Kama kuna wakati ambao Viongozi Wahifadhina ndani ya Chadema wamewahi kuchanganyikiwa basi ni wakati huu ambao umeibuka mtafuruku mkubwa miongoni mwa Makada wake.Mtafuruku huu unawahusisha akina Zitto Z. Kabwe kwa upande mmoja na Mwenyekiti pamoja na Katibu Mkuu kwa upande mwingine.Sintofahamu hii imezuka kufuatia kuvuja kwa nyaraka kadhaa katika mitandao ya Kijamii zikimshambulia Mwenyekiti Mbowe pamoja na aliyekuwa N/Katibu Mkuu Zitto ikifuatiwa na kuvuliwa kwake nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama.Kinachoendeleasasa ni mwendelezo wa mpambano wa kisiasa baina yao.Kwa kiasi kikubwa Mwenyekiti na mshirika wameonekana kutishwa sana mara baada ya Zitto kuamua kujibu mapigo kwa kuitisha mikutano ya hadhara na kupata mapokezi mazuri sana.Zitto ameamua kuwaambia Watanzania ukweli wa kinachoendelea ndani ya Chama,Dr Slaa ametishika na kuamua kumtisha Zitto lakini Zitto ameapa kwamba haogopi na anapanga kuzunguka Tanzania nzima kusema ukweli wa mambo juu ya hawa Wahifadhina.Ujasiri huu wa Zitto umewachanganya sana.