PreGE2025 Zitto Kabwe achukua Fomu ya Ubunge Kigoma Mjini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, leo Jumapili amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama hicho.

IMG_4613.jpeg
Zitto amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Jimbo, Ndugu Idd Adam, katika tukio lililoshuhudiwa na wafuasi na viongozi wa chama hicho.

IMG_4612.jpeg
Tukio hili linakuja siku moja baada ya kufanyiwa maombi maalumu na wanakwaya wa Kanisa la Moravian Kigoma, na leo asubuhi alifanya ziara ya kimya kimya katika makaburi ya Rubengela ambako mama yake mzazi, Hajjat Shida Salum, amezikwa. Aidha, kinamama wa Kigoma mjini walimfanyia dua maalum katika Zawiya za wanawake kama sehemu ya kumuombea baraka katika safari yake ya kisiasa.

IMG_4614.jpeg
Katika kuonesha mshikamano na hamasa, zaidi ya wanawake 600 kutoka matawi yote 72 ya ACT Wazalendo Kigoma Mjini walitembea naye kwa umbali wa kilomita mbili kutoka Ofisi ya ACT Wazalendo Mkoa iliyoko Rubuga Ujiji hadi Ofisi za Jimbo Buzebazeba.

IMG_4615.jpeg
Akizungumza baada ya tukio hilo, Zitto alisema, "Ilikuwa ni shughuli ya Wanawake wa Mji kwa heshima ya mwenzao ‘Da Shida’. Ninaukabidhi mchakato mzima wa mimi kurejea Bungeni kwa Wanawake wa Mji wa Kigoma Ujiji. TUTASHINDA KWA KUPAMBANA!"

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Zitto Kabwe aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa vipindi viwili na sasa anarejea kwenye kinyang’anyiro akijivunia sapoti kubwa ya wanawake wa Kigoma.
 
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, leo Jumapili amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama hicho.

Zitto amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Jimbo, Ndugu Idd Adam, katika tukio lililoshuhudiwa na wafuasi na viongozi wa chama hicho.

Tukio hili linakuja siku moja baada ya kufanyiwa maombi maalumu na wanakwaya wa Kanisa la Moravian Kigoma, na leo asubuhi alifanya ziara ya kimya kimya katika makaburi ya Rubengela ambako mama yake mzazi, Hajjat Shida Salum, amezikwa. Aidha, kinamama wa Kigoma mjini walimfanyia dua maalum katika Zawiya za wanawake kama sehemu ya kumuombea baraka katika safari yake ya kisiasa.

Katika kuonesha mshikamano na hamasa, zaidi ya wanawake 600 kutoka matawi yote 72 ya ACT Wazalendo Kigoma Mjini walitembea naye kwa umbali wa kilomita mbili kutoka Ofisi ya ACT Wazalendo Mkoa iliyoko Rubuga Ujiji hadi Ofisi za Jimbo Buzebazeba.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Zitto alisema, "Ilikuwa ni shughuli ya Wanawake wa Mji kwa heshima ya mwenzao ‘Da Shida’. Ninaukabidhi mchakato mzima wa mimi kurejea Bungeni kwa Wanawake wa Mji wa Kigoma Ujiji. TUTASHINDA KWA KUPAMBANA!"

Zitto Kabwe aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa vipindi viwili na sasa anarejea kwenye kinyang’anyiro akijivunia sapoti kubwa ya wanawake wa Kigoma.
Huyu ndiye mrudisha nyuma jitihada na kuleta mabadiliko ya kiuongozi nchi hii
 
Makubwa
Hivi huyu kawaje jmn?
Ndo huyuhuyu zitto wa kipindi kile?
 
Watamkata kuwa hajui kusoma na kuandika.
 
Msimlaumu jamani kitaa kigumu sana akiwa nje ya ubunge anapoteza connection za ulaji🤔😅🤣
 
inawezekana kajihakikishia ushindi.....na abadani hatokatwa lengo ni kurekebisha joto na fukuto la wanaodai vifungu vya tume huru virekebishwe
 
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, leo Jumapili amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama hicho.
View attachment 3324377
Zitto amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Jimbo, Ndugu Idd Adam, katika tukio lililoshuhudiwa na wafuasi na viongozi wa chama hicho.
View attachment 3324378
Tukio hili linakuja siku moja baada ya kufanyiwa maombi maalumu na wanakwaya wa Kanisa la Moravian Kigoma, na leo asubuhi alifanya ziara ya kimya kimya katika makaburi ya Rubengela ambako mama yake mzazi, Hajjat Shida Salum, amezikwa. Aidha, kinamama wa Kigoma mjini walimfanyia dua maalum katika Zawiya za wanawake kama sehemu ya kumuombea baraka katika safari yake ya kisiasa.
View attachment 3324379
Katika kuonesha mshikamano na hamasa, zaidi ya wanawake 600 kutoka matawi yote 72 ya ACT Wazalendo Kigoma Mjini walitembea naye kwa umbali wa kilomita mbili kutoka Ofisi ya ACT Wazalendo Mkoa iliyoko Rubuga Ujiji hadi Ofisi za Jimbo Buzebazeba.

View attachment 3324382
Akizungumza baada ya tukio hilo, Zitto alisema, "Ilikuwa ni shughuli ya Wanawake wa Mji kwa heshima ya mwenzao ‘Da Shida’. Ninaukabidhi mchakato mzima wa mimi kurejea Bungeni kwa Wanawake wa Mji wa Kigoma Ujiji. TUTASHINDA KWA KUPAMBANA!"

Zitto Kabwe aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa vipindi viwili na sasa anarejea kwenye kinyang’anyiro akijivunia sapoti kubwa ya wanawake wa Kigoma.
Zito ni kiongozi mjinga na mbinafsi sana.
 
Aliyewahi kuwa Kiongozi mkuu wa Act Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amechukua fomu ya kugombea ubunge
Ni baada ya kuahidiwa na Mh. Rais Samia Sulluhu Hassan kuwa endapo atagombea atatangazwa mshindi hata kama ccm itashinda nafasi hiyo ya Ubunge.
 
Hilo umelijua je?
 
Back
Top Bottom