WABHEJASANA
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 4,225
- 869
Wakuu Habari za Krismas jana?,najua kwa sasa wengi wanfungua zile zawadi za jana!!!!!!!!
Kuna jambo ambalo nimelifikiria kwa muda mrefu sana tangu yalipoanza malumbano humu Jamvini juu ya Zitto na masalia yanavyofanya mkakati wa kumchafua Dr.Slaa Thread nyingi nilizosoma juu ya kilichoibuka nikabaini kuna kushambuliana kwa hali ya juu na inavyoonekana ni jambo ambalo watu walik na kujipanga namna ya kufanya mashambulizi.
Maoni ya wachangiaji wengi ambao wamekuwa wakichangia kwenye Thread hizo wamekuwa wakizungumzia sual la ukabila wakifikia hadi hatua ya kulitaja kabila la wachaga kwamba ndilo linalomsakama Zitto eti kwa sababu Muasisi wa CHADEMA anatokana na kabila hilo hivyo wanamhitaji Dr Slaa kwa sababu naye anatokea ukanda huo pamoja na kwamba yeye si Mchaga.
Kwanza sitaki kuamini saana hili suala la ukabila na hata kama lipo kwa namna yoyote ile binfasi kwa maoni yangu naona haliwezi kuathiri utendaji kazi wa Zitto wala Dr.Slaa kwa sababu siku zote naamini kwamba unapoona unaandamwa na matatizo utambue kwamba kuna furaha mbeleni kwa hiyo binafsi naichukulia kama sehemu ya mapito ya zitto pamoja na Dr Slaa katika mafanikio.
Anayoyapata Zitto hivi sasa ndani ya chama chake hayana tofauti na anayoyapata Dr Slaa kutoka ndani ya CCM na ndiyo maana utaona kila siku kunakuwepo na hoja zinazojaribu kumchafua Slaa ama aonekane hafi katika jamii,ama basi wajaribu kupunguza mvuto wake kwa jamii.
Kwa maoni yangu na kwa mujibu wa uchunguzi wangu,CCM inamuhofia sana Dr Slaa na hasa endapo atawania Urais mwaka 2015 na hili halina ubishi kwamba Slaa ni mtu ambaye anapendwa na watanzania walio wengi na hii inatokana na hazina kubwa aliyoiweka miaka mingi katika kutetea rasilimali za watanzania ndiyo maana leo hata ukisema nini watu hawawezi kukuelewa juu ya Slaa na pamoja na kwamba kuna mambo yanyogusa lakini watu wanachukulia kama sehemu ya ubinadamu kwa sababu na yeye ni binadamu anayetumia Damu,maji na Nyama.
Kinachonishangaza na kuniumiza ni hili ambalo linaonekana kuibuka ndani ya CHADEMA yenyewe ambayo sasa imeanza kuchafuana wao kwa wao,kwa sababu ni uwazi wa kweli kwamba ndani ya CHADEMA hivi sasa kuna makundi mawili kundi la kwanza likiwa ni la Zitto na la pili likiwa ni la Dr Slaa ambalo kila moja linahofia mwenzake katika suala la Urais na ndiyo maana utaona kuna mambo ya ajabu ajabu ambayo yanaendelea kutokea kama ambavyo tunashuhudia mengine humu JF.
Yawezekana kweli kundi la Dr Slaa linafanya kila jitihada za kuhakikisha kwamba linalidhoofisha kundi la Zitto lakini pia huenda kundi la Zitto nalo linafanya jitihada za kulidhoofisha kundi la Dr Slaa ili liweze kupata nafasi,lakini ukweli ulio wazi ni kwamba hili jambo ni la hatari sana na hapa napenda niseme wazi kwamba huu ndio mwanzo wa chama kugawanyika na mwisho wa siku hata kama kilikua na asilimia kubwa ya kuing'oa CCM madarakani lazima asilimia hizo zitapungua tena kwa kiwango kikubwa jambo ambalo naona kwamba linaweza kuipa nafasi tena CCM kuitawala nchi hii.
Hakuna ubishi kwamba Zitto anakubalika na anao wafuasi wengi na hasa ukanda wa Ziwa ambao hakuna ubishi kwamba una watu wengi,lakini Slaa naye ana kundi kubwa ingawa kwa kiwango kikubwa anaonekana kuungwa mkono zaidi na watu kutoka kaskazini ambao ukiangalia idadi yake si kubwa kama ile ya Ziwa,kwa hiyo kinachokuja kutokea hapa ni kwamba zitabaki zile kanda za kusini,kati na mashariki ambapo huko itategemea nani mwenye mvuto zaidi na kwa vyovyote ni lazima watagawana ingawa kuna mshindi lazima tapatikana bila kujali ni Zitto ama Dr Slaa.
OMBI LANGU:Kuna kila sababu ya hizi pande mbili kukaa chini na kuumaliza huu mgogoro na aina yoyote ya kuwatimua ama kuwasimamisha watu wa kundi fulani ni kutengeneza bomu lingine kubwa ambalo linaweza kuwalipua watu wengi zaidi,jamani tukumbuke hii ni vita ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu,vinginevyo mnaweza kukaa mnapigana ndani kwa ndani mwisho linakuja jamaa linanawateka wote na kuwa baba wa mji na ninyi mnabaki kuwa wajakazi wake.
Tukumbuke kwamba waswahili walisema "Vita vya Panzi,furaha ya Kunguru" Msemo huu una maana kubwa sana.
Naomba kuwasilisha na Tudadavue kwa nia ya kujenga.