Zitto Kabwe afanya Mapinduzi Kigoma Mjini

Zitto Kabwe afanya Mapinduzi Kigoma Mjini

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
TUNAKUPONGEZA SANA MBUNGE WETU PEKEE KUPITIA CHAMA CHA ACT Wazalendo KWA KAZI KUBWA UNAYOIFANYA KATIKA JIMBO LAKO.

"Katika kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani Kigoma, Manispaa ya Kigoma Ujiji ina mkakati wa kuhuisha mji wa Ujiji Kwa kuimarisha soko la Ujiji na Bandari ya Ujiji.

Soko la Ujiji lina Mradi maalumu wa kujenga Kituo cha Kikanda cha Biashara ( trading and logistical center - Ujiji City Project ).

Mradi huu utakaotokana na uwekezaji kutoka nchini China utawezesha ujenzi wa maduka 3000, Warehouses na nyumba za makazi.

Lengo la Mradi huu ni kuwezesha Ujiji kuwa eneo ( a Hub ) la wananuzi wa bidhaa kutoka Nchi za Maziwa Makuu badala ya watu hao kusafiri kwenda Mashariki ya mbali.

Leo nilikutana na Balozi wa China nchini Tanzania ili kufuatilia Kwa karibu Mradi huu pamoja na miradi mingine ambayo wawekezaji wa China wanawekeza nchini kwetu. Kigoma ni mkoa wa biashara.

Ujiji ni mji wa biashara. Tunataka kuirudishia Ujiji hadhi yake hiyo ya toka karne ya 16.

Zitto Kabwe

Mbunge Kigoma Ujiji "​
 
Mkuu ACT Wazalendo, hii thread yako bado haijakaa vizuri! , Intro para, umeianza vizuri kwa kuonyesha wewe ni mtu baki, nafsi ya pili kuonyesha ni someone else anampongeza mbunge pekee wa ACT, kwa kazi nzuri anayefanya kwa mji wa Kigoma Ujiji! .

Then ilipokuja "leo nimekutana. ..

Mwisho ni Zitto. Huwezi kuanza as someone else na kisha kumaliza as Zitto.

Ama anza as Zitto na kumaliza as Zitto au anza as someone else na kumaliza as someone else! .

All and all, hongera sana Mbunge pekee wa ACT, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe.

Pasco
 
Zitto, kwa weledi wako uzi huu umeboronga ktk uandishi, hongera kwa mipango yako ktk uwekezaji!
 
Kwahiyo Ujiji itakua Godown la bidhaa za China?
Kwanin hao wachina wasijenge viwanda huko?
 
Muwe mnamalizia vichwa vya habari ,wengine mtatuua na presha ...hebu malizia ni mapinduzi ya nini
It is true.

Hivyo vichwa vya habari vingine ni shidaaa......

Nami nilidhani Zitto amefanya Mapinduzi ya kumpindua yule mama Mghwira.........
 
Hongera kwa kufunguka. ..chapa kazi sio bla bla tu....hapa kazi tu!
 
Mbona kama mwandishi kaeleza tofauti na kichwa cha habari?
 
Ukikamilisha mradi huu ndio ntakupongeza. Maana huwa unaanzisha halafu unaishia mitini? Vipi kuhusu ecotourism mwamgongo,? Wale wazungu ulioeatelekeza wanaendelea?
 
Ukikamilisha mradi huu ndio ntakupongeza. Maana huwa unaanzisha halafu unaishia mitini? Vipi kuhusu ecotourism mwamgongo,? Wale wazungu ulioeatelekeza wanaendelea?
we umekamilisha upi?

wewe ni mkosoaji...haujawahi kuwa original ili ukosolewe

bisha!
 
TUNAKUPONGEZA SANA MBUNGE WETU PEKEE KUPITIA CHAMA CHA Act Wazalendo KWA KAZI KUBWA UNAYOIFANYA KATIKA JIMBO LAKO.

"Katika kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani Kigoma, Manispaa ya Kigoma Ujiji ina mkakati wa kuhuisha mji wa Ujiji Kwa kuimarisha soko la Ujiji na Bandari ya Ujiji.

Soko la Ujiji lina Mradi maalumu wa kujenga Kituo cha Kikanda cha Biashara ( trading and logistical center - Ujiji City Project ).

Mradi huu utakaotokana na uwekezaji kutoka nchini China utawezesha ujenzi wa maduka 3000, Warehouses na nyumba za makazi.

Lengo la Mradi huu ni kuwezesha Ujiji kuwa eneo ( a Hub ) la wananuzi wa bidhaa kutoka Nchi za Maziwa Makuu badala ya watu hao kusafiri kwenda Mashariki ya mbali.

Leo nilikutana na Balozi wa China nchini Tanzania ili kufuatilia Kwa karibu Mradi huu pamoja na miradi mingine ambayo wawekezaji wa China wanawekeza nchini kwetu. Kigoma ni mkoa wa biashara.

Ujiji ni mji wa biashara. Tunataka kuirudishia Ujiji hadhi yake hiyo ya toka karne ya 16.

Zitto Kabwe

Mbunge Kigoma Ujiji "​
Lakini Mbagala Zakhem wanakusubiri umshitaki Dr Tulia kwa kufuta TV live? Wanakusubiri Makumbusho pia kuichambua bajeti. Uvinza Ujiji utapata muda kweli.
 
Pasco bhana...Sasa sijui ni wivu wako tu uliyoandika au umezingatia tu weledi.Nimecheka sana
 
Pasco bhana...Sasa sijui ni wivu wako tu uliyoandika au umezingatia tu weledi.Nimecheka sana
Mkuu Ben, wivu wa nini?!. Bahati nzuri nimetoka, lile kabila ambalo hatunaga wivu kabisa!. Mimi mwenyewe baada ya ndoa na kufyatua wawili, nilimruhusu wife kwenda US kupiga shule ya miaka 4!. Mtu mwenye wivu angeruhusu? !.

Tatizo la kabila letu kutokuwa na wivu kunatuponza hadi kukosa wivu wa Maendeleo! . Unakuta mtu ana ng'ombe elfu, wake 6, watoto 18!, Nyumba ya nyasi! ,watoto haeaendi shule!, usafiri ni baiskeli ya baba! . Starehe ni kutembea na radio ukisikiliza RTD! .

Pasco
 
Back
Top Bottom