Zitto decides to take a BULL by the horns!!!

TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
553
Kama kuna wakati ambao Viongozi Wahifadhina ndani ya Chadema wamewahi kuchanganyikiwa basi ni wakati huu ambao umeibuka mtafuruku mkubwa miongoni mwa Makada wake.Mtafuruku huu unawahusisha akina Zitto Z. Kabwe kwa upande mmoja na Mwenyekiti pamoja na Katibu Mkuu kwa upande mwingine.Sintofahamu hii imezuka kufuatia kuvuja kwa nyaraka kadhaa katika mitandao ya Kijamii zikimshambulia Mwenyekiti Mbowe pamoja na aliyekuwa N/Katibu Mkuu Zitto ikifuatiwa na kuvuliwa kwake nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama.Kinachoendeleasasa ni mwendelezo wa mpambano wa kisiasa baina yao.Kwa kiasi kikubwa Mwenyekiti na mshirika wameonekana kutishwa sana mara baada ya Zitto kuamua kujibu mapigo kwa kuitisha mikutano ya hadhara na kupata mapokezi mazuri sana.Zitto ameamua kuwaambia Watanzania ukweli wa kinachoendelea ndani ya Chama,Dr Slaa ametishika na kuamua kumtisha Zitto lakini Zitto ameapa kwamba haogopi na anapanga kuzunguka Tanzania nzima kusema ukweli wa mambo juu ya hawa Wahifadhina.Ujasiri huu wa Zitto umewachanganya sana.
 
Hawezi kuiongoza NCHI ni MKABILA na MDINI HUYO --- NYERERE alituonya na KIONGOZI kama HUYO...

Sasa Yalimtokea Mbunge wa NZEGA ROSTAM Aziz -- Yeye alikuwa MHINDI na ISMAILIA kwahiyo hakuwa KABILA la Watu wa NZEGA na DINI YAO kwahiyo Alivyojiondoa Hakuweza kwenda HUKO NZEGA kujitetea kama ZITTO KABWE anavyojizungusha NCHINI

Sasa Mfano MWINGINE Uumtokee MBUNGE wa SINGIDA MJINI - DEWJI ni MHINDI na DINI TOFUATI hayo yakimtokea ni yeye kufungasha na kuondoka hata weza kwenda JIMBONI na kuzunguka kama ZITTO KABWE Is that a DEMOCRACY?
NOT AT ALL

NDIO MAANA NYERERE alikataa UDINI na UKABILA KUCHAGUWA WAGOMBEA UONGOZI NCHINI...

ZITTO KABWE ANGEPASWA KUKEMEWA lakini serikali yetu imelala inaotesha masuala haya ili ishinde 2015 haijui kuwa watakaoshinda 2015 Ndani ya CCM pia watatumia vigezo hivyo dhidi ya wenzao ndani ya CCM na hivyo NCHI IMEPASUKA

NA HAKUNA SASA HIVI MTANZANIA MWENYE HEKIMA anayeelewa CHOCHOTE... AKILI ZIMEPUNGUA... HATUONI MBALI TENA
 
Leo Zitto Kabwe ni mkabila na mdini!

Siku tukiwachoka kina Mbowe tutayatamka pia haya.

Ni style za kumshindwa mtu kwa hoja.

CCM pia wanaisemaga hivi hivi CDM pale wanaposhindwa kujibu hoja.
 
Hawa wanaomvika kilemba cha ukoka ndo wamemwaribia mpaka hapa dogo bichwa limevimba babu kubwa, na laiti angejua kamwe Nazi haishindni na jiwe angeelewa ni nini maana na tafsiri ya anachokifanya kwa watu wenye uelewa wa kutosha,hauwezi ukaidharau KK ya chama chako kiasi hicho cha kufika kuwaandaa walevi waje kuhujumu mikutano ya Katibu mkuu alafu ukafikiri wewe bado ni mwema,hata ukiamua kukata rufaa pia kwanza haiwezi kusomwa tena kama mkata rufaa mwenyewe ni wa hivi,sasa utaulizwa ulikata rufaa ya nini?
 
CV ya Zitto mbele ya Wananchi iko wazi, Propaganda za Akina Mbowe zimeshindwa kuushawishi Umma kwamba zitto ni mkosaji. Hoja ya madini ya Buzwagi ilimfanya Zitto awe kipenzi cha Raia kwenye miji ya madini kama kule Geita n.k

Hoja ya Kumn'goa Waziri mkuu imemfanya awe kipenzi cha Raia wengi wa mikoa ya Kusini, mtwara Lindi, n.k
Hoja ya manufaaa ya Hifadhi ya jamii kwa mkulima imemfanya awe kipenzi cha Wakulima wengi nchini.
Hoja ya Mapesa yaliyofichwa Uswis imemfanya awe kipenzi cha walalahoi mitaani.
Uwezo wake wa kukata Ishu na kuzielezea nje na ndani ya Bunge umemfanya kuwa kipenzi cha Wasomi
Historia yake ya kuwa miongoni mwa wanasiasa wachache kuanzia siasa katika upinzani na kuendelea kuwa mpinzani bila ya kuhama hama vyama Kumemfanya aonekane ni Mpinzani halisi.

SASA UKIWA NA MOYO WA HUSDA HUWEZI KUONA POTENTIAL YA HUYU MTU, HUYU ALIFAA AWE GROOMED NA CHAMA ILI KUKIPEPERUSHA CHAMA VYEMA, SIYO KUMUWEKEA VIKWAZO NA KUMPIGA NGWALA ZA KISIASA.
WANACHOKIFANYA CHADEMA SASA NI KAMA VILE MCHAWI, ANAROGA ILI UKOSE, BADALA YA KUROGA ILI YEYE APATE!
 
Kinachoendelea sasa ni upuuzi wa kupumbaza watu kuficha ukweli wakati huo huo kuzorotesha harakati za mabadiliko kwa maslahi ya wachache wenye malengo yao! Zito ni mtu makini sidhani kama ana wasemaji wengi kiasi hiki wa kumpikia mawazo na kumjazia schedule ambazo huenda hata yeye mwenyewe hazijui...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom