyo ukutegemea kwa kuwa umesema wewe mwenyewe.

4: Nimezushiwa mengi sana
Zitto unajua sana madhara ya kuzushiwa hakika na kiongzoi mwadilifu uwa anajua dhahili uwezo wa taarifa ambazo si za kweli na hivyo ni dhahili atachukua hatua.Sijua kama ni upeo wangu mdogo wa kufuatilia habari sikumbuki kuona kwa nafasi yako kubwa kama Model kwa baadhi ya vijana na Public Figure umeita au umepeleka malalamiko yako kwenye vyombo vyetu vya dola au kuitisha vyombo vya habari na kukanusha tuhuma hizo ambazo umezitaja mwenyewe hapo juu.Utanisaidia kunikumbusha lini umeongea na vyombo vya habari kuhusiana na tuhuma ulizozitaja hapo juu.

5:Sina na wala sijwahi kuwa natamaa ya utajiri.
Siamini kwa level yako ya elimu na upeo wako wa exposure unaamini kuwa utajlli ni Tamaa.Kwa nafasi yako au kwa level yako kama unaamini utajli unapatikana kwa tamaa basi, kuna somethin wrong somewhere!!.Mimi kwa upeo wangu mimi Utajili kwa uelewa wangu na kwa mujibu wa wanataaluma utajili sio dhambi hivyo sio taama.Kwa kuwa chochote kinachopatikana kwa njia ya tamaa ndio dhambi.Ni vyema ukafuta usemi wako kwa kuwa kama kiongozi wa Wananchi unaamin utajili unapatokana kwa njia ya tamaa,basi wananchi wako wa Kigoma ambao wamepata utajili wao kwa njia halali na wengine wako njiani kutafuta utajili kwa njia halali utakuwa umewaweka wapi?

6: Property isn't my thing kabisa
A property is a building and the land belonging to it, sijui hapa unamaanisha nini?kuwa hakika maisha yako yote utamilki Nyumba au Ardhi kwa kuwa kwa usemi wako hapo juu kwa lugha nyepesi Nyumba na Ardhi sio vitu vinakaa chumba au karibu yako wewe.Yani kama ingekuwa ni uchaguzi wa chaguo lako la mke yupi wa kuoa kwako kati ya mrefu au mfupi na watu wakakupa option ya uchaguzi wako ukatwambia Mfupi isn't your type hatutegemei kukukuta ukiwa n aina hiyo ya mwanamke ukatwambia kuwa huyo ni mkeo tukukubalie vinginevyo tutakuona unamatatizo kwa kuwa ulishatuthibitishia kuwa sio choice yako.Point hii imekaaje Zitto?

7: Mfano picha ya nyumba,
Kuna Nyumba picha imeletwa hapa JF hapo juu wewe ujasema chochote kuhusiana na Nyumba hiyo?

8: Tuache umbeya tuseme kweli.
Hakika kiwango chako cha ufahamu, uelewa na kujulikana kwenye umma matumizi ya lugha ya maneno,ambayo kwa hadhi na wajibu wako kwa umma ni mapungufu ambayo yanaonyesha kwa sasa wewe sio Zitto wa zama zile mwenye kuzungumza kwa lugha ya staha na yenye kuwakilisha sauti za wengi.Napata shida kuamni kuwa story hii hapo juu imeandikwa kukanushwa na wewe. Vinginevyo utakuwa umekasirika na je kilichokukasirisha nini au ndio tupigie mstari kuwa UKWELI UNAAUMA KUMBUKA HASIRA HASARA MASECHU ANASEMA.


 
Nakusifu Zitto kwa ujasiri wako wa kuface accusations jamvini na au hata kwenye public media.

Si wa kutokomea mitini.
 
KISASA - Dodoma Mjini?

Labda kama Dodoma Mjini sipafahamu vizuri!!!

Kisasa ni nje kidogo ya Dodoma Mjini,.Af hotel yenyewe haiwezi kuwa na hadhi ya nyota tano, ni ghorofa flani la kawaida,.Mi mwenyewe kuna mtu alinionyesha kipindi np Dodoma, ila sina uhakika kama ni kweli ni la Zitto au la?!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom