CV ya Zitto mbele ya Wananchi iko wazi, Propaganda za Akina Mbowe zimeshindwa kuushawishi Umma kwamba zitto ni mkosaji. Hoja ya madini ya Buzwagi ilimfanya Zitto awe kipenzi cha Raia kwenye miji ya madini kama kule Geita n.k
Hoja ya Kumn'goa Waziri mkuu imemfanya awe kipenzi cha Raia wengi wa mikoa ya Kusini, mtwara Lindi, n.k
Hoja ya manufaaa ya Hifadhi ya jamii kwa mkulima imemfanya awe kipenzi cha Wakulima wengi nchini.
Hoja ya Mapesa yaliyofichwa Uswis imemfanya awe kipenzi cha walalahoi mitaani.
Uwezo wake wa kukata Ishu na kuzielezea nje na ndani ya Bunge umemfanya kuwa kipenzi cha Wasomi
Historia yake ya kuwa miongoni mwa wanasiasa wachache kuanzia siasa katika upinzani na kuendelea kuwa mpinzani bila ya kuhama hama vyama Kumemfanya aonekane ni Mpinzani halisi.
SASA UKIWA NA MOYO WA HUSDA HUWEZI KUONA POTENTIAL YA HUYU MTU, HUYU ALIFAA AWE GROOMED NA CHAMA ILI KUKIPEPERUSHA CHAMA VYEMA, SIYO KUMUWEKEA VIKWAZO NA KUMPIGA NGWALA ZA KISIASA.
WANACHOKIFANYA CHADEMA SASA NI KAMA VILE MCHAWI, ANAROGA ILI UKOSE, BADALA YA KUROGA ILI YEYE APATE!