Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema atafanya kila aliwezalo kuhakikisha mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, anashinda nafasi hiyo.
Uchaguzi Mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Oktoba 27, ukitanguliwa na ule wa Bodi ya Ligi (TPL-Board), Oktoba 25.
Kabwe, mbunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliandika jana katika ukurasa wake wa kijamii (Twiter), kuwa, yeye ni mdau mkubwa wa michezo hususan soka hapa nchini, hivyo atahakikisha Malinzi anakalia kiti hicho.
Aidha, Kabwe alisema kutokana na hilo atahakikisha kwa gharama yoyote Malinzi anachukua kiti cha Rais anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga.
Katika hatua nyingine, Malinzi ameahidi, endapo atafanikiwa kuwa Rais wa Shirikisho hilo, atafanya mambo makubwa ya kuinua soka ya Tanzania ambayo inashuka kila siku katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kwa kujikita katika soka ya vijana, ambao ni hazina ya baadaye.
Source:Tanzania Daima