Zitto Kabwe ajisalimisha polisi

Zitto Kabwe ajisalimisha polisi

Mzee wa majipu anaanza kuchezea katiba, amevunja nyumba za walalahoi tumekaa kimya amesababisha bei ya sukari na vitu vingine kupanda tumekaa kimya sasa ameanza kukandamiza upinzani, hili hatutakubali
Umenena vema mkuu...na kuna watu wanamchochea afanye ayafanyayo ili watu wengi Zaidi wamchukie
 
Naona Zitto anataka kuurudisha upinzani uliopotea kwa miaka mingi.
 
Sema hukubari
Unajificha nyuma ya Id fek kisha unaanza kuroha kama umepandwa na mashetani
Safari ndio kwanza imeanza na hakuna serikali yoyote iliyoshinda vita ya unguvu ya umma
 
Zito anatafutwa na polisi lawama kwa Rais zinatoka wapi? Kwani huyo Zito ndiyo anaanza kukamatwa na polisi katika harakati zake za siasa?
Wacha kudanganya watanzania, kwani hao polisi hawakujui makao makuu ya act?
 
Nimegundua Lowasa alikuwa mtu sahihi kwa Tz najuta kutomsapoti wakati wa uchaguzi yule ndiye alikuwa rafiki wa kweli wa wanyonge
Mkuu kufanya kosa siyo kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa,2020 mpatie kura yako lowasa na wabunge na madiwani wake ili tuikatae ccm kistaarabu
 
Wewe unasema nini, hakuna cha moto wala nini, lazima serikali iwawadabishe mpaka mtakapojifunza kutii sheria
Ubabe siku zote hauzai mema. Kumbuka hata kwenye familia yako tu ukiwa mkali na mbabe mwisho wake ni familia kuharibika. watoto watakuwa na heshima na nidhamu ya woga sababu ya ukali wa baba, Mke naye atakuogopa huwezi kukaa na familia yako kujadili mambo mazuri ya kujenga familia yako. Baadaye watoto wakikua ndo utaona misuguano kati ya baba na watoto. Nadhani kwa ulimwengu wa sasa hivi ubabe siyo njia ya kuongoza. Mbona Mh. Rais alikuwa kisha jenga imani kubwa kwa watanzania? Kuwakandamiza wapinzani wake kisiasi sioni kama ni njia sahihi.
 
Kwa mbali naona picha,lakini itaonekana vizuri
kama tashwira yake ikigeuzwa au uiangalie kupitia Maji.
 
Bonge limekuwa kama mihadarati mkuu linaendeshwa gizani na bajeti inajadiliwa na upande unaotakiwa tu chini ya dola.
 
Amani ....Amanii.....huu Mwezi mtukufu.....tusubiri umalizike...mwezi wa kuomba mema...tuutumie vuzuri...tusiombe mabaya.Wahusika fanyeni subra na tafuteni suluhu.
Amani ya Taifa ndio kila kitu
 
Back
Top Bottom